Mratibu mwandamizi wa polisi mkoa wa Mwanza SSP Christopher Cyprian Fuime, akikata utepe kuzindua duka la Airtel Mwanza mara baada ya matengenezo na kulifanya duka hilo kuwa la kisasa, pembeni yake ni Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba akiwa pamoja na wafanyakazi wa Airtel Mwanza. Uzinduzi huu umefanyika mwisho mwa wiki hii
Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba (kulia) akimwonyesha mgeni rasmi Mratibu mwandamizi wa polisi mkoa wa Mwanza SSP Christopher Cyprian Fuime kaunta maalumu zilizotengenezwa kwenye duka jipya kuhakikisha usalama katika huduma ya Airtel money wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel lililopo Mwanza, akishuhudia ni Violet Gyumi Afisa mauzowa Airtel kanda ya ziwa
Mratibu mwandamizi wa polisi mkoa wa Mwanza SSP Christopher Cyprian Fuime akipewa maelezo na mfanyakazi wa kitengo cha wateja wakati wa uzinduzi wa dula la Airtel Mwanza, pichani ni Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba pamoja na wafanyakazi wa Airtel
Mkuu wa kitengo cha huduma za wateja wa Airtel Bi Adriana Lyamba (kushoto) akitoa maelezo kwa Mratibu mwandamizi wa polisi mkoa wa Mwanza SSP Christopher Cyprian Fuime kuhusu sehemu mbalimbali za duka jipya la mwanza wakati wa uzinduzi wa duka hilo ulifanyika mwishoni mwa wiki , pichani kulia ni Afisa mauzo wa Airtel kanda ya ziwa Violet Gyumi
Wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa duka la kisasa lililopo mwanza.
Afisa mauzo wa Airtel kanda ya ziwa Violet Gyumi akitoa zawadi kwa wateja waliohudhuria halfa ya ufunguzi wa duka la Airtel Mwanza uliofanyika mwishoni mwa wiki
---
Na Mwandishi Wetu, Mwanza.
Mrakibu mwandamizi wa polisi mkoa wa Mwanza SSP Christopher Cyprian Fuime, ameipongeza Airtel kwa kuboresha mazingira ya maduka yao kuwa ya kisalama zaidi kwa watumiaji wa huduma zao mbalimbali husasani ya Airtel Money.
SSP Christopher Cyprian Fuime, aliyasema hayo kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola wakati wa uzinduzi wa duka la kisasa la Airtel lilipo Mwanza uliofanyika mwishoni mwa wiki hii.
SSP Fuime alisema” nimefurahishwa sana na maboresho makubwa katika duka hili ambayo yatawawezesha wakazi wa Mwanza na wateja wa Airtel kupata huduma bora kwa haraka zaidi katika mazingira mazuri.
“Tunawashauri wateja na wakazi wa Mwanza kupata muda na kutembelea duka hili na kufurahia huduma zinazotelewa hapa”. Aliongeza SSP Fuima.






No comments:
Post a Comment