Pages

Tuesday, 27 May 2014

VODACOM YAANZISHA "ZOGO" KWA WATEJA WAKE

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, akifafanua jambo wakati akitangaza huduma mpya ya 'Zogo' inayoyawezesha wateja wa mtandao wa Vodacom  kupiga simu ndani na nje ya mtandao na kujipatia vifurushi kwa gharama nafuu. Ili kujiunga mteja anatakiwa kupiga *149*01#.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Mawasilino ya Vodacom Tanzania, imezindua huduma mpya ijulikanayo kama 'Zogo' ambayo itawawezesha wateja wa mtandao huo kupiga simu ndani na nje ya mtandao kwa gharama nafuu.

Akizungumza juu ya uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amebainisha kuwa ofa ya Zogo ni maalum kwa wateja wa Vodacom ambapo sasa tutawawezesha kujipatia muda mwingi wa maongezi kupitia mtandao wetu na kwa gharama nafuu zaidi.

 "Vodacom ni kampuni inayoendeshwa kutokana na mahitaji ya wateja wake na Zogo imekuja muda muafaka ambapo wateja wetu wameomba muda zaidi  wa maongezi kupitia vifurushi vyetu vya ChekaBombastiki ambavyo vinajumuisha muda wa maongezi, ujumbe mfupi na intaneti viongezwe zaidi."

Twissa aliendelea na kuwatoa hofu wateja wake kuwa, vifurushi vya ChekaBombastiki vitaendelea kuwepo kama vilivyo kwa wateja wote wanaopendelea kufuruhia huduma mchanganyiko za dakika za muda wa maongezi, kutuma ujumbe mfupi, huduma za intaneti pamoja na kupiga simu kwenda mitandao yote nchini.

"Ofa ya huduma ya Zogo inapatikana kwa wateja wa ndani ya mtandao wa Vodacom na inaunafuu  mkubwa zaidi ukilinganisha na vifurushi vya ChekaBombastiki. Ofa hii inampatia mteja dakika 30 za muda wa maongezi kwa Sh. 495 tu ndani ya masaa 24, wakati Sh. 645 na 995 zinawapatia wateja dakika 45 na 90 za muda wa maongezi kila moja." Alisema Twissa.

No comments:

Post a Comment