Na MatukiodaimaBlog
MKOA wa mbeya umepania kuboresha miundo ya kituo cha mambo ya kale cha Kimondo wilayani Mbozi mkoani hapa iwapo Idara ya Mambo ya kale iliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii itakubali ombi la mkoa huo kukabidhi kivutio Halmashauri ya Mbozi.
Hatua hiyo imekuja kufuatilia ziara ya wanahabari mkoani Iringa wanaotembelea vivutio vya utalii mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa kama njia ya kuhamasisha utalii mkoa ya nyanda za juu kusini na pia kubaini sababu za utalii kutokua kwa kasi katika mikoa hiyo .
Mhifadhi msaidizi wa kituo cha makumbusho ya mambo ya kale ya Kimondo
wilayani Mbozi Bw Mussa Nsojo alisema kuwa mbali ya watalii wengi kupenda kutembelea eneo hilo la Kimondo ila miundo mbinu ya eneo hilo si rafiki kwa watalii kuendelea kutembelea kutokana na serikali kushindwa kuboresha majengo na eneo hilo kwa ujumla.
Alisema kuwa kimondo hicho ambacho mwaka kilipoanguka eneo hilo haufahamiki ila utafiti wake ulianza kati ya mwaka 1930 -1931 na kubainika kuwa si jiwe la kawaida bali ni sayari iliyoanguka kutoka angani toka wakati huo kimendelea kupata umaarufu wa watalii kufika kutembelea eneo hilo japo katika eneo hilo mazingira yake ni mabovu zaidi.
Mhifadhi huyo akielezea historia ya kimondo hicho alisema kabla ya
watafiti kubaini kuwa ni kimondo miaka ya nyuma kulikuwa na wenyeji ambao walikuwa wakiishi eneo hilo na mkazi mmoja aliyefahamika kwa jina la Harele ambae alikuwa akifanya kazi ya uhunzi kuweza kubaini jiwe hilo la ajabu wakati akitafuta udongo chuma kabla ya kumega kipande kidogo na kutengenezea shoka .
Alisema kutokana na wakati huo chuma kuwa na dhamani kubwa alipeleka
taarifa kwa chifu wa eneo hilo na kulifanya eneo hilo kuwa la tambiko kabla utawala wa Waingereza kuchukua eneo hilo na kulihifadhi kabla ya serikali ya Tanzania kupitia idara ya mambo ya kale kuhifadhi eneo hilo.
Kuhusu changamoto kubwa zilizopo eneo hilo alisema ni pamoja na kukosekana
kwa nyumba bora za watumishi ,jengo la ofisi ya makumbusho kutokana na kibanda kilichopo kutokuwa na sifa ya utalii ,pia miundo mbinu ya barabara kufika kituoni hapo.
Afisa utalii ofisi ya utalii kanda ya kusini Bi Risala Kabongo akielezea kivutio hicho alisema kuwa ni moja kati ya vivutio visivyo vya kawaida hapa nchini na kuwa iwapo serikali itaboresha zaidi eneo hilo upo uwezekano wa uchumi wa mkoa wa Mbeya kukua zaidi kupitia kivutio hicho .
Kivutio hiki kinavutia zaidi ila ushauri wangu kwa serikali kuboresha miundo mbinu ikiwa ni pamoja na kutenga eneo la banda la wageni na eneo la kujenga mahema kwa wageni.....Kimondo hiki kimetoka katika sayari ya Mars na hivyo ni kivutio cha ajabu zaidi"
Katibu tawala msaidizi (miundombinu) mkoa wa Mbeya Kastory Msigala alisema kuwa mkoa huo kupitia kikao chake cha kamati ya ushauri ya mkoa kimeiandikia barua idara ya mambo ya kale ili kuipa eneo hilo la Kimondo Halmashauri ya Mbozi ili kusimamia kwa lengo la kuiboresha zaidi.
Kwani alisema shida kubwa ya Halmashauri hiyo na mkoa kushindwa kuboresha majengo na miundo mbinu inayozunguka makumbusho hayo ni kutokana na kutokuwa na mamlaka ya kufanya hivyo kutokana na usimamizi wa eneo hilo kuwa chini ya idara ya mambo ya kale ila pale idara hiyo itakapokabidhi katika serikali ya wilaya upo uwezekano wa wilaya kusimamia vizuri zaidi.
Alisema katika mkoa huo kuna jumla ya vivutio 13 vilivyotambuliwa kikiwemo kivutio hicho cha Kimondo na kuwa mbali ya vivutio hivyo bado mkoa umejipanga zaidi kutangaza utalii kufuatia ushirikiano mkubwa uliopo kati ya mkoa huo na ofisi ya SPANEST, bodi ya utlii ,wizara ya utalii na wadau mbali mbali kukuza utalii mkoani humo .
|
Toa Maoni Yako:
0 comments: