Mwenyekiti kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Ayubu Njenza (kushoto) akimkabidhi vifaa vya michezo katibu wa
chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Kinondoni,Isaac Mazwile kwaajili ya
mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars,
inayoanza tarehe 24 Julai mkoani Mbeya. katikati ni Afisa Uhusiano
Airtel,Jane Matinde. Makabidhiano hayo yalifanyika leo jijini
Dar-es-Salaam.
Mwenyekiti kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Ayubu (katikati kushoto), Afisa Uhusiano Airtel, Jane
Matinde, katibu wa chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Kinondoni,Isaac
Mazwile kulia na Afisa Maendeleo wa TFF bwana Jemadari kwa pamoja
wakionyesha vifaa vya michezo vitakavyotumika wakati wa michuano ya
Airtel Rising Stars. Airtel jana ilikabithi vifaa kwa timu zote
zitakazoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu.
Mwenyekiti kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Ayubu Njenza (kushoto) akimkabidhi vifaa vya michezo katibu wa
chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Ilala Kanuti Daudi kwaajili ya
mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars
katikati ni Afisa Uhusiano Airtel Jane Matinde. Makabidhiano hayo
yalifanyika leo jijini Dar-es-Salaam.
No comments:
Post a Comment