Baraza la Habari Tanzania (MCT), limekabidhi Tuzo kwa Mshindi wa Jumla wa Uandishi bora kwa mwaka 2009, aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro ikiwa ni baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili yeye na wenzake wawili.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Kajubi Mkajanga, alisema tuzo hiyo imeambatana na fedha taslimu shilingi milioni 6 na laki mbili na kuwa walishindwa kuitoa mwaka huo kutokana na Mshindi huyo kukabiliwa na kesi ya kuomba Rushwa ya shilingi milioni 10 kutoka kwa aliyekuwa mhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo Michael Wange.

Kwa upande wake Mshindi huyo Bwana Jerry Muro , ameishukuru MCT, na kuwataka waandishi wa habari kushirikiana na kutokata tamaa pindi wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali katika majukumu yao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: