Diwani wa Kigamboni, Halima Kisenga akishukuru kampuni ya Tigo kwa msaada wao wa kugawa vibao kwa kujifunzia wanafunzi wa shule ya msingi Mjimwema, jijini Dare s Salaam.
Afisa Viwango wa kampuni ya simu ya mkononi, Pamela Shellukindo akionyesha herufi na namba kwa wanafunzi na walimu wa Shule ya Msingi Mjimwema, na pia akiwaelekeza jinsi ya kutumia vibao hivyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mjimwema iliyopo Kigamboni wakiwa na vibao vya kuandika vya mapajani.
Afisa Viwango wa kampuni ya simu ya mkononi, Pamela Shellukindo akiongea na wanafunzi wa shule ya msingi Mji mwema.
---
Ikiendelea katika jitihada zake za kusaidia sekta ya elimu nchini Tanzania, kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imetoa msaada wa vibao 1000 kwa shule ya Msingi ya Mjimwema ya jijini Dar es Salaam.
Vibao hivyo ambavyo vimetengenezwa kwa kutumia plastik ili viweze kubebeka kwa urahisi. Juu ya kibao hicho kuna michoro na maandishi ya vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kumsaidia mwanafunzi kujifunza. Kuna michoro ya maumbo mbalimbali kama vile alfabeti, tebo ya kuzidisha na aina mbalimbali za rangi. Pia mwanafunzi anaweza kutumia kibao hiki kwa kusomea hata akiwa nyumbani.
Kampuni ya Tigo imefikia umamuzi wa kutoa msaada huo kwa kuthamini umuhimu wa elimu ya shule ya msingi. Halikadhalika kwa kuzingatia kuwa watoto wa leo ndiyo watakuwa viongozi wa kesho kwahiyo ni vyema kuwaboreshea mazingira ya elimu.
Mwakilishi wa Tigo Pamela Shellukindo alisema “Tunajisikia furaha sana kuwasaidia watoto hawa ambao ni viongozi wa kesho ili kuwarahishia njia ya kuzidi kujifunza hata kwa muda wao wa ziada. Tunafuraji kuona kwamba watoto hawa wataweza kuwa na hivi vibao na pia kuwaonyesha na wenzao na kujifunza pamoja.
Alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo hasa ni kusaidia badhi ya shule za msingi ambazo zimekuwa zikihitaji za nyezo za kujifunzia na kuongezea kuwa msaada huo utaendela kutolewa katika shule nyingine za msingi hapa nchini.
Mwalimu Nalu, ambaye ni mwalimu msaidizi wa shule ya msingi ya Mjimwema alisema “tuna furaha kubwa kwa Tigo kutufikiria kwa kutuletea vibao hivi. Kwakweli watoto wetu wanashukuru sana na najua kwamba watavitumia vibao hivi vizuri kwa kuangalia michoro hiyo pamoja na vitu vingine mbali mbali. Tunawapenda sana Tigo
Wakilishi wa Tigo Pamela aliendelea kusema ikiwa ni moja kati ya tamaduni tulizojiwekea Tigo kurudisha sehemu ya faida kwa Jamii tutaendelea kuisaidia jamii katika sekta mbali mbali ikiwemo elimu.

Toa Maoni Yako:
0 comments: