Pages

Monday, 5 March 2012

SIMBA ILIVYOWAGALAGAZA KIYOVU, RWANDA 2-1


Wachezaji wa timu ya Kiyovu wakijaribu kumdhibiti
...Kiyovu wakiwa na mpira
...Ilikuwa raha tupu

...kaba nikukabe

Goooooooooooooooooooooooooooo!~Dakika ya 19 na 32 za mchezo,Mshambuliaji wa timu ya Simba,Felix Sunzu anaipachikia mabao 2 ya kuongoza timu yake baada ya kumalizia pasi nzuri za Mchezaji Emmanuel Okwi (Balloteli). Ambapo timu ya Kiyovu iliandika  bao 1 katika  dk ya 76 kipindi cha pili. 
Mshambuliaji wa Timu ya Simba, Emmanuel Okwi na Felix Sunzu wakishangilia bao la pili lililofungwa na Felix Sunzu.
Hapa ilikuwa ni vita kati ya mashabiki wa timu ya Yanga na Simba ambao walianza kurushiana viti hali hiyo ilifanya kupotea kwa amani kwa muda eneo hilo mpaka polisi waliingilia kati.
Mashabiki wa Yanga wakimwadabisha shabiki wa Simba ambaye alienda eneo lao huku akiwa amevaa jezi ya Simba jambo ambalo liliwakera mpaka wakamvua na kuichana chana.
...Askari akijaribu kuondoa viti walivyokuwa wakirushiana
Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage (mwenye kofia) akiwasalimia mashabiki wa Simba waliojitokeza uwanjani hapo.

...Siyo mimi niliyemwangusha
...Baki mpira uende
...Ukicheza mpira lazima uwe na msuli na stamina
Kiyovu wakishangilia goli lao la kwanza walilolipata
...ahaaaaaaaaa

Kocha wa Simba akiwaangalia wachezaji wake mara baada ya mpira kumalizika
Mchezaji wa Simba Emamuel Okwi akijaribu kubadirishana mawazo na wachezaji wa Kiyovu mara baada ya kumalizika kwa mechi.
Wachezaji wa timu ya Simba wakiondoka uwanjani kwa furaha. Timu imetinga hatua ya pili ya michuano ya kombe la shirikisho baada ya kuifunga timu ya Kiyovu magoli mawili kwa moja. Mabao ya Simba yamepatikana kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji Felix Sunzu, wakati bao la Kiyovu likifungwa na mchezaji Nelly Mayanja.
Furaha baada ya Kazi kuisha
Wachezaji wa timu ya Kiyovu wakitoka uwanjani baada ya kufungwa na Simba.

No comments:

Post a Comment