Eneo la tukio la moto soko la Kigoma Kibanda namba 16A.
Kaimu kamanda wa mkoa wa Kigoma SSP, Kihenya Kihenya kushoto na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya wakikagua ajali ya moto uliotokea katika soko hilo.
 Kikosi cha zima moto waki wamefaulu kudhibiti moto
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibwa akitazama juhudi za askari Polisi na zima moto za kuokoa na kufanikiwa kuzibiti moto.
 OC CID ASP Mohamed Kilonzo wa Kigoma mjini (kushoto).
Polisi Wakidhibi wananchi ili upote wa mari usitokee.

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limefanikiwa  kuzuia na kuokoa  mali  na kudhiti moto kwa kushirikiana na askari zima Moto wa kikosi cha zimamoto Halmashauri ya Kigoma Ujiji na Kikosi cha zimamoto viwanja vya Ndege.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP, Kihenya Kihenya amemtaja mmiliki wa duka hilo kuwa ni Faustine  Samweli 39, Mfanyabiashara wa Lumumba  Road chumba NO.16 kiliungua moto.

Kaimu Kamanda  amesema kuwa  Chanzo cha moto huo ni Freezer iliyokuwa imeachwa ikiwaka usiku mzima bila kuzimwa hivyo kusababisha chanzo cha moto huo.

Kamanda huyo amesema kuwa Thamani halisi ya mali iliyoteketea bado haijajulikana  na uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea.

Hata hivyo Kamanda, Kihenya amewataka wafanya biashara wa eneo hilo kuhakikisha usalama wa mali zao kabla na baada ya kufanya shughuli zao kuwa waangalifu wakati wa ufungaji wa maduka yao ili kuzuia tukio la aina hiyo.

Picha/Habari: NA PARDON MBWATE WA JESHI LA POLISI KIGOMA
NA ANAMARIA MASIKA WA JESHI LA POLISI KIGOMA
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: