Sakata la kumtaka mwenyekiti wa Chama cha NCCR – MAGEUZI Taifa Bw. James Mbatia kutakiwa ajiuzulu na baadhi ya wanachama,limechukua sura mpya baada ya Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini kupitia chama hicho Moses Machali kusema haungi mkono hoja hiyo na kuuita  uamuzi huo kuwa ni wa kipuuzi na kama wanaosambaza hoja hiyo watafanikiwa basi yeye atajiuzulu nafasi ya ubunge na kuachana kabisa na shughuli za siasa nchini.

Mbunge Machali alisema hayo mbele ya waandishi wa habari mjini Dodoma. Ripota wa Kajunason Blog anaturushia hii... Hebu msikilize mwenye Mheshimiwa Mbuge akiongea... 
Bw. Machali pia alisema kundi linaloongozwa ma Mbunge wa Kigoma Kusini Bw. David kafulila ndilo linaloharibu hali ya utulivu katika chama cha NCCR-MAGEUZI akidai kuwa Bw. Kafulila anautamani Uwenyekiti wa Chama Taifa. 

Pia alikanusha kauli inayosambazwa na baadhi ya wanachama na wabunge kuwa wanachama na wabunge wa mkoa wa Kigoma wote kwa pamoja wanaunga mkono hoja hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: