Pages

Saturday, 1 February 2014

WAZIRI WA HABARI,VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA SHULE ZA SEKONDARI JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara (wa pili kushoto)akikabidhi moja ya vifaa vya michezo kwa mwanafunzi wa shule ya sekondari Kibasila, Simon Nungu (kulia)Vifaa hivyo vya michezo vilivyotolewa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya mashindano ya michezo mbalimbali itakayoanza hivi karibuni na kuzihusisha shule za sekondari kumi na mbili(12)za jijini Dar es Salaam.Wanaoshuhudia makabidhiano hayo kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Elisante Ole Gabriel, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania(wa tatu kushoto),Salum Mwalim.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mh. Dk. Fenella Mukangara(wapili toka kushoto)akishuhudia Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania(kulia) Salum Mwalim akikabidhi mfano wa hundi ya Milioni moja(1,000,000) kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Henry Lihaya (wa pili kushoto) fedha hizo zitatumika katika maandalizi wakati wa mashindano ya michezo shule za sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Prof. Elisante Ole Gabriel.

No comments:

Post a Comment