MHE. PINDA ATOA SALAMU ZA POLE

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ametoa salamu za pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu waliopoteza maisha katika ajali ya mabasi iliyotokea karibu na Gairo mkoani Morogoro mapema leo (Jumanne Aprili 1, 2008).
Kwa mujibu wa habari kutoka Morogoro, ajali hiyo ya kugongana kwa basi la Champion na la Happy Nation, imesababisha vifo vya watu wanane ambao kati yao watano papo hapo na wengine watatu walipofikishwa hospitalini.
Majeruhi 17 walipelekwa hospitali ya mkoa wa Dodoma kwa matibabu zaidi.
Katika salamu zake hizo, Waziri Mkuu Pinda alisema alipokea kwa masikitiko habari za vifo hivyo vilivyotokana, kwa mara nyingine tena, na ajali ya barabarani na kusema lazima ipatikane dawa ya kupunguza ajali hizo.
"Natoa pole kwa ndugu na jamaa wa marehemu na inasikitisha kuwa taifa limepoteza tena maisha ya watu kutokana na ajali za barabarani. Naomba majeruhi wapone haraka," Waziri Mkuu alisema.
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021,
DAR ES SALAAM
Jumanne Aprili 1, 2008

Toa Maoni Yako:
0 comments: