Weweeee! usinipige picha... hapa alikuwa akimfukuza mwandishi na ndipo mwandishi alipotafuta chimbo kujificha na kunasa tukio zima.
Picha liliendelea kwa askari huyu wa Jiji la Dar es Salaam alipomkuta mama huyu amesimama pembezoni mwa jengo la IPS jijini Dar na kuanza kumfokea pindo alipomuomba kidogo dogo ili asimfikishe ofisini kwao.
Mazungumzo ya kupata kidogo dogo yaliendelea...
...askari huyo baada ya kumaliza mazungumzo na mama aliyekuwa kwenye gari ndipo alipoangalia kulia na kushoto kama kuna mtu alikuwa anamtizama bila kujua kamera ya Habari na Matukio ilikuwa kazini ikifanya kazi yake.
... Baada ya kumalizia mazungumzo alichukua kidogo dogo kwa staili ambayo si rahisi mtu kujua alichokuwa akifanya. Mambo kama haya ndiyo wanayoyafanya askari hawa wa jiji la Dar kwa kunyanyasa wananchi hasa akina mama pindi wanapowakuta wamepaki vibaya magari yao. Lakini jambo la kushangaza kwa nini magari hasa ya viongozi/serikali yakipaki hayasumbuliwi.
...baada ya kuwa amekula kidogo dogo kutoka kwa mwanamama na kumuachia akaondoka, zilipita dakika 3 tu ndipo lilipokuja gari lililokuwa limeandikwa Wizara ya Kazi na Ajira (W KA), na kupaki ila hawakulifanya lolote.


Hii hatari jamani??!!
ReplyDeleteDuuuh jamaa anatia huruma kwny hiyo picha alivokua anamfukuza cameramen!!kila mtu na uwanja wake nae anatafuta ugali wa watoto.
ReplyDelete