Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network  na mmiliki wa Blog ya The Habari.com Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi. Kutoka kushoto ni  Mkala Fundikira,Shafia Mpanja wa AM,Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale na Khadija Kalili.
 Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.
 Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano.
 Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano.
Baadhi ya Bloggers na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam.
Msanii kutoka TMK Wanaume Family, Amani James aka Mh Temba jana amefikishwa katika mahakama ya mwanzo ya Temeke jijini Dar es salaam akikabiliwa na mashitaka ya kutishia kuua kwa kisu kutokana na wivu wa mapenzi.

Mhe. Temba alipandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka yake mbele ya hakimu Claudia Frank wa mahakama hiyo.


Mheshimiwa Temba alifikishwa mahakani hapo mapema saa 3:00 asubuhi huku akiwa amefungwa pingu chi ya ulinzi wa askari kanzu wa kituo cha Mkoa wa Kipolisi Chang’ombe.

Aliwekwa chini ya ulinzi katika kituo cha mahabusu ya mahakama hiyo kabla ya kusomewa mashitaka yake. Kesi hiyo imesajiliwa mahakamani hapo kwa namba 371 chini ya kifungu cha 89 kidogo cha (2) (a) sura ya 16 ya mwenendo wa sheria ya Makosa ya Jinai.

Akisomewa mashitaka na karani wa mahakama hiyo, Joyce Ngamesha, alidaiwa kuwa Januari 28, mwaka huu, saa 1:00 jioni katika baa ya Scorpion iliyopo Temeke jijini Dae es salaam, mshitakiwa alimtishia kumchoma kisu Godrey Deogratius ama Sulla.

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na yupo nje kwa dhamana.

Hakimu Frank alisema kesi hiyo itasikiliza ushahidi March11,  mwaka huu,. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Mshitakiwa alifikishwa katika kituo cha polisi cha Chang’ombe akituhumiwa kutishia kumchoma kisu mlalamikaji kwa madai ya kuwa na mahusiano wa kimapenzi na mke wa msanii huyo.


Ilidaiwa kuwa mshitakiwa alimtishia kumchoma kisu mlalamikaji huku akijua ni kinyume na sheria.
Askari wa upelelezi mkoa wa Morogoro waliofanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa Francis James Washa (24) aliyevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), askari wa kike mwenye tisheti ya mistari ni WP Agnes, mwenye silaha ni D/C Alex.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kwenye Kitabu cha maombolezo ya marehemu Esther Gigwa, Mama mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika kushiriki kuaga mwili huo nyumbani kwa mkurugenzi huyo, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea, wakati alipofika kushiriki kuaga mwili wa marehemu mama mzazi wa Mkuruenzi huyo nyumbani kwake, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiifariji, Familia ya wafiwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Edward Hosea na nduguze, waliofiwa na mama yao mzazi wakati Makamu alipofika kushiriki katika shughuli ya kuaga, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR
Wanafamilia wafiwa wakiwa katika shughuli hiyo ya maziko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu mama mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dkt. Ewdard Hose, Mama Esther Gigwa, wakati wa shughuli za maziko zilizofanyika nyumbani kwa Mkurugenzi huyo, Masaki jijini Dar es Salaam, leo Feb 27, 2015. Picha na OMR
A Palestine solidarity group in Ireland on Wednesday launched a billboard campaign to urge the Irish government to support the recognition of Palestine.

Palestine solidarity group Sadaka said that former Irish minister for foreign affairs Micheál Martin, Sinn Féin leader Gerry Adams, and PA ambassador to Ireland Ahmed Abdelrazek urged the Irish government to recognize Palestine based on the two state parameters as part of the campaign.

John Douglas, President of the Irish Congress of Trade Unions said: "The Dáil and Seanad have given the Government a clear mandate to recognize the state of Palestine."

"Ireland's stated policy is that it supports a two state solution in Palestine and Israel. Ireland already recognizes Israel – we should now recognize the State of Palestine."

"Israel, as an occupying power, continues to hold a veto over Palestinian statehood. No country should deny another nation its right to statehood. And, as the maps on these billboards powerfully demonstrate, time is running out for the establishment of a Palestinian state."

The adverts will appear on billboards, buses, bus shelters and train stations in Dublin.

In December 2014, Irish lawmakers urged their government to recognize Palestine as a state in a symbolic motion that sailed through parliament unopposed.

The non-binding motion agreed by lawmakers in Dublin called on the government to "officially recognize the State of Palestine, on the basis of the 1967 borders with East Jerusalem as the capital, as established in UN resolutions".
4
Kitengo wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi Shemweta akikabidhi zawadi kwa Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo tayari kwa mashindano ya NIC Corporate Lugalo Challenge 2015 yanayofanyika kesho February 28 kuanzaia saa 7:00 asubuhi kwenye viwanja hivyo yakishirikisha wachezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Mpaka sasa wachezaji 60 wameshathibitisha kushiriki katika mashindano hayo na wachezaji wengine wanaendelea kujisajiri ili kushiriki katika michezo hiyo ya Gofu, Kapteni Japhet Masai ametoa mwito kwa wachezaji mbalimbali kuendelea kujisajiri na amesema wanatarajia zaidi ya wachezaji 120 watashiriki katika mashindano hayo.

Shindano la NIC Corporate Golf Chalennge linaandaliwa na shirika la bima la taifa NIC na linafanyika kila mwaka kuanzia tangu lilipoanzishwa mwaka 2013 na linashirikisha wachezaji wa rika zote na jinsia zote NIC imeandaa zawadi mbalimbali kwa washindi, ambapo mshindi wa kwanza atapata jiko kubwa la umeme. Pia wshindi wengine watapata zawadi mbalimbali zilizotayarishwa kwa ajili yao ambazo ni meza kubwa ya ofisini, mikoba ya akina mama, mabegi ya wanafunzi, Feni , Friji, Microwave na zawadi nyingine nyingi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 5
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi Shemweta akikabidhi zawadi kwa ya jiko kubwa la umeme Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo 6
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi Shemweta na Japhet Masai Kapteni wa mchezo wa Gofu katika viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo wakipiga picha pamoja na zawadi hizo. 7
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa NIC Bi. Mwanaidi Shemweta akipiga picha mara baada ya kukabidhi zawadi hizo kwenye viwanja vya gofu vya TPDF Lugalo.
Nilipofika ndani nikapanda ngazi haraka haraka akanifuata, wakati huo mie napanda ngazi moja moja yeye mbili mbili kabla sijafika hata mlangoni akanivuta akanishusha chini akasema leo nakuuwa... siwezi penda mwanamke nikampa kila kitu anachotaka kisha anisaliti alinipiga sana pale chini... salama yangu ni kijana wa getini kuja kuniokoa maana nilipiga kelele kama nimekalia moto.

Hakuongea aliponipiga nikaokolewa akaenda kwenye wine space akakaa huko akaanza kunywa wine... huku analia sana... nikaingia chumbani nikaanza kulia asubuhi kufika nikamkuta kalala pale pale juu ya meza ya wine, sikumsemesha kitu... nilivaa nikaondoka kwenda kazini... sijui aliamka saa ngapi?.. ila mida ya mchana akanipigia simu sikupokea... akapiga nikakata akatuma meseji pokea simu mke wangu wala sikupokea.

Niliporudi jioni kaka wa getini akasema shemeji nae kaondoka sasa hivi toka asubuhi ameamka alikuwa analia tu. Kaja rafiki yake wameondoka... sikujibu kitu nikafika.... kidogo ikaingia meseji kwamba nimfate Samaki Samaki kule Mliman City ...nikamjibu siji ... sijakaa sawa akamtuma mtu anifate nikaenda kufika akaniomba radhi sana mbele ya rafiki yake kwa kunipiga... Yeye mwenyewe anajutia kwanini alinipiga aliomba radhi sana nilimshangaaa kukuta anakunywa pombe wakati alikuwa hanywi nikamuuliza Franco... when did you start this???... akajibu Yesterday... and it's becouse of you... basi aliomba radhi na wenzie wakanisihi nimsamehe tukarudi home... that day ilikuwa full malavidavi ... lakini upande wangu niseme kweli yule kijana Kelvin aliniroga jamani... wakati nipo kwenye malavidavi na mume wangu huku namkumbuka Kelvin.

Za mwizi zilifika ambazo hadi leo najiuliza sijui alijuaje hoteli niliyokuwa nimeenda kulala na Kelvin... nawaza hadi leo nakaribia miaka miwili toka nimeachika sijui alijuaje Franco.

Ilikuwa siku ya Jumamosi Kelvin akaniambia kuwa ameninunulia kiwanja Mkuranga niende akanikabidhi... hakusema kama nitalala huko sikujipanga kuaga chochote ... nikamwambia Franco naenda kwenye Chama tuna kikaon huko Mbagala akasema sawa nenda... nikaondoka kufika huko tukakaa bar moja hivi tukala... akaenda kunionyesha hicho kiwanja nikakitazama tulipomaliza kukiona akasema twende kwenye kituo chake kimoja cha mafuta mbele ya Mkuranga.

Wakati huo ilikuwa saa 12 jioni nikamwambia si unajua natakiwa kurudi home akasema ndiyo nafahamu hatukai sana... tulipaki gari yangu nyumbani kwake Kawe tukaondoka na gari yake. I was comfortable kwa vile gari ilikuwa ni full tinted (ukisema uchungulie ndan unajiona sura yako unavyochungulia ndani huoni kitu).

Kufika huko tukatembelea kituo chake nikapaona... Kelvin alikuwa hajaoa kabisa hivyo nilikuwa fee kwake... akaniintroduce kwa wafanyakazi wake kama mkewe mtarajiwa... bad enough nilikuwa nikikutana na Kelvin tu ananiambia toa mapete yako.. na kuna siku alitaka kuzitupa alisema hazipendi ikawa ugomvi basi nikawa nazivua.

Baada ya hapo akaniambia anafeel joto nimsindikize kupaga hoteli moja hivi na akasema hawezi niacha bila kumpa malavidavi nami kuonyesha ushirikiano wa kiwanja kile nikaenda ila kwa makubaliano tukimaliza tunarudi nyumbani ... siku nzima sikuwa nimeongea na wale mabest zangu hata mmoja... tukaenda hotelini huko huko Mkuranga.

Tukiwa hotelini pale baada ya malavidavi akaniambia leo huondoki... simu hii hapa mpigie mmeo sema unavyosema leo tunalala wote nikalia sana akanipokonya funguo za mlangoni... akasema siku nikisikia mme wako kafa nitafurahi sana... hana hadhi ya kumiliki mtoto mzuri kama wewe.

Nililia aniruhusu kuondoka akagoma... basi mida ya saa mbili simu ikaita kucheki ni mme wangu... nikafungua madirisha ili mwangwi utoke nikapokea nikamwambia nimepitia msibani kuna rafiki yangu kafiwa ... akachekaaaaa akasema okay! kwahiyo hurudi? nikasema naweza kuchelewa sana.. akasema haya mke wangu. Nakupenda nikamwambia nakupenda pia. Akakata simu.. hapo nilikuwa na hofu sana.

Nikiwa hapo tulikuwa tumeagiza kuku wa kuchoma nje. Nikasema hatuendi kula nje walete chumbani... basi nilikaa ndani kama saaa moja baada ya kuongea na Franco akapiga tena akasema nipo hapa ulipo naomba nikuone mara moja... Nikashtuka akasema tena unakuja au Mimi nije?... sauti ile ilikuwa kama MTU analia... pembeni nasikia MTU anamwambia Franco utaharibu sasa... nikakata simu.

Nikamuuliza Klevin,  Franco anasema yupo hapa nilipo kuna MTU yeyote ulimwambia tutakuwa hapa leo? Klelvin akajibu huyo mumeo bwege ni muongo anakutishia tu... mie sikumwambia MTU ila niliongea na Rachel asubuhi nikamwambia leo  nakuja kukupa KIWANJA ila sikusema nitakuja hapa.

Simu ikaita tena nikapokea akasema Mke WANGU. Nipo nje... unakuja au nije? Ila sauti yake kama anabana kilio... nikakata simu bila kujibu... Jamani sitakaa kusahau Siku hii huwa nalia sana hapa pia nalia nimekumbuka mbali.

Ghafla simu ya chumban kwetu ikaita... wote tukaogopa kupokea... kidogo mlango wa chumbani ukagongwa... Kelvin akauliza nani? Wakati huo mimi niko hoi jasho linanitoka... mwili unaishiwa nguvu... nikaomba nikasema Mungu wa uzima nitetee kwenye hili naahidi nikitoka salama sitakutenda dhambi tena... nikasahau kama Mungu hasikii maombi ya mwenye dhambi.

Kama mnakumbuka nilikuwa kwenye purukushani za kutaka kumkimbia Kelvin tulipofika... moyo haukuwa na amani kabisa Siku hiyo kwahiyo Kelvin aliuchukua ufunguo ili nisitoroke akawa nao mlangoni kukabaki hakuna kitu chochote cha kuzuia ufunguo mwingine kupita... tukasikia sauti ya muhudumu ikisema Mimi muhudumu fungua mlango.

Kelvin akamfokea... kwanini unasumbua wateja???.. Hii ni sheria ya wapi?? muhudumu kumwamulisha mteja afungue mlango???... hakujibiwa... nikasikia nyayo zikitembea kama zinaondoka vile moyo ukarelax.

Baada ya dakika tano tu nikasikia mlango unafunguliwa ndio nikaju kumbe na hoteli huwa wana funguo mbili mbili na spare... oh! kikubwa zaidi inaniuma mazingira niliyokutwa nayo... Kila nikikumbuka roho inaniuma... I'm crying always.

Nilikutwa nikiwa uchi kabisa nimekaa kwenye kona ya kitanda nimeshikiria MTO... Kelvin akiwa uchi kabisa ameganda kona ya kitanda hajui afanye nini akashika simu...moja haikai wala mbili haikai... anaacha anainuka, anakaaa anaangalia pa kukimbilia... mwisho akasema niingie uvungu wa kitanda... rum tulochukua INA vitanda vya box vile vikubwa sana havina uvungu akatoa godoro ili niingie kupotia chaga za kitanda... ndipo mlango ulipofunguliwa nikiwa nimesimama natafuta pa kuitetea ndoa yangu.

Endelea kufuatilia sehemu ya tano bila kukosa ya sita ambayo itakuwa ya mwisho...
Nilizaliwa kwenye familia ya watoto sita nikiwa mtoto pekee mwenye albinism. Mama alitupenda na anatupenda sawa bila kujali hali yangu na kunifanya nijione sawa na wenzangu. Tunapendana sana. (Pichani ni Bi. Clara Peter akiwa na mwanae).
Nilizaliwa kwenye familia ya watoto sita nikiwa mtoto pekee mwenye albinism. Mama alitupenda na anatupenda sawa bila kujali hali yangu na kunifanya nijione sawa na wenzangu. Tunapendana sana. 

Hali hii ilinifanya nisijute na wala haitokaa itokee nijute kuzaliwa na hali (mwenye albinism). Mungu aliniumba kwa kusudi lake, kusudi maalum na wala si kwa bahati mbaya. Ila kusudi hili linaharibiwa na kukatishwa na baadhi ya wapumbavu (wauaji) wenye fikra mgando. Ila bado sijakata tamaa nitapambana mpaka dakika za mwisho za pumzi yangu.

Moyo wangu unavuja damu, damu na maji, japo bado nina tumaini la kuishi, moyo wangu huu umekunja ngumi ambayo sijui itatua kwa nani kwani adui yangu simjui. Je Ni familia, wazazi na ndugu zangu, majirani na marafiki au watu kuja nisowajua?

Hivi ni nani hasa anayedhamini mauaji haya ya kikatitili kwa watu waenye albinisim? Hakika hii ni system pana tena pana sana yenye kujitosheleza katika kila Nyanja. System inayolindwa kama nyara za serikali ama hata zaidi ya nyara hizo, kwani siamini kama serikali yetu hii ya maisha bora kwa kila mtanzania imeshindwa kuwakamata wahusika. 

Muda mwingine najiuliza hivi mauaji haya yanasababishwa na imani za kishirikina tu au kuna mengine chini ya mwamvuli huu mpana wa imani za kishirikina? Mh! Mimi na wewe hatujui. Na je soko kuu la bidhaa hizi haramu lipo wapi na nani ana hisa nyingi? Pia mimi na wewe hatujui. Kuna connection gani kati ya hawa majasusi wauaji na watunza usalama? Mbona inakuwa ngumu kuwatia mikononi mwa sheria? ama kwa hakika kuna jambo zito ambalo limejificha chini ya kapeti ambalo mimi na wewe hatuljui.

Naamini kwa kutumia teknolojia ya sasa na hasa ya mawasiliano kuyakamata haya majitu mauji kuanzia jani, tawi, shina na hata mzizi wake, mwezi ni mrefu.

Mtukufu Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete watu wenye albinism tunakulilia baba tunaomba utuokoe sisi wana wa Israel tunapukukutika kwani tunaamini AMRI yako itasaidia kusitisha tatizo hili ikiwemo ya kunyongwa mpaka kufa kwa wote waliobainika kuhusika na uchafu huu. 

Tunaomba haki itendeke kwa familia zilizopoteza wapendwa wao na wahanga wote. Tunahitaji uhuru katika nchi yetu, tunahitaji amani na upendo. Mbona tuishi kwa kujifichaficha kama wahalifu wa mihadarati katika nchi yetu? Hatuna hatia wala hatuna bahati yoyote badala yake tumekosa vimelea vinavyosababisha rangi ya asili (melanin) MSITUUE hakuna tulichotofautiana. 

WE NEED NO WE DIMAND JUSTICE
03
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama kazi ya uandiskishaji wapiga kura baada ya ya kuzinua Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako.
 .06
Baadhi ya watalaamu wa kuandikisha wapiga  wakiwa na zana  za kazi kabla ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kuzindua Uborereshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako.
---
Kazi ya kuandikisha wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kupitia mfumo wa Biometrick Voters Registration (BVR), ambao huhusisha uchukuaji wa alama za vidole na picha, jana iliingia siku ya tatu, huku baadhi yao wakipongeza utendaji wake.
Kwa mujibu wa ripoti iliyokusanywa na mwandishi wetu inasema kuwa tokea siku ya kwanza lilipoanza zoezi hilo lilionyesha matumaini maana wananchi wetu walijitokeza kwa wingi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi katika vituo vya uandikishaji, wananchi hao walisema kuna mabadiliko ukilinganisha na siku zilizopita, hivi sasa kazi zinafanywa haraka.
“Watu wanaokwenda kwenye vituo kujiandikisha idadi yao ni kubwa kuliko hata makadirio ya tume, kama hawataongeza muda au vifaa, siku saba walizopanga, hazitatosha na wengi wataachwa bila ya kujiandikisha,” alisema.

Baadhi ya waandikishaji na wasimamizi wa mashine wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuongeza muda ili kazi hiyo ifanyike kwa ufanisi zaidi.
66
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua  Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva na Katikati ni Katibu wa Tume hiyo, Ndugu Malaba.
02
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekititi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva (kushpoto) , Naibu Katibu Mkuu  na Katibu Mwenezi wa CHADEMA, John Mnyika (kulia), Yusufu Mbungiro ambaye ni Afisa Uchaguzi na Mafunzo taifa wa Chama cha CUF (wapili kushoto) na Allan Bujo ambaye ni Mkuu wa Ulinzi wa CHADEMA baada ya kuzinua Uborereshaji wa Daftarila Kudumu la Wapigakura  katika mji mdogo wa Makambako.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kulia) akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe Shabaan Kondo Kissu Februari 25, 2015, anayeshuhudia katikati ni Katibu Tawala wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Shabaan Kondo Kissu akitia saini hati ya kiapo cha kuwa Mkuu wa Wilaya mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa Februari 25, 2015, anayeshuhudia katikati ni Katibu Tawala wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe. Shabaan Kondo Kissu Katiba ya Tanzania kama muongozo katika kazi yake baada ya kumuapisha Februari 25, 2015.
Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Mbunge wa kuteuliwa, Al Shaimar Kweigyir, amtembelea majeruhi wa tukio la uporwaji wa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino,Yohana Bahati, aliyetekwa nyara na kukutwa akiwa amekufa.

Katika ziaraa hiyo kwenye Hospitali ya Bugando jijini Mwanza, Mh Shaimar aliongozana pia na Katibu Tawala Msaidizi wa Ofisi ya Mkoa wa Mwanza, Crencencia J`oseph na August Tesha, ambaye ni Meneja wa Baypor Financial Services mkoani Mwanza.
Wakiwa Hospitali ya Bugando, Mbunge Shaimar na alioambatana nao alipata fursa ya kuzungumza na wahudumu katika wodi aliyolazwa Ersther ambaye ni wa Yohana na kumfariji katika kipindi kigumu cha kuuguza majeraha yake pamoja na kulia msiba wa mwanae.

Tukio la utekaji na uporwaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi limezidi kushika kasi, ambapo kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wadau hususan wale wenye ulemavu wa ngozi akiamini kuwa serikali imeshindwa kuwapatia ulinzi wa kutosha.

Akiwa jijini Mwanza, Mbunge Shaimar na taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services watakuwa kwenye safari ya kuelekea wilayani Kwimba kwa ajili ya kwenda eneo alilokuwa akiishi Ester na watoto wake, hususan wawili kati ya watano waliobaki wakiwa ni albino.
Mbunge wa kuteuliwa Shaimar Kweigyir katikati akiwa na bibi wa Yohana Bahati (Tabu Maganiko) kulia ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyeuawa hivi karibuni mkoani Mwanza, huku mama yake akiachwa na majeraha makubwa wakati wanagombania mtoto katika tukio hilo la kusikitisha. Kushoto kwake ni Mweka Hazina wa Chama Cha Albino Tanzania Abdullah Omari.
Katibu wa Mheshimiwa mbunge, Semeni Kingalu, kulia akipiga picha wakati walipomtembelea majeruhi Ester Maganiko, ambaye mtoto wake Yohana Bahati mwenye ulemavu wa ngozi aliuliwa katika tukio hilo la kusikitisha. Anayefuata ni Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Bugando na Clencencia Joseph, Katibu Tawala Msaidizi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza.

 Kinyesi kikiwa kimehifadhiwa ndani ya chumba cha mwalimu

Maulid Liuguyo ambaye ni mfanyakazi wa Manispaa ya Temeke kitengo cha usafi akishiriki katika zoezi hilo. 
Mfanyakazi wa Manispaa ya Temeke Kitengo cha Usafishaji, Ramadhani Athuman akiweka dawa katika vyombo alivyokuwa akitumia kuhifadhia kinyesi mwalimu Gaudensia Albert wa Shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar es Salaam, kabla vyombo hivyo havijaenda kutupwa dampo. (Picha na Francis Dande)



 Umati wa watu ukiwa nje ya nyumba wakati zoezi la kuteketeza kinyesi likiendelea.
 Mlango ukivunjwa ili maofisa wa afya waweze kuingia ndani ya chumba cha mwalimu.

Na Mwandishi Wetu

Manispaa ya Temeke leo imeteketeza kinyesi kilichokutwa katika chumba cha mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Gaudensia Albert baada ya maofisa wa afya wa manispaa hiyo kuchukua hatua hiyo ili kunusuru afya za wakazi wa eneo hilo.

Kazi hiyo ilifanyika majira ya saa tisa alasiri katika eneo la Yombo, Kisiwani Kata ya Sandari jijini Dar es chini ya uangalizi wa Jeshi la Polisi na wakishirikiana na Mwanyekiti wa Mtaa huo, Yahya Bwanga.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini wakati wa zoezi hilo, Ofisa Afya wa Manispaa ya Temeke, Floyd Tembo alisema tukio hilo walilipata juzi juzi jioni, baada ya kulipata waliwatuma Watendaji wa Afya wa Kata hiyo wafanye utafiti wakujua tatizo hilo lilikuwa na ukubwa gani.

“Baada ya kufanya utafiti wao pia walimpata mhusika, ambapo tulischukua jukumu la kwenda kumhoji Mkuu wa washule hiyo ili kujua kama mwalimu Gaudensia alikuwa na akili timamu au la, hata hivyo, Mkuu wa shule atueleza kuwa alikuwa na akili timamu,”alisema Tembo.  

Alisema pamoja na kuutekeza mlundikano huo wa kinyesi pamoja mikojo na matapishi bado wanaendelea na utaratibu wa kumfikisha mwalimu huyo kwenye vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka.

“Hili tukio halihusiani na ugonjwa wa akili inawezekana kuna tatizo lingine ingawa hatuwezi kuamini mambo ya ushirikina lakini haiwezekani mwalimu kama yule ajisaidie na kuhifadhi uchafu kama ule ndani,”alisema.

Aidha, alisema mwalimu huyo hakuweza kufika kwenye eneo la tukio hali iliyofanya mlango wa chumba chake uvunjwe chini ya uwaangalizi wa polisi.

Tembo, alisema mwalimu huyo alishindwa kutokea kwenye eneo la tukio kwa vile alipelekwa Hospitali ya Temeke kisha kuhamishiwa Haspitali ya Taifa muhimbili kwa ajili ya kupimwa afaya baada ya kupata mshituko ambao umesababishwa na taarifa hizo.

Afisa Afya wa Usafi wa Mazingira, Jumamne Muhogo, alisema uchafu walioubaini ulikuwa ni uchafu wa kinyesi, mikojo na matapishi inasemekana kuna kipindi alikuwa anatapika.

Pia alisema kipo kifungu cha sheria, walifika pale maofisa kutoka idara mbalimbali kupima uzito wa tukio, ambapo kama wangemkuta wangemkamata kwa hatua za kimfikisha mahakamani.

Mhogo, alisema hata kama alikuwa mtaalamu wa sayansi, alikuwa amehifadhi uchafu ule kwa ajili ya utafiti basi hayo yote angekwenda kuyaeleza mahakamani. 

“Tukio hili kwa manispa ya Temeke ni la kwanza kutokea yani inaekekea huyu mtu hana akili ya kawaida kama angekuwa na akili za kawaida asingeweza kufanya na mna hii,”alisema.

Umati mkubwa wa wakazi wa eneo hilo walikusanyika kwa wingi tangu saa tatu asubuhi wakisubiri kazi hiyo hadi ilipofnyika saa tisa jioni na wataalamu wa manispaa hiyo.

Wataalamu hao walimwagia dawa uchafu huo kisha kuanza ubeba na kutumbukiza chooni kwa uangalifu mkubwa.

Walipomaliza walvisafisha vyombo hivyo kwa kutumia dawa ambazo zimeweza kusaidia kuondoa harufu mbaya iliyokuwa imezagaa hewani.

Awali, Sajenti wa Jeshi la Polisi  Ramadhan Kagolo, alisema aliwajibika kusimamia kuvujwa kufuli la chumba hicho kwa vile kazi iliyokuwa ikifanyika likuwa ni kwa ajili ya kulinda afya ya jamii.

Tukio hilo ambalo limekuwa likifuatiliwa na majirani hususan jana wakati wa uteketezaji lilitokea Februari 22 mwaka huu.  

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha miaka mwili jela au kulipa faini ya shilingi laki tisa baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa hayo.

Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.

Hata hivyo, Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu leo imemwachia huru mwanamuziki huyo baada ya kulipa faini ya 900,000.
KUMEKUWA NA TABIA MBAYA KWA SISI WADADA WA SIKU HIZI, ETI MTU HATAKI SHULE, HAFANYI KAZI HUKU AKISEMA ATAOLEWA NA MWANAMME TAJIRI ILI AWE NA MAISHA MAZURI.

-ANASAHAU KUWA PESA ZA MWANAMME NI ZA MWANAMME.

-ANASAHAU KUWA SAA NYINGINE HUYO MWANAMME MWENYE PESA ANAWEZA AKAUGUA AKASHINDWA KWENDA KAZINI KWA MIAKA.

-ANASAHAU KUWA HUYO MWANAMME MUNGU ANAWEZA AKAMCHUKUA NA AKABAKIA YEYE NA WATOTO HUKU AKITAZAMANA USO WA DUNIA.

- ANASAHAU KUWA KUNA KUACHWA/KUACHIKA KWENYE NDOA.

HEBU JIULIZE WEWE LEO HII HUYO MWANAMME AKIONDOKA KATIKA MAISHA YAKO UTAWEZA KUSURVIVE HAYA MAISHA?

HEBU TUACHE FIKRA POTOFU ZA KUTAKA KUOLEWA NA WANAUME WENYE PESA ILI MAISHA YAWE VIZURI.

FANYA KAZI, SOMA KWA BIDII NA UJITENGENEZEE MAISHA MAZURI WEWE MWENYEWE KWANZA ILI HATA MMEO AKIPATA TATIZO LA UCHUMI UWEZE KUBEBA FAMILIA.

USAIDIZI WAKO USIWE WA KUTUMIA TU ATM YA MWANAMME USAIDIZI WAKO UWE PALE AMBAPO MWANAMME AMEKWAMA NA WEWE UNAMBEBA.
Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA imetoa tamko kuhusiana na malalamiko kutoka kwa watumiaji wa huduma za simu nchini kufuatia kubadilika kwa vifurushi vya mawasiliano.

Malalamiko hayo yalikuja baada ya baadhi ya mitandao ya simu kupunguza ukubwa wa data anazopata mtumiaji wa simu anapojiunga na vifurushi vya muda wa maongezi, sms na data kwa pamoja.

Baadhi ya mitandao imekuwa ikitoa Mega Bytes 8 peke yake ambazo kwa matumizi ya kawaida ni ndogo mno.

“TCRA imechambua mpangilio wa vifurushi – tozo za zamani na mpya na kugundua kwamba ingawaje baadhi ya watoa huduma wamebadilisha bei, kwa ujumla bei za muda wa kuzungumza na idadi ya meseji hazikubadilika sana. Hata hivyo, kuna upungufu mkubwa kwa idadi ya uniti za data (MBs),” amesema Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumanne.

Kupitia kifungu cha 5 cha Kanuni za tozo (EPOCA Tariff Regulations) za mwaka 2011, TCRA imeyataka makampuni ya simu kuwasilisha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania gharama mpya wanazokusudia kutoza wateja wao kabla hazijaanza kutumika. Pia imeyataka kupitia upya bei na tozo mpya kwa kuzingatia mapendekezo hayo na kuwasilisha kwa Mamlaka kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Kanuni za EPOCA za 2011 kuhusu tozo.

“TCRA inawaagiza watoa huduma kuhakikisha kwamba mabadiliko yoyote yanatekelezwa kidogo kidogo na sio ya ghafla ili kuepuka sintofahamu katika soko,” imesema.

“TCRA inawaagiza watoa huduma kuwapa wateja wao nafasi ya kuchagua mpangilio wa vifurushi tofauti kwa huduma wanazohitaji: Kifurushi cha mazungumzo, Meseji na Intaneti cha siku, siku saba au mwezi ambacho kinampa mtumiaji uhuru wa kuchagua kiasi ambacho wako tayari kulipia kwa mazungumzo, meseji na intaneti.”

“TCRA inawashauri watumiaji wa huduma za mawasiliano kuchagua vifurushi na mpangilio wa tozo ambao unafaa kwa matumizi yao. Watumiaji wanatakiwa kudai taarifa kamili kuhusu huduma wanazozilipia na waelewe taarifa za watoa huduma kuhusu bei na tozo, ikiwa ni pamoja na vigezo na masharti ya huduma. Mtumiaji asiporidhishwa na huduma anayopata anatakiwa alalamike – kwanza kwa mtoa huduma wake, na asiporidhika na ufumbuzi awasilishe malalamiko yake TCRA,” imesisitiza.

“Watumiaji wanashauriwa kuchukua fursa ya soko huria la mawasiliano nchini kama nafasi ya kulinganisha huduma na bei za watoa huduma na vifurushi wanavyouza kabla ya kuamua kujiunga na kifurushi chochote au huduma yoyote. Watumiaji wa simu janja zinazowezesha matumizi ya huduma nyingi, maarufu kama “smart phone”, kuwa makini wakati wa kuzitumia. Wahakikishe kwamba wanazima maeneo ambayo yanaweza kutumia data hata kama wakati huo hawatumii vifurushi vya data walivyonunua kwenye vifurushi.”

Katika hatua nyingine taarifa hiyo imetoa takwimu ya kuongezeka kwa matumizi ya simu na internet nchini katika kipindi cha miaka 10.

Imesema hadi sasa kuna laini za simu za mkononi zipatazo 31,862,656 ukilinganisha na laini 2,963,737 mwaka 2005.

“Idadi ya simu za mezani ni 151, ukilinganisha na 154, 420 mwaka 2005. Watumiaji wa intaneti wameongezake hadi kufikia 11,000,000 Desemba 2014 kutoka 3,563,732 mwaka 2008. Kwa sasa, kuna hamu kubwa ya matumizi ya intaneti na mwelekeo huu utaendelea; hasa kutakapokuwa na ongezeko la mitandao inayowezesha kutoa huduma za intaneti; na kuongezeka kwa mitandao ya jamii,” imesema.

“Wateja walionunua laini au ambao wanatumia huduma za simu kwa kuzungumza imeongezeka kwa asilimia 91 kutoka milioni tatu (3,000,000) mwaka 2005 hadi milioni 32 ( 32,000,000) mwaka 2014. Hii imewezesha huduma za simu kufikia asilimia 97 ya Watanzania ilipofika Desemba 2014; kutoka asimilia 10 mwaka 2005. Kwa upande mwingine, muda wa kuzungumza kwa simu, ukiwa umepimwa kwa dakika zinazotumika, umeongezeka sambamba na ongezeko la idadi ya watumiaji. Umefikia dakika bilioni 41 kutioka dakika milioni 506 mwaka 2005,” imeongeza mamlaka hiyo.

“Matumizi kwa upande wa meseji, yaani SMS na data pia yameongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka SMS zipatazo milioni 5 mwaka 2005 hadi SMS bilioni 10 mwaka 2014. Watumiaji wa intaneti wanaotumia simu za mkononi sasa wanafikia milioni 10.”
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Zambia kwa ajili ya mazungumzo rasmi na Mwenyeji wake Rais Edgar Lungu ( mwenye suti ya kijivu aliyesimama mbele ya Rais Kikwete).
Rais Lungu akimkaribisha Rais Kikwete (hayupo pichani kuzungumza)
Mhe. Rais Kikwete akizungumza wakati wa mazungumzo rasmi na Rais Lungu na Ujumbe wake katika Ikulu ya Zambia. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Mebe na kulia ni Waziri wa Fedha, Mhe. Saada Mkuya Salu na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace Mujuma.
Mazungumzo yakiendelea
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania wakati wa mazungumzo rasmi akiwemo Mhe. Charles Tizeba (wa kwanza  kulia), Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Abbas Kandoro (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bi. Zuhura Bundala (wa tatu kushoto), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Bi. Talha Mohammed (wa kwanza kushoto), Afisa Mambo ya Nje.
Picha ya Pamoja
Mhe. Rais Lungu akiwa amefuatana na Mhe. Membe.
---

Tanzania na Zambia zimekubaliana kushirikiana na kuimarisha sekta ya miundombinu hususan kufufua Reli inayounganisha nchi hizi mbili (TAZARA) ili kukuza biashara na uwekezaji.

Makubaliano hayo yamefikiwa jana wakati wa ziara ya siku mbili ya Rais wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete nchini Zambia.

Akizungumza wakati wa mkutano rasmi kati yake na mwenyeji wake, Mhe. Edgar Lungu, Rais wa Zambia, Rais Kikwete alisema kuwa umefika wakati sasa  wa kuifufuA Reli ya TAZARA ambayo ni kiungo muhimu na alama kubwa ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia.

Mhe. Rais Kikwete alifafanua kuwa umuhimu wa reli hiyo ni wa kihistoria ambao unahusisha nchi tatu za Tanzania, Zambia na Jamhuri ya Watu wa China ambao kwa kiasi kikubwa walichangia ujenzi wa reli hiyo.

“Upo umuhimu mkubwa wa kuifufua Reli ya TAZARA ili ifanye kazi kama awali kwani ni alama na kiungo muhimu cha ushirikiano wetu sisi Tanzania na Zambia”, alisema Rais Kikwete.

Aidha, aliongeza kuwa Tanzania na Zambia zimekubaliana kuwekeza zaidi katika reli hiyo ikiwemo kuboresha uendeshaji na ukarabati ili kuirejesha katika hali yake ya awali na hatimaye kukuza biashara na uwekezaji. 

Alifafanua kwamba hapo awali reli hiyo iliweza kusafirisha tani zaidi ya milioni 2 za bidhaa kwa mwaka wakati sasa reli hiyo inasafirisha  tani laki 2 kwa safari inayotumia hadi siku 12 kutoka Dar es Salaam hadi New Kapiri Mposhi wakati malori yanatumia siku tano pekee.

“TAZARA inapita katika kipindi kigumu sasa, hivyo tumezungumza namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili ikiwemo uendeshaji na ukarabati ili irejee katika hali yake ya awali”, alisisitiza Rais Kikwete.

Katika  hatua nyingine Mhe. Rais Kikwete alimpongeza Rais Lungu kwa kuchaguliwa hivi karibuni kuwa Rais wa Zambia na pia alitoa salamu za pole kwa Rais huyo na Wazambia wote kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Hayati Michael Satta.

Kwa upande wake, Rais Lungu alisema kuwa Tanzania na Zambia zinajivunia mafanikio ya ushirikiano yaliyopo baina ya nchi hizi mbili ambayo yamejikita katika sekta za Kilimo, Usafirishaji, Nishati na Mawasiliano.

Pia, alisema kwamba nchi yake ipo tayari kuimarisha ushirikiano wa kihistoria uliopo ambao unaanzia ngazi ya serikali, kanda, Bara  na Kimataifa na kusisitiza umuhimu wa kuitumia Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 1992 kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yanayofikiwa na nchi hizi mbili. Aidha, alikubaliana na hoja ya kuifufua reli ya TAZARA kwa manufaa ya nchi hizi mbili.

Rais Kikwete ambaye alikuwa nchini humo kwa mwaliko wa Rais Lungu alifuatana na Mama Salma Kikwete, Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Saada Mkuya Salum, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Grace Mujuma, Balozi wa Tanzania nchini Zambia na Viongozi Waandamizi kutoka Serikalini na Mamlaka mbalimbali.
Today when I was going to work, my driver asked : Godwin are you from Tanzania?

My answer was YES, then with a BIG SMILE he responded... Tanzaniiiaaaa, ooooh grandfather of Mozambique... Mwl. Nyerere Chama cha Mapinduzi.

Godwin, you know Tanzania is the FIRST DIPLOMAT of Mozambique, the SECOND is Zambia and THIRD Zimbabwe. Tanzania played a big role for our independence.

Kauli hii ilinifanya niendelee kutafakari juu ya alama tunazoziacha kwa namna zinaishi hata kama sisi tukitwaliwa na kupumzika katika nyumba ile ya milele.

Wazee wetu waliacha alama, nasi kila mmoja wetu kwa nafasi yake aweza kuacha alama safi na sio chafu kama za:-

- Wizi
- Madawa ya kulevya
- Mauaji / uuaji wa albino
- Ufisadi
- Kauli chafu

Na mengine mengi yasiyo mema.

Naendelea kujifunza

@ BAGATECH

Godwin D. Msigwa
Maputo, Mozambique.
25th February 2015