
Akikabidhi zawadi hizo Bungeni mjini Dodoma mara baada ya kipindi cha maswali na majibu, Waziri Mkuu mheshimiwa Mizengo Pinda alisema licha ya wanafunzi hao, wazazi na walimu waliowafundisha nao watazawadiwa ili kuongeza ari ya kujifunza na kufundisha mashuleni.
Mbali na hatua hiyo serikali pia itatoa meza ya maabara yenye thamani ya shilingi milioni tano na cheti kwa kila shule za kata walikosomea wanafunzi saba kati ya ishirini waliofanya vizuri kwenye mtihani wa kidato cha sita.

Toa Maoni Yako:
0 comments: