Mwanamuziki wa Reggae na Dancehall wa nchini Jamaica, na mshindi wa tuzo za muziki za Grammy, Mark Myrie aka Buju Banton (pichani), amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kufadhili na kujihusisha moja kwa moja na biashara ya madawa ya kulevya mwaka 2009

Buju Banton amehukumiwa nchini Marekani, na alitiwa hatiani kutokana na ushahidi wa video baada ya kuonekana aki-test cocaine kama ni yenyewe huko pande za Florida.

Awali Banton aliiambia mahakama kwamba hakuwahi kufanya biashara hiyo haramu hata siku moja zaidi ya kuiimba tu kwa majigambo katika sanaa yake ya muziki. Waendesha mashtaka walifuta kesi yao hapo awali baada ya kushindwa kuonesha ushahidi endapo mtuhumiwa wake aliwahi kushiriki moja kwa moja katika biashara hiyo haramu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: