Waziri wa Katiba na Sheria (Kulia), Mathias Chikawe akijandaa kuvaa kofia ya kujikinga (Helmet) kabla ya kuanza ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) linaloendelea kujengwa katika mtaa wa Makunganya jijini. Kushoto ni Afisa Mteandaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) Phillip Saliboko akitoa maelezo mafupi kwaWaziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe (kulia) kabla ya kukagua jengo lao lililopo mtaa wa Makunganya jijini.
Waziri wa Katiba na Sheria , Mathias Chikawe akifafanua jambo mara baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la RITA. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko.Na Mwandishi Wetu
---
Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe amesema kuwa amefuraishwa na manedeleo ya ujenzi wa jengo la Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) na kutangaza rasmi kuwa atamuomba Rais Drk Jakaya Mrisho Kikwete kulifungua rasmi jingo hilo mwishoni mwa mwaka huu.

Waziri Chikawe alisema hayo wakati alipotembelea maendeleo ya ujenzi wa jingo hilo lenye ghorofa 27 katika mtaa Makunganya jijini karibu na ukumbi maarufu wa burudani wa Club Billicanas.

Alisema kuwa amefuraishwa na kitendo cha kampuni za kizalendo kuhusika kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha wa jingo hilo ambalo litakuwa la pili kwa urefu ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Alifafanua kuwa ukiondoa mkandarasi mkuu, kampuni ya China Railway Jianchang Engineer (T) Limited, kampuni nyingine zilizobaki katika kufanikisha ujenzi huo ni za kitanzania.

Kampuni hizo ni Undi Consulting Group Limited ambayo inahusika na mradi wa ujenzi huo, Design Concern (iliyofanya kazi ya kubuni na kuchora ramani ya jengo) na kampuni ya Kamu Cost Engineering Centre ambayo ilifanya savei ya ujenzi wa jengo.

Kampuni nyingine ni Unicool (East Africa) Company Limited, Sec (East Africa) Company Limited, Techno Image Limited na Derm Electrics (T) Limited.

“Haya ni maendeleo makubwa kwa Tanzania kuona makampuni ya kizalendo yanatumika katika kufanikisha ujenzi wa majengo ya kisasa kama hili la RITA, ni jengo lenye ubora wakimtaifa, nimevutiwa na maendeleo ya mradi na nitamuomba Mheshimiwa Rais, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuja kulifungua rasmi,” alisema Chikawe.

AfisaMtendajiMkuuwa RITA, Phillip Saliboko alisema kuwa ujenzi wa jengo hilo umegharimiwa na Mfukowa Hifadhi ya Jamii wa (NSSF) na utagharimu shs 35.86 Bilioni ambazo zitalipwa kwa kipindi cha miaka nane kwa mujibu wa makubaliano yao.

Saliboko alisema kuwa mbali ya ofisi yao ambayo kwa sasa ipo Upanga kuhamia hapo, jengo hilo pia litapangishwa kwa makampuni na taasisi nyingine kama kitega uchumi chao.

“Jengo letu ni la kisasa, lina vifaa maalum vya kuzuia ajali za moto ikiwa pamoja na milango ambayo moto hauwezi kupenya na kusambaa, kwa kweli tumewekeza kwa kiasi kikubwa na kwa kuzingatia usalama wetu na wapangaji wengine,” alisema Saliboko.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: