Gabriel Mollel. |
Wabunifu wa mavazi nchini Tanzania wametakiwa kuacha dharau, majungu na fitina badala yake wasaidiane ili kuiboresha na kuitangaza vyema tasnia hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa na mbunifu wa mavazi, Gabriel Mollel wakati akifanya mahojiano na blog hii jijini Dar es Salaam, ambapo mbunifu huyu alisema kuwa ni vyema wabunifu wakajitoa kuiendeleza tasnia hiyo na kuacha tabia ya majungu na fitina.
"Tatizo sio nani kuingia kwenye tasnia hii kwa mara ya kwanza, ni muhimu wewe mwenyewe kujiuliza umeifanyia nini tasnia hii tokea umeingia, tusiwabeze wabuni wachanga eti kwa sababu tu ya umaarufu ulionao, hatutaweza kufika mahali popote tusipokuwa waangalifu tutazidi kubezana kila siku bila sababu za msingi," alisema Gabriel.
Alisema kuwa wakati umefika sasa kwa wabunifu wote kuacha kushindana kwa midomo bali waonyeshe vitendo ili kuweza kuinusuru tasnia hiyo ya mitindo iweze kusonga mbele zaidi na zaidi.
Mwanadada akiwa katika moja ya vazi alilobuni Gabriell. |
Aliongeza kuwa wabunifu wote wanaweza kuijenga Tanzania yenye nguvu na umoja, "Mpaka sasa hivi hatuna vazi la Kitanzania kama nchi za mangharibi, badala ya kutafakari jinsi kupata mavazi kutambulisha Mtanzania tunaendelea kupeperusha majungu,"
Gabriell Mollel ni mmoja ya wabunifu wa mavazi hapa nchini Tanzania ambaye ananembo yake ya Sairiam na amekuwa akitengeneza mavazi ya asili pamoja na viatu.
Viatu ambavyo anavyotengeneza. |
Toa Maoni Yako:
0 comments: