Pages

Monday, 11 July 2011

JUKUMU LA KUTUNZA FAMILIA NI JUKUMU WA WAZAZI WENYEWE: MHE: UMI ALI MWALIMU.

Serikali imesisitiza kwamba jukumu la kutunza familia ni la wazazi wenyewe na kwamba itaendelea kuweka mazingira mazuri yatakayowezesha familia kupata fursa za kimaendeleo na huduma za Jamii ikiwemo chakula, huduma za Afya, Elimu na pembejeo za kilimo.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Umi Ali Mwalimu aliliambia Bunge mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Naomi Kaihula aliyetaka kujua Serikali itazisaidiaje familia zinazotunzwa na mzazi mmoja ili kuondokana na tatizo la watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

No comments:

Post a Comment