Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 22 Juni 2011 Serikali, kupitia kwa Waziri
wa Fedha na Uchumi wakati akihitimisha Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka
2011/12, ilitoa maagizo kwa EWURA kuchukua hatua mbalimbali zitakazochangia
kupunguza bei za mafuta kwa utaja maeneo mengi kama ifuatavyo (tunanukuu):
(a) Ukokotoaji wa thamani ya shilingi kwa kuioanisha na Dola ya Marekani (yaani Exchange rate);(b) Kuondoa au kupunguza wigo wa asilimia 7.5 ambayo makampuni yaliruhusiwa kuwekwa ili kufidia baadhi ya gharama;
(c) kupitia upya misingi ya ukokotoaji wa viwango vya tozo mbalimbali za taasisi za Umma kwa lengo la kubakia na tozo stahili na kwa viwango stahili bila kuathiri majukumu ya udhibiti ma usimamizi yanayofanywa na Taasisi hizo;
(d) kupunguza tozo za kampuni za mafuta ikiwa ni pamoja na gharama za kibenki (yaani Financing Charges); na
(e) Upotevu wa mafuta yanayosafirishwa kwenye meli na gharama ya ukaguzi (yaani inspection fee).
(a) Ukokotoaji wa thamani ya shilingi kwa kuioanisha na Dola ya Marekani (yaani Exchange rate);(b) Kuondoa au kupunguza wigo wa asilimia 7.5 ambayo makampuni yaliruhusiwa kuwekwa ili kufidia baadhi ya gharama;
(c) kupitia upya misingi ya ukokotoaji wa viwango vya tozo mbalimbali za taasisi za Umma kwa lengo la kubakia na tozo stahili na kwa viwango stahili bila kuathiri majukumu ya udhibiti ma usimamizi yanayofanywa na Taasisi hizo;
(d) kupunguza tozo za kampuni za mafuta ikiwa ni pamoja na gharama za kibenki (yaani Financing Charges); na
(e) Upotevu wa mafuta yanayosafirishwa kwenye meli na gharama ya ukaguzi (yaani inspection fee).
(mwisho wa kunukuu).
Aidha, mnamo tarehe 4 Julai 2011, EWURA ilianza mchakato kwa kutoa
matangazo kwenye vyombo vya habari kuhusu mchakato wa kupunguza bei za mafuta.
Pia EWURA iliandaa dokezo (discussuon paper) lililokuwa na vipengele mbalimbali
ambavyo vitapunguzwa na kusambazwa kwa wadau mbalimbali wakiwemo wauzaji wa
mafuta hapa nchini.
Wadau mbalimbali walichangia dokezo hilo na kuwasilisha EWURA kwa
maandishi na hatimaye mchakato wa utengenezaji wa Kanuni mpya ambayo imepunguza
bei za mafuta ulihitimishwa kwa kuitisha Mkutano wa TAFTISHI uliofanyika Julai
22, 2011 katika Ukumbi wa Karimjee
USHIRIKISHAJI
WADAU
Mchakato wa kupata maoni ya wadau (taftishi) ulianza tarehe 04 Julai 2011
na kukamilika tarehe 26 Julai 2011. Kwa kawaida, mchakato huu ungechukua siku
81 lakini kutokana na unyeti wa suala hili, Mamlaka ililazimika kuufupisha hadi siku 23. Wadau walioshirikishwa katika
taftishi hiyo ni pamoja na kampuni za mafuta, Baraza la Watumiaji wa Huduma
zinazodhibitiwa na EWURA (Consumer Consultative Council), Baraza la Ushauri la
Serikali, Taasisi za Umma kama vile TRA, TBS, WMA, TPDC, TPA, SUMATRA, na
TIPER.
MATOKEO BAADA Maoni mbalimbali
ya wadau yalipokelewa na kuchambuliwa na timu ya wataalam kutoka taasisi
mbalimbali zikiwemo Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha na Uchumi, Shirika la
Maendeleo ya Mfuta Tanzania (TPDC), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na
EWURA na katika mfumo mzima wa kufanikisha utayarishaji wa kanuni hii mpya,
wadau wote walifahamishwa katika mchakato huu kuwa bei mpya zitatolewa tarehe 1
Agosti 2011.
YA KUTANGAZ BEI MPYA
Baada
ya kutangaza bei mpya zilizoanza Agosti
3, 2011 kampuni zilianza mgomo baridi wa kutouza mafuta kutoka kwenye magahala
yake. Hata hivyo mgomo huo haukufahamika sana
kutokana na kutokea wakati kukiwa na siku za mapumziko ya muda mrefu yaani
taari 6 hadi tarehe 8 Agosti 2011.
Baada
ya kugundua hilo ,
Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA ilikaa Agosti 9, 2011 na kutoa AGIZO LA KISHERIA
(ORDER) kwa kampuni nne ambazo zilionekana ndizo kinara wa mgomo husika.
Kampuni hizo ni BP (T) Ltd, Oilcom (T)
Ltd, Camel Oit (T) Ltd na Engen Petroleum (T) ltd.
Agizo
hilo la
kisheria lilizitaka kampuni hizotajwa kutekeleza yafuatayo;
Baada
ya agizo kutolewa tarehe 9 Agosti 2011, kesho yake kampuni zote zilianza kuuza
mafuta kwenye maghala ambapo siku ya kwanza tarehe 10, Agosti 2011 ziliuzwa
lita 8,535,700 kutoka kwenye maghala .
Hata
hivyo, pamoja na kuuzwa kwa mafuta kwa wingi, bado BP (T) Ltd alionekana
kukahidi amri halali ya EWURA kwa kuzingatia Sheria ya Petroli ya mwaka 2008,
kifungu 24 (1) kwa kutouzaa mafuta kwenye vituo vyake vyote.
HATUA ZINAZOCHUKULIWA
Baada
ya kuchambua kwa undani kuhusu suala hili, Bodi ya Wakurugenzi imekutana leo na
kuamua yafuatayo:
USIMAMIZI WA MAFUTA
IMESAINIWA
Haruna Masebu
MKURUGENZI
MKUU
MAMLAKA YA UDHIBITI WA
HUDUMA ZA MAJI NA NISHATI (EWURA)
Toa Maoni Yako:
0 comments: