Ndani ya uwanja wa Carnivo jijin Nairobi, ilikuwa ni shangwee tuu.
Mwanamuziki Cabo Snoop na densa wake wakilshambulia jukwaa vilivyo,huku shangwe na mikono kupunga kwa hewa kwa mashabiki kama kawa tu.
Utamu wa ngoma Live bwaana wee, palikuwa hapatoshi jukwaani, midomo ya bata kama kawa ilikuwepo kuongeza na kunogesha utamu wa live.
Mmoja wa madada wakali katika miondoko ya hipo hop nchini Marekani, Eve E akiwaachia mistari wakazi wa Nairobi, ambao wengi wao walikuwa wakivutiwa nae kwa namna ambavyo alikuwa akionesha kukomaa kwake kwenye anga ya muziki wa hip hop.
Shaggy ni mmoja wa wanamuziki ambao kiukweli awapo jukwaani hana masikhara kabisa na uwanja wake, kila wakati hupenda kuhakikisha watu wanashangweka tu, na ndivyo ilivyokuwa kwenye shoo yake usiku waleo, kila wakati alikuwa akiwaimbisha mashabiki nao bila hiyana walikwenda nae sambamba, hali iliyomfurahisha zaidi.
Hivi ndivyo Wakazi wa la Nairobi na kwingineko walivyotapika ndani ya uwanja wa carnivo, ambako ndiko tamasha la Tusker All Stars 2011 lilikofanyika, ama kwa hakika ni tamasha ambalo limefana sana ndani ya jiji hilo,pamoja na kuwepo na hali ya mvua mvua,lakini washabiki wa tamasha hilo ndio kwaanza walikuwa wakijiachia vilivyo uwanjani hapo huku wakipata vinywaji mbalimbali kutoka kampuni ya EABL-Kenya.Tamasha la Tusker All Stars 2011 limeratibiwa na kampuni ya Prime Time
Promotions kwa kushirikiana na wadau wengine, huku wadhamini wakuu wa tamasha hilo ni Kampuni ya East African Breweries Ltd-Kenya kupitia kinywaji chake cha Tusker.
Toa Maoni Yako:
0 comments: