Pages

Thursday, 12 February 2026

CCM na SWAPO Zaendelea Kuimarisha Uhusiano wa Kihistoria

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, leo Alhamis, Februari 12, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini, Mheshimiwa Gabriel Pandureni Sinimbo.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, yakilenga kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya vyama hivyo viwili pamoja na mataifa yao.

Katika kikao hicho, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kisiasa na kidiplomasia, wakisisitiza umuhimu wa kudumisha urafiki wa kidugu uliodumu kwa miaka mingi kati ya CCM na Chama cha SWAPO cha Namibia.


Aidha, walieleza dhamira ya kuendeleza ushirikiano katika kubadilishana uzoefu, mafunzo na mikakati ya kuimarisha vyama vyao pamoja na kuchochea maendeleo ya wananchi wa Tanzania na Namibia.

Uhusiano kati ya Tanzania na Namibia umejengwa katika misingi ya mshikamano wa kihistoria tangu enzi za harakati za ukombozi wa Afrika, ambapo Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kuunga mkono mapambano ya uhuru wa Namibia.

No comments:

Post a Comment