Pages

Wednesday, 27 April 2011

CHOO CHA STENDI YA BASI LA SHABIB, GAIRO MOROGORO KINAHATARISHA AFYA ZA ABIRIA.

Muonekano wa Choo kwa nje ambapo kinaonekana kinapendeza ila kwa ndani ni balaa.
Muonekano wa choo kilivyo kwa ndani.
Wafanyabiashara wakifanya biashara nje ya choo hali ambayo ni hatari kwa afya zao na kwa wateja wao.

Huo ni muonekano wa Choo cha stendi ya basi la Shabib, Gairo- Morogoro ambacho kinahatarisha afya za abiria licha ya abiria hao kuwa wanalalamika mara kwa mara kwa uongozi na haufanyii kazi malalamiko yao. Blog yako ya Habari na Matukio ilitembelea choo hicho na kukuta hali ya kusikitisha sana, licha ya wahusika kuona na kufumbia macho. Hali kadharika eneo hili linasikitisha sana kutokana na wajasiriamali ambao wamezunguka eneo hilo la choo na kuendelea na biashara zao. Hivyo basi ni vyema uongozi husika kutembelea na kujionea hali halisi ili kuwanusuru ufumukaji wa magonjwa kwa abiria watokao Dar- Dodoma ama Dodoma- Dar.

No comments:

Post a Comment