“Jina langu limevuma, Kwenye mitaa. Jina langu lina hadhi ya ki-superstar.Jina langu…..” Hayo ni maneno kutoka kwenye wimbo Jina Langu wa msanii mahiri wa Bongo Flava, PROFESSOR JAY au Prof Jiizeh. Hakuna ubishi, jina lake limevuma na ni kweli ana hadhi ya ki-superstar.Alizaliwa jijini Dar-es-salaam tarehe 29 December 1975. Ni mtoto wa sita kati ya watoto tisa wa Mzee Leonard Steven Haule na Mama Rose Majanjara. Baadaye akasoma Ukonga Primary School kabla hajaelekea mji kasoro bahari(Morogoro) kusoma Kigurunyembe Secondary na baadaye Mbeya Lutengano High School.
Sasa anatarajia kuzindua albamu yake ijulikanayo kwa jina la 'Aluta continua' itakayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambapo atasindikizwa na wasanii akiwemo Juma Nature, A-Sele, Jose Kamilioni, Blue III na wengine wengi.
Professar Jay ana tuzo za muziki zisizopungua 25 ambazo amezikusanya ndani ya miaka 15 ambayo amekuwa kwenye game.
Professar Jay ana tuzo za muziki zisizopungua 25 ambazo amezikusanya ndani ya miaka 15 ambayo amekuwa kwenye game.


Toa Maoni Yako:
0 comments: