Baadhi ya wanenguaji wa THT wakikamua stejini.
Godzila alipoteza ajabu.
Wasanii wanawakilisha kundi la Makomandoo kutoka THT wakiwajibika mari hapo.
Young Dee akicheza na jukwaa namna hii.
Msanii wa Top Band, Ommy Dimpoz akitumbuiza kwa hisia kali huku akiwa amemkamatia mbwa wake jukwaani hapo.
Baadhi ya mashabiki waliofurika mahali hapo.
MPANGO mzima jana ulikuwa ndani ya Tamasha la XXL Afta Skui Bash 2011, lililofanyika katika Ufukwe wa Mbalamwezi Mikocheni, Dar es Salaam ambapo umati ulijitokeza kujumuika katika kufanikisha sherehe za likizo ya masomo kwa mwaka huu.
Tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka na kuandaliwa na Kampuni ya Clouds Media Group kupitia kipindi cha XXL, lilifana vilivyo huku wasanii kibao wakali wakishambulia jukwaa vilivyo.
Baadhi ya wasanii walikonga mioyo ya mashabiki ni Godzilla, Young Dee, AT, Ommy Dimpoz, Bob Junior, Linex, Ditto, Mataluma, Hemedy Suleiman, Stamina, Shetta, Amini, Makomandoo, THT Dances na chipukizi kibao.
Katika tamasha hilo, pia kulifanyika michezo mbalimbali kama mashindano ya kucheza muziki, urembo, kufananisha sura na staa na kumatafuta Mr & Miss XXL 2011.

Toa Maoni Yako:
0 comments: