Msanii wa muziki wa kizazi kipya ajulikanaye kwa jina la Mwanaisha Nyange a.k.a Dayna anatarajia kuachia ngoma yake jumamosi hii katika vituo mbali mbali vya redio ijulikanayo kwa jina la 'Nivute kwako' aliyoshirikiana na msanii mwenzake aitwaye Barnaba.

Akizungumza na blog hii msanii huyu alisema kuwa nyimbo yake hiyo ni kama muendelezo wa ile nyimbo yake ya 'Fimbo ya Mapenzi' na anasema aliutunga siku yake ya kuzaliwa.

"Wimbo huu nimeutunga kwa siku rasmi maana ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa, wimbo ni mkali sana na unamaneno matamu, melody nzuri na pia mwenzangu Barnaba kafanya vyema sana.

Wimbo huo ambao ameurekodia studio ya Burn chini ya producer, Seddy Clever.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: