Mwanamuziki Shaggy wa Marekani akiondoka kwa kucheza huku akiwa ameshikilia usinga na kusindikizwa na vigoli wa kabila la kisukuma wakati alipokuwa akiondoka katika eneo la tukio mara baada ya kutawazwa kuwa chifu wa kabila la wasukuma, katika tamasha la ngoma za asili la Siku ya Mavuno yaani (Bulabo) kwa Kisukuma lililofanyika katika kijiji cha Kisesa mahali ambapo pana makumbusho ya Bujora yaliyohifadhi tamaduni zote za kabila la wasukuma.

Mwanamuziki Shaggy akishangilia mara baada ya kumtawazwa kuwa chifu wa kabila la wasukuma katika kijiji cha Kisesa.Chifu Charles Kaphipa akizungumza katika tamasha hilo la Bulabo kabla ya kumtawaza mwanamuziki Shaggy, wanaosikiliza kutoka kulia ni Chifu Makwaiya, Meneja wa kinywaji cha Serengeti Lager Allan Chonjo Allan Chonjo, Mkurugenzi wa Masoko wa SBL Caroline Ndungu, Mwanamuziki Shaggy na Mzee Mark Bomani.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: