Wakati Tanzania waimbaji wa muziki wa bongoflava wakiukimbia muziki huo, hata huko kwa mzee Mandela, Afrika Kusini Mwanamama Yvonne Chakachaka ameamua kusalimisha maisha yake kwa Yesu na kubadilika kuanza kuimba gospel.

Yvonne Chakachaka ambaye alitangaza uamuzi wake hivi karibuni na anatarajia kuzikonga nyonyo za wapenzi wa muziki huo, mwishoni mwa mwezi huu yaani tarehe March 30 pale atakaposhuka Dar kwa ajili ya kusindikiza uzinduzi wa Kwaya ya New Kitimutimu ya Dodoma.
Uzinduzi huo wa albamu yao ya kwanza ijulikano kwa jina la 'Mapigano ya nini' unarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee na utamkutanisha mkongwe huyo wa muziki wa
culture (asili) aliyetamba kwa muda mrefu lakini ameamua kubadirika.
Habari na matukio ilipoongea na mmoja wa viongozi wa maandalizi hayo alitutell kuwa sasa wakati umefika wa kuleta mageuzi katika muziki wa gospel kwa kuwaleta waimbaji wa kimataifa ili walete changamoto.
New Kitimu timu iliundwa upya baada ya kujitenga na aliyekuwa kiongozi wa kikundi hicho malkia wa muziki huu wa injili Rose Muhando. Mwanamama huyo kwa sasa ameokoka na anaimba nyimbo za injili na ameshaandaa albamu yake ya kwanza itakayotoka hivi karibuni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. Ni baraka na inapendeza hasa waimbaji wa nyimbo zisizomtukuza Mungu wakiamua kumpa Yesu maisha yao na kuamua kumuimbia Yeye! Reene Lamira, pia K-Basil na wengi nao wanaona kumtumikia Mungu ni bora kuliko kutumikia mambo mengine ndo maana wakaamua kumpa Yesu maisha yao. Bado tunaamini na wengine pia watakuja. Mungu amewapa vipaji ili wamuimbie YEYE! Amen

    ReplyDelete