Pages

Thursday, 18 October 2018

DC MURO AVIONYA VYAMA VYA SIASA KUTODUMAZA MAENDELEO

Baadhii ya Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe.Jerry Muro alipokuwa akizungumza nao.

Na Imma Msumba, Arumeru.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe.Jerry Muro amevitaka vyama vya siasa kuacha  malumbano na mvutano isiyokuwa na tija kwa wananchi wa Arumeru na badala yake amewataka kuungana na serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Arumeru.

Mh. Muro ameyasema hayo baada ya kuingilia kati  mgogoro wa umiliki wa jengo ambalo awali lilikuwa likitumiwa na chama  cha ushirika kata ya Ilikiurei hatua iliyosababisha kufungwa kwa ofisi  ya serikali ambayo ilikuwa ikihudumia wananchi wa vitongoji viwili.

Kwa upande wao wananchi wanaoishi katika vitongoji hivyo mbali na  kumpongeza Dc Muro kwa kuchukua hatua kwa haraka kuwa ofisi hizo  zifunguliwe wamesema uamuzi huo utawasaidia kupata huduma ambazo  wamekuwa wakizikosa kwa muda mrefu kutokana na mvutano wa umiliki wa  jengo hilo kutoka kwenye vyama viwili vya siasa.

No comments:

Post a Comment