Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Aman mjini humo.
  Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akipunga mkono kwa waandamanaji waliokuwa wakipita mbele ya jukwaa kuu wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika leo Uwanja wa Aman mjini Zanzibar .
  Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Shariff Hamad.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali wakiwa jukwaani Uwanja wa Amani katika Sherehe hizo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri, Mama Zakhia Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, wakiwa katika sherehe hizo.
Kutoka (kulia) Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri, Mama Asha Bilal,Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, Jaji Mkuu, Othman Chande na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakiwa katika sherehe hizo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa jukwaani wakati ukipigwa wimbo maalum wa Taifa wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akikagua gwaride maalum wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Vijana wakipita kwa maandamano na mabango mbele ya Jukwaa Kuu.
Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakipita mbele ya Jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni rasmi.
Kikosi cha Polisi Wanawake wakipita mbele ya Jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni rasmi.
Kikosi cha kutuliza ghasia FFU, kikipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa haraka na kutoa heshima kwa Mgeni rasmi.
Kikosi cha Wanajeshi waenda kwa miguu, kikipita mbele ya Jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni wa rasmi. Picha na IKULU NA OMR.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: