Na Andrew Chale.

“KIPAJI  si umri  ni uwezo kwa kila mwanadamu aliyebarikiwa na kutumia kipawa alicho nacho.”

Hivyo ndivyo anavyoanza kuzungumza Mtunzi wa mashairi  Mohamed  Juma Shaaban (20)  mkazi wa mjini  Zanzibar .

Mohamed ambaye ameshatoa kitabu cha “If tomorrow Comes” alisema hayo katika mahojiano  na mwandishi wa makala hii.

Anasema kitabu cha mashairi cha “If tomorrow Comes,”  alichokitoa kwa mara ya kwanza mwaka 2010 jamii imekipokea.

Kupitia kitabu hicho anasema alipokea maoni mbalimbali ya kumpa moyo ikiwemo ya kuandaa kitabu kipya, maoni ambayo ameweza kutafanyia kazi kwa kutunga kingine cha “Hope Never Decays.”


Mohamed anasema kitabu cha “Hope Never Decays” chenye mashairi zaidi ya 65, kimejaa mafunzo mbalimbali ambayo yamegusa jamii na taifa kwa ujumla.

Kitabu hiki kinatarajiwa kuzinduliwa visiwani Zanzibar huku Agosti 20 na  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  Zanzibar, Ramadhan Abdulla Shaaban ambaye atakuwa ni mgeni rasmi.

Akielezea histori ya maisha yake, Mohamed anasema yeye ni mtoto wa nne kati ya watoto watano wa familia ya Mzee Juma Shaaban, na kusema alizaliwa Agosti 30, 1990 visiwani Zanzibar .

Anasema tangu alipokuwa mtoto alikuwa na uwezo mkubwa wa kusoma vitabu vya watoto.

Mohamed anasema mwaka 1998 hadi 2002 alipata elimu yake ya awali kwenye Skuli ya Msingi Mombasa na kisha kuamia kwenye Shule ya  High View international visiwani humo hiyo ilikuwa mwaka 2003, na kusoma darasa la sita hadi la saba mwaka 2004.

Alipokuwa shuleni hapo alieweza kutumia muda wake mwingi kujihusisha na usomaji wa vitabu na alipoaingia elimu ya sekondari mwaka 2005 alitumia masomo yake vema.

Mohamed anasema akiwa kidato cha nne, alipenda somo la Fasihi, ndipo alipopata msukumo mkubwa wa kujituma kutunga mashahiri.

“Masomo yote niliyapenda ila ili la Fasihi kidato cha nne nililipenda zaidi kwani nilitumia muda wangu mwingi kuhakikisha nasongambele ili kutimiza ndoto yangu ya kuwa mtunzi mahiri Barani Afrika,” anasema Mohamed.

Anasema kwa kutumia elimu ailiyopita na uwezo alionao, mwaka 2010  alifanikiwa kutoa kitabu cha mashairi kwa mara ya kwanza  kilichojulikana kwa jina la “If tomorrow comes,” kilichokuwa na jumla ya mashahiri 40.

Kitabu hicho anasema kipo kwenye lugha ya Kiingereza, lakini kilipendwa na watu mbalimbali, hapo  ndipo alipopata msukumo wa kutoa kitabu cha “Hope Never Decays,” anachokizindua  Agosti 20.

Mohamed akikielezea kitabu hicho anasema mashairi yake yamejaa kila aina ya mafunzo ambapo kimetoa taswira mbalimbali kwa jamii  juu ya kujiamini na kufanya jambo bila kukata tamaa.

 “Maana halisi ni juu ya mtu aliye na mabadiliko kwenye uchumi, kijamii na siasa  na ambaye atakuwa na matumaini, kwani matumaini hayaozi,”anasema.

Akielezea kwa nini amekuwa akitoa vitabu vyake vya mashairi kwa Kiingereza na sio Kiswahili, Mohamed anasema kutumia Kiingereza ni kutanua wigo wa kujuilikana kwenye anga za kimataifa kwani ametoa fursa ya kupata radha tofauti kwa wasomaji ambapo wengi wa watunzi nchini wamekuwa wakitunga mashairi kwa Kiswahili.

“Watunzi wengi wanatumia lugha ya Kiswahili kwenye vitabu vyao hivyo nimeona ni bora nitumie Kiingereza ili kuwafikia watu mbalimbali ikiwemo kuleta Soko la Afrika mashariki, Afrika  na duniani kote… hii itasaidia kuinua soko la ndani na nje,” anasema Mohamed.

Anasema amegundua wengi wa Watanzania wamekuwa wakinunua vitabu vya mashahiri na hadithi kutoka nchi jirani vilivyo na lugha ya Kiingereza zikiwemno nchi za Nigeria , Kenya na Ulaya.

Kwa kutumia Kiingereza anasema  wasomaji waliokuwa wanatafuta vitabu vya nje watapata fursa ya kusoma kwa sasa.

Kwenye kitabu cha “Hope Never Decays,” anasema kuna mafunzo kwa jamii kuacha kuvunjika moyo kwa matumaini yao mazuri kwani tumaini jema haliozi wala haliaribiki kamwe.

“Kuna shairi linasema kijana asikate tamaa zaidi andelee mbele kwani mambo ya ulimwengu ni mengi anatakiwa kuachana nayo bila kuyaweka rohoni hakika atafanikiwa, hii ni pamoja na aliye na kipaji akiendeleze hakika atafanikiwa,” Mohamed ananukuu mistari ya baadhi ya shairi hilo .

Katika kitabu hicho kipya cha mashairi chenye mashairi 65, baadhi ya mashairi hayo ni pamoja na “Time will tell,” “Tomorrow will come,” “Last coin,”  “My Africa,” “ Some tears,”  “Yes I can,” “Beyond your verge,” “Better Dew the no rain,” “Freedom song” na mengine mengi.

Akielezea kwa kifupi baadhi ya mashahiri hayo, likiwemo shairi la “Last coin,” anasema ni juu ya mtu aliyebakiwa na kiasi kiduchu cha fedha ambayo hawezi kuitumia kwa lolote ambayo haitoshi kununua sumu au kununulia dawa ya kuweza kumsaidia kuishi.

Mbali na na shairi hilo kuna shairi la “Better Dew than no rain,” ambalo linaelezea kuridhika kupata kidogo kuliko kusubiria kitu usicho na uhakika nacho.

“Shairi ili linaelezea ni jinsi gani mtu anaweza kuamini kile kidogo alicho nacho kuliko kufikiria kikubwa…bora matone ya asubuhi kuliko kutegemea mvua ambayo hujui kama itakuja kunyesha,” anasema Mohamed.


Mohamed ana ndoto ya kuwa mtunzi mahiri wa kimataifa wa mashairi na kuhakikisha anasonga mbele kama walivyokuwa watunzi wakubwa wakiwemo Shaaban Robert   na watunzi mbalimbali wa mashahiri na riwaya duniani.

 “Namshukuru Mungu kwa kunijaria uwezo na hekima ambayo imeweza kuniongoza siku zote mpaka kufanikisha kukamilisha kazi yangu ya utunzi wa kitabu cha “Hope Never Decays,” kitachokuwa mwanga kwa watakaokisoma,” Mohamed anasema.

Kwa wasomaji na wauzaji wa vitabu wa jumla na reja reja kwa watakaohitaji wanaweza  kuwasiliana na mtunzi wa kitabu hichi Mohemed ‘MJ’ kupitia +255714460595, anapatikana Zanzibar , Tanzania

Ama mwandishi  wa habari hizi, Dar  es Salaam, Tanzania, 0719076376
chalefamily@yahoo.com
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: