Pages

Monday, 6 July 2015

MEYA JERRY SILAA WA ILALA ATANGAZA RASMI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA UKONGA


Diwani wa kata ya Gongo la Mboto na Meya wa Manispaa ya Ilala,Jerry Slaa akihutubia wananchi katika uwanja wa shule ya msingi kitunda mwishoni mwa wiki ambapo alieleza mafanikio yaliyopatikana wakati wa kipindi chake cha uongozi na kukamilisha ahadi mbalimbali alizokuwa amezitoa.
Mmoja wa wawakilishi wa kikundi cha akina mama akipokea fedha kwa niaba ya wenzake kutoka kwa Meya wa Manispaa ya ilala ambazo alikuwa amewaahidi wakati wa mkutano wa Meya huyo kuelezea mafanikio yake.
Baadhi ya madiwani na wazee wa Ukonga wakimpongeza Meya Jerry Slaa kwa kutimiza ahadi alizotoa muda mfupi baada ya kueleza mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wake ambapo vilevile alitangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Ukonga.
Baadhi ya madiwani na viongozi wa CCM kata ya Ukonga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano huo.

No comments:

Post a Comment