Katibu mkuu wa Wizara ya fedha Mr Ramadhani Khijjah kushoto akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya wizara hiyo jijini Dar es salaam wakati wa kutiliana saini mkataba kwa shilingi Bilioni 102.3 kwa ajili ya kuendeleza kupanua viwanja vya ndege nchini Tanzania, (kulia) Kurt Simonsen Mkuu wa benki ya European Investment Bank kanda ya Afrika Mashariki.
Mkuu wa benki ya European Investment Bank kanda ya Afrika Mashariki Bw. Kurt Simonsen akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya Wizara Fedha jijini Dar es salaam wakati wa kutiliana saini mkataba kwa shilingi Bilioni 102.3 kwa ajili ya kuendeleza kupanua viwanja vya ndege nchini Tanzania, (kushoto ni Katibu mkuu wa Wizara ya fedha Mr Ramadhani Khijjah.
Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Bw. Ramadhani Khijjah kushoto na Kurt Simonsen Mkuu wa benki ya European Investment Bank kanda ya Afrika Mashariki, wakibadilisha hati za mikataba mara baada ya kutiliana saini leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania Suleiman Suleiman, akijaribu kufafanua jambo wakati hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuendeleza viwanja vya ndege nchini Tanzania. Ambapo viwanja vya ndege vitakavyoendelezwa vya mikoa ya Kigoma, Tabora, Bukoba, Shinyanga na Sumbawanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments: