Mtanzania
Rajabu Maoja anajifua ili kumpa kipigo cha aina yake bondia wa
Namibia Gottlieb Ndokosho katika mpambano wao wa kugombea ubingwa wa
Afrika unaotambulika na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF).
Mpambano huo uliopewa jina na “Vita ya Jangwa la Kalahari”
utafanyika katika jiji la Windhoek, nchini Namibia tarehe 29 mwezi
huu.
Mtanzania
Rajabu Maoja ni mmoja kati ya mabondia waliojizolea sifa kemkem
katika mchezo wa ngumi za kulipwa akiwa na makao yake katika jiji la
Tanga.
Maoja
amepigana mapambanoi 32 wakato Ngoboko ameshaingia ulingoni mara 14
akishinda mapambano yote.
Wawili
hawa watakutana katika ukumbi wa SKW Hall, Olympia ulioko kusini
mashariki mwa jiji la Windhoek, nchini Namibia, ukumbi huu ndio
mabandia wengi wa Namibia wanapokutana na mabondia wengi kutoka nje
kila mara.
Mpambano
wa Maoja na Ndokosho unaratibiwa na Kinda Promotions chini ya promota
mahiri nchini Namibia bwana Simon Nangolo anayeishi katika jiji la
Windhoek!
Bodi
ya ngumi na mieleka ya Namibia itasimamia mpambano huo wakati Rais wa
IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Urarabuni na
Ghuba ya Uajemi, Mtanzania Onesmo Ngowi atakuwa ndiye msimamizi mkuu
wa mpambano huo!
Katika
mapambani ya utangulizi bondia Cecilia Pitiseni kutoka nchi ya
Zimmabwe atakungutana na bondia wa Namibia.
Mapambano
haya yanayotambuliwa na IBF yako katika mpango kabambe wa programu ya
“Utalii wa Michezo” ambao IBF/USBA imeridhi kuufadhili na
kuuendesha katika bara la Afrika. Tanzania na Ghana ni nchi za
majaribio!
Programu
hii itawapa mabondia wengi wa Kitanzania nafasi kadhaa wa kadha za
kugombea mikanda ya IBF sehemu mbalimbali duniani na kuitangaza ya
Tanzania!
Rais
wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya kati, Ghuba ya Urarabu na
Uajemi anawahimiza watanzania watumie fursa hii kuzitangaza biashara
zao kupitia programu hii!
Anazihimiza
pia taasisi za kibiashara, watu binafsi na mashirika yanayotoa huduma
kwa jamii kuitumia programu hii ya IBF kujitangaza.
Toa Maoni Yako:
0 comments: