• Hili swali pengine hata wewe unaweza kujiuliza wengi wetu tumekuwa tunashindwa kwenye usaili na kutka na visingizio vingi kama kubebana,au kazi zinawenyewe sisi wengine ni wasindikizaji baadala ya kutafuta makosa yako na kuweza kuyarekebisha ili yasijirudie tena hapa nitaeleza baadhi ya sababu zinazo fanya watu washindwe kwenye usaili nazo ni kama ifuatazo:
1.KUKOSA UMAKINI JUU YA KAMPUNI HUSIKA AU TAASISI HUSIKA
Watu wanaingia kwenye usaili hata bila kuja japo kwa kifupi kampuni husika inajishughulisha na nini, nini malengo na shabaha ya kampuni husika au taasisi,watu hufikiri wataulizwa kuhusiana na mambo aliyosomea kumbe unatakiiwa kujua hata historia kwa ufupi juu ya taasisi au kampuni husika
2.MUONEKANO
Hili ni jambo la msingi sana unapoitwa kwenye usaili jitahidi kuwa nadhifu toka chini mpaka juu na hili wengi wameshindwa labda kwa kuwaona baadhi ya wafanyakazi wa sehemu husika wakiwa wamevaa vibaya hiyo inapelekea hata wao kuchukulia rahisi tu hatimaye kukosa marks,kumbuka pale uko kwenye ushindani hivyo inatakiwa uonyeshe kila aina ya ushawishi.
3.MAANDALIZI MABAYA
Wengi wamekuwa hawajiandai vizuri linapokuja suala la usaili,jitahidi kutafuta maswali ambayo yanaweza yakaulizw na uwe na majibu yake,pia kujiandaa kisaikolojia maana utakutana na watu wakikusiliza wewe na kukuhoji maswli hivyo kisaikolojia inatakiwa ujiandae pia
4.USIKIVU
Usikivu siku zote hufanya mtu akaelewa jambo lolote hapa wengi huwa si wasikivu labda kwa sababu ya hofu hivyo kujikuta akitoka nje ya swali ni vema ukawa mtulivu kusikiliza vizuri swali na kulielewa
5.KUEGEMEA UPANDE WA MSHAHARA
Wengi wamekuwa wakifiria sana mshahara kuliko kazi yenyewe yaani wanataka mshahara mkubwa hata bila kujua ukubwa wa kazi yenyewe labda kwakuwa alisikia toka kwa mfanya kazi wa sehemu hiyo waajiri huwa wanakuwa na wasi wasi juu ya utendaj wako wa kazi.
Ni hayo tu nilitaka tukumbushane unaweza ukaongezea na wewe kama unayo

No comments:
Post a Comment