Linda Kapinga mteuliwa mmojawapo.
Lucy akitoa ufafanuzi wakati wa mahojiano.
Lucy Minde Mteuliwa wa Pili.
Kushoto Lucy na Linda katika picha ya pamoja Ubalozini,
MH Naibu balozi kwenye picha ya Pamoja akiwa na baadhi ya maofisa wa ubalozi, TMK na mapromota wao waliokuja kuwaunga mkono Lin.
Urban Pulse Na Miss Jestina wakifanya mahojiano na Linda.
Kushoto Lucy na Linda katika picha ya pamoja Ubalozini.

Ubalozi wetu wa Tanzania Hapa Nchini Uingereza Kwa Kushirikiana na Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania wamewateua Linda Kapinga na Lucy Minde ili kwenda kutuwakilisha katika mkutano wa nne wa Commonwealth Youth Parliament ( Bunge la Vijana) ulioanza tarehe 6-10 Septemba 2011 jijini London. Mkutano huu Umeandaliwa na Commonwealth Parliamentary Association tawi la Uingereza ikishirikishwa na Sekretarieti ya CPA ambayo ni Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Katibu wake ni Mwafrika wa kwanza kuteuliwa na Pia ni  Mtanzania mwenzetu  Dr William Shija. 

Lengo kuu la mkutano huu ni kuwawezesha vijana kati ya miaka 19-29 kwa kuwapatia uzoefu wa shughuli za Bunge hasa katika kuimarisha demokrasia ya mabunge na Uchumi. Motto wa Mkutano wa mwaka huu "MABADILIKO YA HALI YA HEWA"

Ubalozi wa Tanzania hapa Uingereza unapenda kuwapongeza sana Linda Kapinga na Lucy Minde kwa kuchaguliwa kwao na pia kuwatakia kila la kheri katika kutuwakilisha kwenye mkutano huu.

Asanteni,
Urban Pulse ikishirikiana Miss Jestina Blog Na Ubalozi wa Tanzania
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: