Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa akipata maelezo kuhusu Idara na Taasisi za Ofisi ya Waziri Mkuu zilizoshiriki katika maonesho ya Miaka 50 ya Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Habari Elimu na Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. David Kirway alipotembelea Banda hilo katika Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akitoa maelezo kuhusu masuala ya Maafa kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika maadhimisho ya Kitaifa ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere vilivyopo Kilwa Dar es Salaam.
 Bw. Martin Masaly Afisa Mtafiti wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) akitoa maelezo kuhusu kazi na masuala ya uwekezaji Tanzania kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa alipotembelea banda hilo. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mtafiti Bw. Martin Masalu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
 
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa (Katikati) akipokea maelezo ya Uwekezaji na Uwezeshaji kutoka kwa Bw. Suleiman Malela Mkaguzi wa Ndani wa Baraza la Uwekezaji Wananchi Kiuchumi, alipotembelea banda hilo. Kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Malecela akinunua Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu katika maadhimisho ya Kitaifa ya MIaka 50 ya Uhuru yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. J.K Nyerere vilivyopo Kilwa Dar es Salaam. Kushoto ni Mpigachapa  Bibi. Joyce Benjamin wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: