

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dkt. John Pombe Magufuli, baada ya kutangazwa kuwa Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, katika uchaguzi uliofanyika Jana Julai 11, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM (Dodoma Convition Centre), uliopo Mjini Dodoma. Dkt. Magufuli ameibuka mshindi kwa jumla ya kura 2104, wakati wapinzani wake, Balozi Amina Salun Ali akipata kura 253 na Dkt. Asha-Rose Migiro akipata kura 59

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana wakipitia moja
ya magazeti ya kila siku wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM, Mjini Dodoma.

Wanachama waliohudhuria katika uchaguzi uliofanyika Jana Julai 11, 2015 kwenye Ukumbi wa
Mikutano wa CCM (Dodoma Convition Centre), uliopo Mjini Dodoma.
WAZIRI wa Ujenzi na Mbunge wa Chato, Mh.Dkt. John Pombe Magufuli, ameteuliwa na Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, kuwa Mgombea wake wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Habari za mkutano huo uliofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Dodoma, kinachomilikiwa na CCM, zimeeleza kuwa, Mh. Dkt. Magufuli amepata jumla ya kura 2, 104, na kuwashinda wapinzani wake, Dkt. Asha-Rose Migiro, aliyepata kura 59, na Mh. Amina Salum Ali, amenyakua kura 253.
Awali kabla ya kufikia kilele cha mchakato huo wa kumpata mgombea wa CCM palizuka mvutano mkali kwenye vikao vya mchujo, ambapo manung’uniko na mifarakano ilianza pale Kamati Kuu ya chama hicho, kutojadili majina yote ya wagombea na badala yake kujadili majina machache huku yale yua makada waliopuwa wakipigiwa upatu, kuachwa.
Hata baada ya kikao nhicho cha kamati kuu, hali ilikuwa mbaya zaidi wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC), ambapo baadhi ya wajumbe walionyesha wazi wazi upinzani wao dhidi ya maamuzi ya kamati kuu, hali iliyopelekea jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama kuongeza nguvu ya ulinzi ikiwa ni tahadhari endapo patatokea jambo baya.
Majina yaliyofikishwa ili kujadiliwa na Halmashauri kuu ni pamoja na lile la Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe, Waziri wa Sheria na Katiba, Mh. Dkt. Asha Rose Migiro, Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, Mh. January Makamba, na Waziri wa Ujenzi, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, na Mh. Balozi Amina Salum Ali.
Halmashauri Kuu ikapitisha majina matatu ya watakaoingia kwenye uamuzi wa msiho wa Mkutano Mkuu wa CCM ambapo hatimaye umemchagua Mh. Dkt. John Magufuli kuwa ndiye atakayepeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu.




No comments:
Post a Comment