Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara ya Mbezi mwisho-Goba- Tangi Bovu.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara ya External –Kilungule.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akiweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa barabara ya Msewe-Baruti
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akipiga tumba huku Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mheshimiwa John Mnyika akicheza kuashiria furaha yao kabla ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Mbezi mwisho-Goba- Tangi Bovu.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli kushoto akiwa na mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Ramadhan Madabida kulia wakifurahia mara baada ya uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Mbezi mwisho-Goba –Tangi bovu.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akisalimiana na wananchi kabla ya uzinduzi wa miradi hiyo ya kupunguza msongamano.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Magufuli akiwashika mikono Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mheshimiwa John Mnyika pamoja na mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee mara baada ya kuzindua mitambo itakayofanya kazi katika ujenzi wa barabara ya Mbezi mwisho-Goba –Tangi bovu.
Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa John Mnyika akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi katika shule ya Msingi Msewe.
Uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Kigogo-Tabata dampo.
Taaswira ya barabara ya Mbezi mwisho-Goba-Tangi bovu eneo la Goba ambalo limeshajengwa kwa kiwango cha lami. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

Waziri wa Ujenzi Mheshimkiwa Dkt.John Pombe Magufuli leo amezindua na kuweka  mawe ya msingi katika Ujenzi wa barabara za pete zitakazopunguza msongamano jijini Dar es salaam.

Barabara hizo zilizowekewa mawe ya msingi ni pamoja na ile ya  Kinyerezi –Kifuru hadi Mbezi Mwisho yenye urefu wa kilometa 14.0, Kigogo-Tabata Dampo yenye urefu wa kilometa 1.6, na Kimara Baruti-Msewe hadi Chuo Kikuu  cha Dar es Salaam yenye urefu wa kilometa 2.6.

Barabara nyingine ni ile ya External –Kilungure hadi Kimara Korogwe kilometa 8.0, Wazo Hill-Goba hadi Mbezi mwisho kilometa 20 na Goba-Tangi bovu kilometa 9.0.

Akizungumza wakati akizindua ujenzi wa barabara hizo Waziri Magufuli amewataka wananchi kufuata sheria za barabarani kwa kutoingilia hifadhi za barabara na wale wenye nyumba pembeni mwa barabara kuzibomoa wenyewe ili kupisha ujenzi huo kwenda kwa wakati.

“Nawahakikishieni kwamba mkifuata sheria za kutojenga karibu na barabara barabara hizi zitajengwa kwa kiwango cha lami na kwa wakati ili kupunguza msongamano wa magari katika barabara kuu na ninyi mtanufaika na fursa za kibiashara kwa kuwa karibu na barabara za lami na hivyo kujikwamua kiuchumi”,amesisitiza Waziri Dkt. Magufuli.

Waziri Magufuli amesema barabara ya Wazo HilL –Goba yenye urefu wa kilometa 20 ikikamilika kwa kiwango cha lami itaziunganisha barabara za Bagamoyo na Morogoro ambazo zimekuwa zikikabiliwa na msongamano kwa muda mrefu.

Aidha, amesema barabara ya Kinyerezi- Kifuru hadi Mbezi mwisho yenye urefu wa kilometa 14 itapunguza pia msongamano kwa kiasi kikubwa kwa kuwa itakuwa inaunganisha barabara ya Morogoro na Nyerere hivyo kuwataka wananchi kuanza kuzitumia barabara hizo ambazo zitakamilika kwa wakati.

Amewataka vijana wanaopata fursa za ajira katika ujenzi wa barabara hizo kuwa waadilifu,waaminifu na wachapa kazi na kujiepusha na vitendo vya wizi vitakavyosababisha kuongeza gharama za ujenzi wa barabara hizo.

“Kumbukeni mkiiba vifaa vya ujenzi hamuibi vifaa vya kampuni zinazojenga bali mnajiibia wenyewe kwa sababu hizi ni fedha za kodi ya wananchi bali kufanya kazi kwa bidii na uadilifu kutawezesha ujenzi wa barabara kukamilika kwa wakati na ninyi kujihakikishia uhakika wa ajira”,alisema Waziri Magufuli.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mheshimiwa Said Meck Sadik amezungumzia umuhimu wa wakazi wa jiji la Dar es salaam kutunza barabara kwa kutofanya biashara kwenye hifadhi za barabara na kuahidi hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale watakaokiuka taratibu za kisheria na kutupa takataka katika mitaro ya barabara.

Amewataka wabunge wa Mkoa wa Dar es salaam na wabunge wengine wanaoishi mkoani  Dar es salaam kutenga fedha za kutosha za ujenzi wa barabara jijini Dar es salaam ili kuhakikisha Wizara ya Ujenzi inamudu kuzijenga barabara za pembezoni zitakazopunguza msongama na kuliwezesha jiji la Dar es salaam kupitika wakati wote.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini  (TANROADS), Eng.Patrick Mfugale ameiomba Serikali kuongeza bajeti ya barabara ili kuwezesha Miradi ya barabara kukamilika kwa wakati na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ili barabara zijengwe kwa kiwango kilichokubalika katika mikataba.

Ziara hiyo ya Uzinduzi wa barabara za pete imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa jiji la Dar es salaam akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Bw.Ramadhani Madabida,Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa John Mnyika,Segerea-Dkt Makongoro Mahanga,na Kawe mheshimiwa Halima Mdee ambapo kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana ili Wizara ya Ujenzi ipate fedha za kukamilisha miradi hiyo itakayopunguza kwa kiasi kikubwa kero ya msongamano jijini Dar es salaam.

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ujenzi.
 Mkurugenzi wa Mikoa na Utawala wa NHC Bw. Raymond Mndolwa(aliyenyosha mkono juu) akiekeza jambo wakati alipokuwa kwenye ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC kwenye mradi wa nyumba za Makazi Wilayani Monduli jana.
 Mkugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akikagua nyumba za makazi za kuuza  zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akipewa maelezo ya mradi wa nyumba za kuuza za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli na Msimamizi wa mradi huo Bw. Hassan Bendera.
 Hii ni sehemu ya nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli kama sehemu ya juhudi za Shirika hilo za kuwezesha wananchi wengi kumiliki nyumba. Nyumba hizi zinajengwa na NHC katika maeneo mbalimbali nchini.
 Msimamizi wa mradi wa nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli Bw. Hassan Bendera (mwenye koti jekundu kushoto) akitoa maelezo  kwa ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa NHC yanayohusu  hatua za utekelezaji wa mradi wa nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akikagua mchoro wa ujenzi wa nyumba za makazi zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Twalib Mbasha na kuhimiza Halmashauri hiyo kukamilisha ulipiaji wa nyumba hizo ili Shirika liongeze kasi ya kukamilisha mradi huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Twalib Mbasha na kuhimiza Halmashauri hiyo kukamilisha ulipiaji wa nyumba hizo ili Shirika liongeze kasi ya kukamilisha mradi huo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli (katikati), Twalib Mbasha akiuonyesha ujumbe wa NHC eneo lililotengwa kwa ajili ya kujenga nyumba ambalo alisema lina miundombinu yote muhimu ikiwemo umeme na maji.
unnamed1jk 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wan Kijeshi mjini Riyadh, Saudi Arabia,  asubuhi ya Jumapili, Januari 25, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi. unnamedjk 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mjini Riyadh, Saudi Arabia,asubuhi ya leo, Jumapili, Januari 25, 2015, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita. PICHA NA IKULU

Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.

Mjini Berlin, Ujerumani ambako Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili kesho, Jumatatu, Januari Ishirini na Sita, akitokea Riyadh, Saudi Arabia, anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) ambako viongozi mbali mbali duniani watajadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.

Baada ya kumaliza ziara yake Ujerumani, Rais Kikwete atakwenda Ufaransa ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ufaransa. Aidha, Rais Kikwete atafungua jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania katika Ufaransa na pia nyumba ya balozi.

Rais Kikwete baada ya kumaliza ziara zake za kikazi katika Ujerumani na Ufaransa atakwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu – Dar es Salaam. 25 Januari, 2015
Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) (Kulia) ambaye awali alikuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) akifafanua jamabo kuhusu masuala ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Waziri wa Nchi aliyeteuliwa kushika wadhifa huo Mhe. Jenesta Mhagama (Mb) (kushoto ) wakati wa kumkabidhi ofisi, leo, Jijini Dar e es Salaam.
Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) (mwenye shati) ambaye awali alikuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) akiwaeleza wakurugenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani) kuendelea kutoa ushirikiano wa kutekeleza majukumu ya ofisi hiyo, kwa Waziri mpya wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenesta Mhagama (Mb) (katikati) wakati wa kumkabidhi ofisi, leo, Jijini Dar e es Salaam (anayeandika) ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Regina Kikuli .
Baadhi ya Wakurugenzi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza aliyekuwa Waziri wa Nnchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. William Lukuvi (Mb) ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi ambaye wakati wa kumkabidhi Ofisi aliyeshisha wadhifa huo wa Waziri Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenesta Mhagama (Mb) wakati wa kumkabidhi ofisi, leo, Jijini Dar e es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Regina Kikuli akimhakikishia ushirikiano Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Mhe. Jenesta Mhagama (Mb) (kushoto ), wakati wa kumkabidhi ofisi, leo, Jijini Dar e es Salaam, (kulia ) ni Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) (Kulia) ambaye awali alikuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angellah Kairuki (kulia) akimkabidhi nyaraka mbalimbali Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Ummy Mwalimu wakati akimkabidhi ofisi leo jijini Dar Es Salaam . kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri lililofanyika Jumamosi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angellah Kairuki akimkabidhi nyaraka mbalimbali Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Maimuna Tarishi wakati Mhe. Kairuki alipokuwa akikabidhi ofisi leo jijini Dar Es Salaam.
IKU
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mawaziri na manaibu waziri aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam jioni hii.Wanne kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue.
IKU1

Moja wa Sura mpya katika baraza jipya la Mawaziri Naibu Waziri wa Elimu Anne Kilanngo Malecela akila kiapo Mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo, (PICHA NA FREDDY MARO)
11
Mfanyabiashara na mmiliki wa duka la dawa katika eneo la Mrombo Arusha Bi elizabeth mshana akiongea na Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde juu ya huduma ya kufanya malipo kwa kutumia kadi ya Airtel Money Near Field Communication (NFC) based solution ya  Airtel Money. kadi hii maalum inamuwezesha mteja kufanya malipo kwa haraka kwa kugusisha kwenye kifaa maalum tu mara moja, kisha kuweka nambari ya siri na kufanya malipo mahali popote. kwa sasa huduma hii imeanza kufanya kazi mkoani Arusha. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) yaani kulipa kwa kugusisha kadi na kifaa tu kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel.
1111
Mama elizabeth mshana mmiliki wa duka la dawa akimuuzia mteja dawa kwa kupitia kadi huduma iliyozinduliwa na Airtel mkoani Arusha inayowawezesha wateja wake kufanya malipo kwa haraka zaidi kwa kutumia kadi hiyo maalumu ya airtel Money yenye teknolojia ya Near Field Communication (NFC) based ikiwa imeunganishwa na  Airtel Money. Akishuhudia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni yasimu za mkoni ya airtel.
11111
Afisa uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya AIRTEL Jane Matinde akimuelekeza Moja ya wateja bi Merry Ngowi jinsi ya kutumia kifaa na kadi maalumu ambacho hutumika kukamilisha miamala ya malipo katika maduka mbalimbali. Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel, tukio lifanyika mwishoni mwa wiki mkoani arusha eneo la muromboo wakati wa uzinduzi huduma hiyo ambayo inaleta njia salama, ya haraka na rahisi kwa wateja kufanya malipo. 
111
Mfanyabiashara wa duka la chakula  katika eneo la Mrombo Arusha Bwana Elibariki Ngowi akipokea malipo kutoka kwa mteja kwa kupitia kadi maalum ya Near Field Communication (NFC) ya Airtel Money, huduma mezinduliwa na Airtel mkoani Arusha inawawezesha wateja wake kufanya malipo kwa kutumia kadi hiyo maalumu kwa haraka bila huanza kupiga *150*60# hii unagusisha tu na kulipa haraka kati kanti ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akishudia huduma hiyo inavyofanya kazi.  Huduma hii ya Near Field Communication (NFC) kupitia huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ni yakwanza kuzindulia nchini na kampuni ya simu za mkoni ya airtel.
Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum  (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akikagua gwaride rasmi kabla ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish 
 
Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akila kiapo cha kuwa Rais Mpya wa Zambia  katika sherehe za zilizofanyika  jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia. Guy Scott, of Scottish
 Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit)iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akitia saini Hati Maalum Muda mfupi baada ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka - Zambia.
 
 Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akipokea salaam Maalum Kutoka kwa Rais wa Mpito wa Zambia Guy Scotts Muda mfupi baada ya   kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka - Zambia.
 Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi  akiwa na Mkewe Eshter Lungu  Muda mfupi baada ya   kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka - Zambia.
---
Na Mwandishi Wetu

Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ameendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia kipaji chake cha ubunifu wa mavazi baada ya kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka - Zambia.

Rais Lungu 58, aling’arisha sherehe hizo baada ya kuvaa suti rasmi (Presidential suit) rangi ya bluu, shati jeupe na tai nyekundu zilizobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi. Lungu aliambatana na mke wake, Eshter Lungu walipokuwa wanaingia viwanjani hapo huku wakisindikizwa na ulinzi mkali.
Akizungumza baada ya hafla hiyo, Sheria Ngowi alisema amefurahi kupata nafasi ya kipekee ya kumvalisha Rais Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake na kusema ni hatua kubwa katika kazi yake kama mbunifu wa mavazi wa kimataifa.

“Hii ni hatua kubwa katika kazi yangu ya ubunifu wa mavazi, namshukuru Mungu kwa kipaji alichonipa kinachoweza kunitambulisha na kunifanya niaminike hata kufikia hatua ya kuvuka mipaka ya Tanzania na kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Mheshimiwa Edgar Lungu”, alisema Ngowi. 

Mbunifu Ngowi alisisitiza kuwa juhudi, nidhamu, bidii na kumweka Mungu mbele ndio chachu ya mafanikio katika kila utendaji wa kazi zake akiwa na malengo ya kuipeleka kazi yake katika nyanja za kimataifa hata kutambulika katika sekta ya ubunifu wa mavazi duniani kote. 

Hafla hiyo ilihudhuriwa na aliyekuwa Rais wa muda wa Zambia, Guy Scott na mke wake Charlotte, Mwenyekiti wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini(SADC), Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, baadhi ya viongozi wa juu wa Zambaia na nchi mbalimbali pamoja na wananchi wake. 

Mbunifu huyo ameendelea kuonyesha na kudhihirisha kuwa Tanzania ni nchi yenye vipaji vinavyoweza kuiletea nchi ya Tanzania sifa na kuinua uchumi wake katika sekta mbalimbali. Hii si mara ya kwanza kwa mbunifu huyo kukata mawingu kuitangaza nchi yetu, kwani ni miongoni mwa wabunifu mashuhuri kutoka Afrika wanaopata fursa kuonyesha ubunifu wa mavazi yao katika maonyesho ya kimataifa kama vile New York Fashion Week nchini Marekani na Mercedes Benz fashion Week nchini Afrika Kusini.

Hii ni changamoto pia kwa wabunifu wa Tanzania kuziwania fursa zilizopo na pia kuongeza juhudi ili kutangaza na kupeleka kazi zao katika soko la kimataifa kama vile Sheria Ngowi alivyofungua mlango.
 Vanessa Mdee akitoa burudani kwenye tamasha kubwa la kihistoria la Tigo Music Kiboko yao lililofanyika viwanja vya leaders jana.
 Msanii JUX akitoa burudani kwenye tamasha kubwa la kihistoria la Tigo Music Kiboko yao lililofanyika viwanja vya leaders jana.
 Msanii Stamina akitoa burudani kwenye tamasha kubwa la kihistoria la Tigo Music Kiboko yao lililofanyika viwanja vya leaders jana.

Msanii mkongwe wa muziki wa HIP HOP nchini Prof. Jay akitoa burudani kwenye tamasha kubwa la kihistoria la Tigo Music Kiboko yao lililofanyika viwanja vya leaders jana.
---
Na Mwandishi Wetu.

Tigo Tanzania leo imetangaza rasmi uzinduzi wa Muziki wa Tigo ujulikanao kama “Tigo Music” kwa kushirikiana na Deezer, ambayo ni huduma ya kimataifa inayorusha muziki itakayowapa Watanzania muziki usiokuwa na kikomo.

Hafla ya uzinduzi kwa ajili ya Tigo Music imefanyika katika viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam Tarehe 24 Januari ambapo wananchi wametumbuizwa na nyimbo tofauti tofauti kutoka kwa wasaniii 18 wa hapa nchini kama Diamond Platinum, Ali Kiba, Professor J, Weusi, Msondo, Ben Paul, Shillole Linah, Christian Bella, AY hao ni kati ya 18.

Kuanzia Januari 24, wateja wa Tigo wenye vifurushi vya malipo ya kabla ya intaneti wana uwezo wa kupata nyimbo milioni 36 za wasanii wa Kitanzania na Afrika kwa ujumla katika simu zao za mkononi za smartphone. Vilevile, Tigo itatafuta miziki mipya ya kusisimua ya wasanii wa ndani kupitia ushirikiano mpya na kampuni ya Africa Music Rights, ambayo inawezesha, kutafuta na kusimamia haki za muziki katika bara la Afrika,

Meneja Mkuu wa Tigo Bi, Cecile Tiano alisema, ‘Tuna furaha kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiliano Tanzania kuwapa wateja wetu muziki usiokuwa na kikomo”. Muziki unajukumu kubwa katika Tanzania yetu tajiri na tamaduni tofauti kama starehe katika matukio ya kijamii na hata wakati binafsi. Haya ni mafanikio makubwa kwetu tukitarajia watu zaidi na zaidi kutumia smartphones katika sehemu hii ya dunia’.

“Kama bidhaa yenye maisha ya kidijitali, lengo letu ni kuiwezesha tasnia ya muziki kwa kujenga jukwaa ambalo si tu linaruhusu kupata nyimbo za wasanii wa ndani kwa urahisi, lakini pia linawapa mafunzo wanamuziki wetu kwenye masuala muhimu kama vile haki miliki na masoko. Hii ni njia yetu ya kusaidia vipaji vya wasanii na kukuza tasnia ya muziki wa ndani, “aliongeza.

Kuanzishwa kwa Muziki wa Tigo (Tigo Music) nchini Tanzania kumetokana na mafanikio ya uzinduzi nchini Amerika ya Kusini mwaka 2012 pamoja na Ghana mwaka 2014, na. Tangu kuanzishwa kwake imekuwa ni sehemu muhimu kwa maisha ya kidijitali ya watu ya kila siku na hii inaendana na matukio ya muziki wa ana kwa ana yaliyowahi kufanywa na wanamuziki mashuhuri duniani, pamoja na yale yaliyorekodiwa ndani ya studio.
Sehemu ya wanafunzi, wazazi, mwalimu na viongozi wa jumuiya waliohudhuria siku ya kwanza ya darasa la Kiswahili DMV
Awamu ya pili ya Darasa la Kiswahili kwa watoto waishio Washington DC na vitongoji vyake umeanza Jumamosi ya Januari 24, 2015.
Rais wa Jumuiya Bw Iddi Sandaly alipata fursa ya kuzungumza nasi kwa ufupi kuhusu darasa hilo.

Karibu umsikilize

Sehemu ya wanafunzi wakimsikiliza Mwalimu Asha Nyang'anyi. Kushoto kwake ni Katibu wa Jumuiya ya waTanzania hapa DMV Said Mwamende
Baadhi ya wazazi wakiwa nje ya darasa wakati watoto wakiendelea na mafunzo
Baadhi ya wazazi waliokuwa ndani ya darasa wakati watoto wakiendelea na mafunzo