Pages

Friday, 21 September 2018

IDADI YA MIILI ILIYOOPOLEWA YAONGEZEKA KUFIKIA 86, WATU WALIO HAI 40 KATIKA AJALI YA KUZAMA KWA KIVUKO CHA MV. NYERERE ZIWA VICTORIA

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe John Mongella hadi leo saa 4 asubuhi Septemba 21, 2018 jumla ya maiti 86 zimeopolewa.

Akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Mongella amesema Miili ambayo imeshaopolewa leo asubuhi pekee ni 42 wakati mingine 44 ilipatikana jana,kwa hiyo Jumla ni 86 na Watu 40 waliokolewa wakiwa hai .

Amesema kuwa pamoja na kupatikana idadi hiyo ya watu bado wanaendelea na shughuli ya uokoaji

MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

No comments:

Post a Comment