Gari la Matangazo la nje (Ob Van) la Azam Media ambalo hutumika kurushia matangazo ya moja kwa moja (live) toka uwanjani. Ob van hilo nila kwanza kwa Tanzania hakuna chombo cha habari ambacho kimewahi kumiliki.
King'amuzi cha Azam Tv ambapo ili kuweza kutumia huduma hiyo unatakiwa kulipia shilingi elfu tisini na tano (95,000/-) utafungiwa na utakuwa unafanya malipo ya mwezi kwa shilingi elfu kumi na mbili (12,500/-) kwa mwezi na utakuwa unapata channel nyingi zaidi za ndani na nje zikiwemo za burudani, michezo na habari.
Wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja kwa wale wanaohitaji kufungiwa ving'amuzi na matatizo ya kiufundi.
Wafanyakazi wa kitengo cha call center
Wafanyakazi wa kitengo cha Malipo kwa mwezi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Azam Media, Rhys Torrington akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari waliopata fursa ya kufanya ziara ya kutembelea Ofisi za Kampuni hiyo juu ya uanzishwaji wa Televisheni yao ya Azam TV yenye muonekano wa kisasa zaidi na yenye lengo la kukuza michezo mbali mbali hapa nchini, zilizopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam leo.
Huduma kamili za Azam TV zinatarajiwa kuanza rasmi mwezi ujao na kwa mujibu wa Rhys Torrington kila kitu knaendelea vizuri. “Tutafungua milango ya Azam TV rasmi katikati ya Novemba kwa huduma ya chaneli 35 ambazo watu wajionea bure na uzinduzi utafanyika Novemba hiyo hiyo,”alisema.
Torrington alisema kwamba king’amuzi cha Azam TV kitauzwa kwa Sh. 95,000 pamoja na dishi lake na pia mteja kupatiwa huduma za kufungiwa na kuunganishiwa bure nyumbani kwake.
Alisema malipo ya mwezi yatakuwa ni Sh. 12,500 tu na mteja atapata chaneli zaidi ya 50 katika king’amuzi cha Azam TV.
Alisema Azam TV pekee kwa kuanzia itakuwa na chaneli tatu ambazo ni Azam One itakayohusu habari za Afrika na zaidi za Kiswahili, Azam Two ambayo itakuwa ya kimataifa yenye vipindi mbalimbali duniani, na baadhi vya Kiswahili na Sinema Zetu itakayokuwa ikionyesha sinema za Kitanzania kwa saa 24 kila siku.
Mashine ya kucahanga picha zinazotoka uwanjani wakati wa matangazo ya moja kwa moja (live).
Mixer ya sauti.
Msimamizi wa matangazo ya moja kwa Moja (live), Yahaya akitoa maelezo kwa wanahabari juu ya mashine ya kuchanganya picha na maelezo (graphics).
Hapa ni sehemu ya kutoa picha za mgando (slow motion).
Jenereta la kuendesha mitambo, hakuna kutegemea umeme wa tanesco.
Blogger Dj Choka akiwa pamoja na wafanyakazi wa Azam TV.
No comments:
Post a Comment