JIFUNZE. Thamani ya mwanadamu huonekana wakati ule akiwa na mchango katika jamii. Aidha kiuchumi, Kimawazo, Nguvu kazi, Kitaaluma na hata Kimichezo. Lakini kile kilichokufanya uwe na thamani punde kinapotoweka, ama potea, Nawe unasahaulika Mara moja.
Wanadamu tuliumbwa na kasumba moja mbaya kabisa. Siku zote tumekuwa tunathamini kilichopo Mbele yetu, na kupuuzia ama kusahau kilichopo nyuma yetu. Kwasababu tu, tunaamini uwepo wa macho mbele yetu, unamaanisha tutazame vya mbele tuu. Tunasahau kuwa tulipewa na uwezo wa kugeuka nyuma pia.
Ndugu, Rafiki, Jirani, Swaiba, Wapenzi, Geuka sasa mtazame alie nyuma yako. Mtazame maskini, omba omba, yatima, mjane, Mlemavu, hata Mgonjwa zaidi ya Mimi alie lala kitandani saa hii kwa maumivu makali asie jiweza, Na yeyote anaenyoosha mkono, wa uhitaji, Geuka na Rudi nyuma kamnyanyue, Muongoze Sehemu sahihi na salama. Na Mungu Atakubariki.
Ikumbukwe kua hata dk 1 ijayo katika maisha yako huwezi bashir nini kitajiri katika maisha yako. Mfano Sekunde zisizo zidi 30 siku napata ajali, Ziliweza nibadili ghafla toka mtu aliyekua akitembea tena kwa majivuno bila maumuvu yeyote, nakua mtu nisie weza japo geuka kitandani pekeangu mpaka sasa. Ninashinda nimelala kwa maumivu makali yakuvunjika Mguu. Sekunde hizo pia ziliweza haribu utekelezaji wa mipango yangu yote ambayo ilikua niwe naendelea itekeleza mpaka sasa, sekunde hizo hizo pia zimeweza nagawa na baadhi ya ndugu jamaa na marafiki kwanamna tofauti tofauti.
Ikumbukwe kuwa Majengo ya Hospital kwa mwonekano wa nje Kwa mtu asie mgonjwa nimazuri na yana mvuto sana. Lakini punde unapokua na matatizo ya kiafya na kuingizwa mule utakutana na mazazingira mabaya sana yasiyo tamanisha hata kiduchu kuendelea kaa mule, nimateso, uchungu, maumivu hasa unapotizama yanayoendelea kwa wagonjwa waliopo jirani nawe wodini na wenye hali mbaya zaidi yako.
Jifunze kugeuka nyuma na kuwatizama wenye matatizo, na wenye uhitaj kama mimi nilivyo kumbukwa na Wasamaria.
Ni mtazamo wangu, na mawazo yangu tuu. Wala isikupe tabu kama inakugusa.
Nimeamua jaribu weka wazi hili, kwa kuwa kwawkipindi kidogo nilicho kitandani sasa nimeweza jionea napia jifunza mambo mengi sana na hata ambayo sikuwahi fikiri wala yajua kabla. Nimeweza Gundua aina ya marafiki, ndugu, jamaa, watu wangu wa karibu, majirani, na hata watu pia nisio wajua juu ya mchango wao na mwitikio wao katika tatizo langu. Siwezi zungumzia hapa lakini picha yote nayo moyoni mwangu.
Mwisho kabisa napenda kuwashukuru wote walio niokota, nikimbiza hospitali, waliotoa magari yao kunipeleka huku nakule mpaka leo. Wanao niwezesha kiuchumi, walio nikumbuka kupitia mitandao ya kijamii, txt, calls, Maombi na sala na hata walio kuja niona macho kwa macho nawashukuru sana. Nawakumbuka wote hata kama ni wengi napia nathamini nakutambua michango yenu. Sitoasahau kiukweli, pia naomba mzidi niombe nizidi imarika kiafya.
Mwisho kabisa napenda kukwambia mtu wangu, Ukitaka jua rafiki wakweli, ndugu wa kweli, jamaa wa kweli, jirani wakweli. Pata tatizo. Majibu yote utayapata hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: