Kufuatia janga liliotokea katika bahari ya hindi huko Zanzibar tarehe 10 Septemba, alfajiri ambapo hadi jana usiku watu mia mbili sabini wamethibitishwa kufariki katika janga hilo.. Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imetoa msaada wa chakula na maji wenye thamani ya shillingi milioni tano kwa walio nusurika katika ajali hiyo.
Tigo ni sehemu ya jamii na janga hili ni msiba kwa taifa zima na katika kuwajali sana wateja wake ambao ni sehemu ya jamii hiyo ikaona ni vyema kuwasaidia kwa vyakula na maji kwa wale walionusurika na ajali hii.
Mwakilishi wa Tigo bw. Alex Msigara alisema “Sisi kama Tigo tumeguswa sana na tukio hii na tunawapa pole wote ambao wamenusurika pamoja na wahanga wa ajali hii kwani watu wamepoteza ndugu, jamaa na marafiki ambao ni tegemeo kwa jamii husika”.
Mpaka sasa watu mia mbili na sabini wamekufa hapo hapo wakiwa hai katika meli iliyozama ya Mv Spice Islanders iliyokuwa ikitokea Bandari ya Malindi Unguja kuelekea Bandari ya Wete Kisiwani Pemba. Meli hii ilikuwa na zaidi ya watu mia sita wakisafiri kwenda bandari ya Wete Kisiwani Pemba.
Bw Alex Msigara wa Tigo ameendelea kusema kwamba “kampuni ya simu za mkononi ya Tigo bado wako katika mikakati mbalimbali yakusaidia wahanga wa tatizo hili ambapo chakula pamoja na maji ni moja kati ya jitihada mbalimbali zitakazotolewa na kampuni ya Tigo.

Toa Maoni Yako:
0 comments: