***WANAUME HALISI NA WANAUME TMK SASA KUPIGA MASAFA YA MBALI

Dar es Salaam 3 April 2008

Kampuni ya Simu ya mkononi ya Tigo imeweka wazi kukabidhi Magari kwa makundi mawili ya wasanii wa kizazi kipya ya wanaume halisi na wanaume Tmk ikiwa ni kutimiza dhamira ya Tigo katika kuchangamana na vijana na shughuli zao.
Meneja masoko wa kampuni ya simu za mikononi ya tiGO Kelvin Twissa, akiongea na waandishi wa Habari.
Kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi Inspekta Haroun akiwa na baadhi ya wasanii wenzake, akiishukuru kampuni ya tiGO kwa kazi kubwa walioifanya kwa wasanii wa makundi hayo yote mawili
Akiongea na waandishi wa habari Meneja Masoko wa Tigo Bw Kelvin Twissa alisema ¨Tigo tunatambua juhudi za wasanii wetu vizuri sana katika kuburudisha na kuelimisha jamii yote, hivyo kwa kuonyesha ukaribu wetu na muziki na vijana wa kitanzania ndani ya zoezi la mkali nani leo tunawakabidhi Wanaume TMK na Wanaume halisi. Magari haya kwamba ni ya kwao ¨Lakini tukiwa kama wadhamini wakuu kwa kushirikiana na TBL tumetoa nafasi ya kuwasikiliza wakali hawa na kutoa uhuru kwao kuwa wanaweza kuchagua kupewa gari ili waendelee kupiga masafa ya mbali au pesa taslimu zenye thamani ya gari hili wafanyie shughuli zao kutokana na maamuzi ya kundi.
Meneja masoko wa TIGO, Kelvin Twisa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za kampuni hiyo leo asubuhiSisi tunawapatia magari tukiwa na imani kuwa gari hizi watazitumia katika shughuli mbalimbali za kuendeleza makundi haya ili kuifikishia jamii burudani kali kulingana na uhitaji wa kila mahali.Sasa tunachongoja ni burudani kutoka kwao kwenda kila kona ya Tanzania na nje ya nchi hii.
Meneja masoko wa kampuni ya simu za mikononi ya TIGO Kelvin Twissa, akimkabidhi ufunguo wa gari kiongozi wa kundi la Wanaume Halisi Inspekta Haroun leo asubuhi nje ya ofisi ya kampuni hiyo.
Kila kundi litakamua liwezavyo katika mikoa nane kwenye tofauti maonesho tofauti ya MKALI NANI? hivyo kwa wale wapenda burudani wakae mkao wa kujiachia non-stop kila muda utakapowahitaji wakali hawa utawapata kwa kuwa wanausafiri wa haraka kutoka Tigo Wananchi na washabiki wa makundi ya muziki wa kizazi kipya wajitokeze kwa wingi katika maeneo ya maonesho yatakapofanyika kulingana na ratiba ilivyopangwa ili waweze kupata burudani kabambe kutoka kwao na kuamua MKALI NANI?
Meneja masoko wa kampuni ya simu za mikononi ya TIGO Kelvin Twissa akimkabidhi ufunguo wa gari Meneja wa kundi la Wanaume TMK Original Mkubwa Said Fella leo asubuhi nje ya ofisi ya kampuni hiyo.

Pia unaweza kuamua kumchagua mkali nani kwa kupiga namba maalumu ya Tigo 15007 ambapo utaweza kujihamishia wimbo wa wanaume halisi wa tatu bila au ule wa wanaume TMK Original wa Dar Mpaka Moro kama muito wa simu yako ili kuwaongezea nafasi ya UKALI kambi ya wanaume unayoipenda. Pia unaweza kuchagua LOGO, ya kundi, picha ya au picha ya msanii kiongozi wa kundi (Temba au Nature) kwa kupitia huduma yetu ya WAP na kwakufanya hivyo utakuwa umeunga mkono kundi unalolipenda kuibuka MKALI.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: