Anatambulika kwa jina la Samir Khasim almaarufu kama Samir, msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya kutoka mjini Morogoro aliyeanza muziki mwaka 2004 akiimba katika talent shows na mashindano mbalimbali ya muziki katika ‘club’ za muziki.
Mnamo mwaka 2004 alianza muziki na kutoka na single yake iliyokwenda kwa jina la 'Nyamaza' aliyorekodia ndani ya Mamasa Recodr iliyopo mjini Morogoro japo wimbo huo haukuweza kufanya vizuri.
Kijana huyu hakusita kuendelea kusonga mbele mpaka ilipofikia mwaka 2010 ndipo alipoibuka na nyimbo yake iliyokwenda kwa jina la 'Ukipenda' aliyorekodia ndani ya studio za Roca Tz, wimbo ambao kiukweli umemtambulisha na kumfanya jamii imtambue.
Mpaka sasa Samir ameshakamilisha kurekodi albamu yake ambayo imekusanya nyimbo zipatazo 10 ikiwemo 'Ukinipenda' ambayo imebeba jina la albamu 'Mnyonge', 'Maumivu', 'Sema', 'Sikuhitaji', 'Bado ni Fumbo', 'Vumilia', na nyingine nyingi.
Anaongeza kuwa nyimbo zilizomo katika albamu hiyo amerekodia katika studio ya Sarobaro, AM Record, Manake pia ameanza kurekodi albamu yake ya pili itakayokwenda kwa jina la 'Maumivu ya Mapenzi'
Akizungumzia kwa nini anaimba nyimbo za mapenzi tu, Samir amasema kuwa kwa sasa jamii inapenda sana nyimbo za mapenzi unapoimba nyimbo nyingine ni vigumu sana kupokelewa na ndiyo maana wasanii wengi wanaishia njiani kwa vile hawajaweza kuisoma jamii inataka nini, anasema kijana huyu huku akicheka.
Kijana huyu ambaye kwa sasa ameamua kufanyia shughuli zake za muziki jijini Dar es Salaam kutokea mjini Morogoro anasema kuwa ni vyema wasamii wakasoma alama za nyakati kwa kusoma mazingira ya kufanyia kazi zao na pia kusoma jamii inahitaji nyimbo gani ili uweze kukubalika.
Samir Khasim ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika familia ya mzee Khasim, alizaliwa mkoani Morogoro miaka 20 iliyopita.
Alipata elimu yake msingi katika shule ya Chamwino mjini humo na baadae kujiunga na shule ya sekondari Jabar Ila ilipo huko Morogoro.
"Samir anashukuru kuwa na uwezo wa kuimba sehemu yoyote ile na bila ya uoga na watu wakamuelewa vyema kabisa, anasema na kuongeza kuwa anategemea kuwa mwanamuziki mkubwa Tanzania ambaye atakuwa na mafanikio makubwa katika anga za muziki wa kizazi kipya,".

Toa Maoni Yako:
0 comments: