Taswira mbalimbali za Jiji la Lima nchini Peru, hapa ni katika mzunguko wa magari Round About kuingia Ukumbi wa Jeshi la nchi hiyo wenye jina hilo pichani.
 Kwa upande wa mandhari kiukweli wanajitahidi kwa usafi na mazingira yanayovutia...
 Katika Garden mbalimbali zilizopo jijini humo, utakuta maandishi yaliyoandikwa kwa lugha yao kama hivi......
 Hii ni njia ya Mabasi yaendayo kasi kama ambayo inaandaliwa hapa kwetu jijini Dar. Picha zote na Sufian Mafoto.
 Mwanamuziki nguri wa muziki wa dansi nchini, John Kitime ameibukia katika filamu na karibuni amezindua sinema iitwayo ‘Kutakapokucha’ ambayo ina akisi watendaji wasio waadilifu wanavyozitumia vibaya ofisi za umma na kuchangia migongano katika jamii.

Katika filamu hiyo ambayo Kitime anacheza kama muigizaji mkuu, akitumia jina la Nongwa, ndiye mwanakijiji pekee ambaye nyumbani kwake kuna umemejua akijivunia televisheni wanayokuja kuiangalia na baadhi ya wakazi wenzake kijiji na huduma za kuchaji simu anazozitoa nyumbani kwake.

Kwa kutumia ofisi yake, anapora ardhi za watu na mbaya zaidi anawachukia wenye mwamko kidogo wa elimu ambao binafsi anaona hawana lolote zaidi ya kuhitaji kiti chake hali ambayo inazua migongano na migogoro mikubwa ambayo mwisho wake ndio kinachoifanya hiyo filamu kuwa na msisimko wa namna yake.

Filamu hiyo ambayo imeandikwa na Irene Sanga chini ya utayarishaji wa Sylone Malalo na kuongozwa na Simon Mwakifwamba, msambazaji mkuu ikiwa kampuni ya Proin Promotion, licha ya pia ina muigizaji mahiri nchini, Charles Magari ‘Mzee Magari’.

Mtayarishaji wa filamu hiyo, Malalo anasema movie hiyo inatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya filamu nchini na anawataka wale ambao wanapenda vitu tofauti kuangalia pia inashirikisha wasanii wa Sanaa za mapigano ‘martial arts’.

Magari ambaye anaigiza kama mtu ambaye anataka mabadiliko kijijini hapo na kuondokana na urasimu na ukiritimba wa Mzee Nongwa, ina waigizaji mahiri ambao pia ni walimu wa Sanaa katika Taasisi ya Sanaa (Tasuba) ambao ni na Thabit Hudu na Mwanaidi Zambo.

Filamu hiyo ni kazi ya kwanza pia ya mzalishaji Malalo ambaye amebobea katika utengenezaji wa picha za video, documentary na filamu mbalimbali za kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusiana na mambo mbalimbali ikiwa ni katika jamii na baadhi ya filamu hizo ni pamoja na ‘Zawadi’ na zingine.
Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Fastjet Bi. Jean Uku akiongea na Bw. Navin Kanabar (kushoto) na Bw. Manish Rughani (katikati) ambao ni wateja wa fastjet waliopata tiketi za punguzo la bei kwenda Entebe Uganda kuhudhuria tamasha la 33 la michezo na Utamaduni lijulikanalo kama Lohana Festival, kampuni ya Fastjet ilitoa punguzo la bei kwa kundi la wateja 150 walionunua tiketi nyingi.
Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Fastjet Bi. Jean Uku akimkabidhi Bi. Nishita Davda tiketi ya kwenda kuhudhuria tamasha la 33 la michezo na Utamaduni lijulikanalo kama Lohana Festival, kampuni ya Fastjet ilitoa punguzo la bei kwa kundi la wateja 150 walionunua nyingi.
Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Fastjet Bi. Jean Uku (mwenye miwani) na Afisa wa Mawasiliano na Masoko Bi. Lucy Mbogoro (kushoto) wakipozi kwenye picha ya pamoja na wateja waliopata tiketi zenye punguzo la bei kwenda kuhudhuria tamasha la 33 la michezo na Utamaduni lijulikanalo kama Lohana Festival, kampuni ya Fastjet ilitoa punguzo la bei kwa kundi la wateja 150 walionunua nyingi.
Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Fastjet Bi. Jean Uku akimkabidhi Bw. Manish Rughani tiketi ya kwenda kuhudhuria tamasha la 33 la michezo na Utamaduni lijulikanalo kama Lohana Festival, kampuni ya Fastjet ilitoa punguzo la bei kwa kundi la wateja 150 walionunua nyingi.

 Sehemu ya Waandishi wa Habari waliofika kwenye Mkutano huo ulioitishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi,Profesa Anna Tibaijuka akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Hyatt Regency,Jijini Dar es salaam leo.
Na Mwandishi Wetu.

Jumla ya vijiji ni 9047 CCM imepata 7290 na Chadema 1248 Cuf 949 mitaa CCM Tanzania ipo 3740 CCM imepata 2116 Chadema 753 Cuf 235 hivyo CCM kwenye vijiji imeshinda kwa asilimia 80.58 Chadema 13.79 mitaa CCM asilimia 67.90 na Chadema 25.63 

Leo mkurugenzi wa uchaguzi tawala za mitaa na serikali za mitaa (tamisemi) Khalist Luanda ametangaza matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa huku chama cha mapinduzi kikipata ushindi katika vjiji 7290 na chadema 1248 kati ya vijiji 9047.

Akitangaza natokeo hayo mkoani Dodoma Luanda alisema katika katika mitaa ccm imepata 2116 na Chadema ikipata 753 Cuf 753 kati ya mitaa 3078.

Aliitaja mikoa ambayo imefanya zoezi hilo bila ya kuwa na vurugu huku akiipongeza kuwa ni dodoma njombe singida katavi pwani mbeya kagera ruvuma arusha mtwara Lindi.

Alisema mikoa ambayo ilikuwa. Na dosari katika zoezi hilo kuwa ni kigoma katika eneo la kasulu tabora. Eneo la kaliua na pwani katika eneo la Mkuranga.

Alisema kwa wale wanaorudia. Uchaguzi hawatakiwa kufanya kampeni kwani wakati wa kampeni uliishapita huku akisema siku ya kufanya uchaguzi ni jumamosi.

"Jumaomosi. Ya wiki hii ndio kwa wale ambao hawajafanya uchaguzi ndio watafanya niwaombe wawe watulivu katika kipindi hichi naamini zoezi letu limeenda vizuri" alisema Luanda.
Mastaa waliokuwa wakiunda kundi la zamani la Kaole wakiongea na wanahabari (hawapo pichani) jinsi walivyopania kufanya kweli kwenye uzinduzi wa kundi lao jipya la Kaone, Boxing Day ndani ya Dar Live.
Muhogo Mchungu akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani). Kushoto ni msanii Thea. 
Wasanii hao wakongwe wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo na wanahabari. Mkutano huo umefanyika leo katika Hoteli ya The Atriums iliyopo Afrikasana, Dar.
Msanii Thea (kulia) akielezea jambo kwa wanahabari (hawapo pichani).
Msanii Kingwendu akitoa burudani wakati akiongea na mwanahabari wa TBC.

ZIKIWA zimesalia siku chache kuelekea ule Usiku wa Wasanii Wakongwe Desemba 26 ‘Boxing Day’ ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar, mastaa kibao waliokuwa wakiunda kundi la zamani la Kaole watazindua rasmi kundi jipya linalojulikana kama Kaone.

Usiku huo utakaokuwa wa aina yake, utawakutanisha wale wakali wote kutoka Kaole kama vile Swebe, Davina, Koletha, Zawadi, Nyamayao, Kingwendu, Muhogo Mchungu, Kibakuli na wengine kibao ambao kwa mara ya kwanza watajulikana kama Kaone na kuzindua tamthiliya yao mpya ya Kipusa itakayoanza kuruka hewani Januari 4, 2015 ndani ya Runinga ya TV1.

Usiku huo pia utapambwa na wasanii wa Bongo Fleva, Baby Madaha pamoja na Isabela Mpanda ‘Bela’ ambapo watatoa burudani mwanzo mwisho.

Mapema kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na burudani kwa watoto ambapo Kundi la Masai Worriors litawapagawisha watoto kwa kuwapa chemsha bongo, mazingaombwe sambamba na kutoa zawadi kibao huku watoto wengine wakipata nafasi ya kubembea, kuteleza na kuogelea.

Promota wa mpambano wa masumbwi nchini Shabani Adios 'Mwaya mwanya' katikati akiwangalia mabondia Ibrahimu Maokola na Selemani Mkalakala wanavyotunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa unaotambuliwa na chama cha TPBC utakaofanyika leo ijumaa katika ukumbi wa Vigae.

Mabondia Ibrahimu Maokola na Selemani Mkalakala wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa ubingwa wa taifa unaotambuliwa na chama cha TPBC utakaofanyika ijumaa katika ukumbi wa Vigae classic Mbagala Zakhem
Bondia Ibrahimu Maokola akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa wa taifa na Selemani Mkalakala kushoto kulia ni Rais wa TPBC Chaurembo Palasa mpambano utakaofanyika ijumaa ya Desemba 19 katika ukumbi wa Vigae classic Mbagala Zakhem.


Saleh Mkalekwa akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Abdalaaha Mohamedi mpambano utakaofanyika ijumaa ya Desemba 19 katika ukumbi wa Vigae classic Mbagala Zakhem.
Dr Hesea Ronard akimpima afya bondia Ibrahimu Maokola kwa ajili ya mpambano wake wa kesho Ijumaa
Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kadi mpya ya B PESA ya banki ya I&M,Kamada wa Polisi Kanda Dar es Salaam,CP Suileman Kova (wa pili kushoto) akiwa pamoja na viongozi wa Banki ya I&M wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi wa kadi hiyo,uliofanyika kwenye ukumbi wa Marquee ndani ya Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.toka kulia ni Mkurugenzi mkuu wa I&M Bank, Anurag Dureha,Kaimu Mkurugenzi wa banki ya I&M, Shameer Patel, Mkurugenzi wa banki ya I&M (Arusha), Michael Shirima pamoja na Afisa Masoko wa banki ya I&M, Salilabbas Sadak (wa kwanza kushoto).
 Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kadi mpya ya B PESA ya banki ya I&M, Kamada wa Polisi Kanda Dar es Salaam,CP Suileman Kova(wa pili  kushoto) akishirikiana na baadhi ya viongozi wa banki ya I&M kukata keki yenye umbo kama kadi mpya ya B PESA. 
Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kadi mpya ya B PESA ya banki ya I&M,Kamada wa Polisi Kanda Dar es Salaam,CP Suileman Kova akizungumza jambo kwenye uzinduzi wa kadi mpya ya B PESA ya banki ya I&M uliofanyika kwenye ukumbi wa Serena hotel jana.
 Mkurugenzi mkuu wa I&M Bank, Anurag Dureha akitoa hotuba yake kwenye uzinduzi wa kadi mpya ya B PESA itakayotumika kufanyia manunuzi mbalimbali na hata kuhamisha pesa kirahisi. 
Kaimu Mkurugenzi wa banki ya I&M, Shameer Patel akizungumza jambo kwenye uzinduzi huo
 Mkurugenzi wa I&M Bank tawi la Arusha,Bw. Michael Shirima akitoa pongezi pamoja na kuwasisitiza watu wajiunge na bank hiyo pamoja na kuwa na kadi ya B PESA kwa ajili ya kupata huduma kwa urahisi bila tatizo lolote.
Afisa Masoko wa banki ya I&M, Salilabbas Sadak akizungumzia changamoto wanazozipata pamoja na faida ya banki ya I&M kwenye uzinduzi wa kadi mpya ya B PESA
Mkurugenzi wa I&M Bank tawi la Arusha, Bw. Michael Shirima (wa pili kutoka kushoto) akizungumza jambo na Afisa Masoko wa banki ya I&M, Salilabbas Sadak kwenye uzinduzi wa kadi mpya ya B Pesa, uliofanyika kwenye hotel ya Serena jijini Dar es  Salaam
Picha ya pamoja
Mkurugenzi wa I&M Bank tawi la Arusha, Bw. Michael Shirima (kushoto) akibadilishana mawazo na Kamada wa Polisi Kanda Dar es Salaam, CP Suileman Kova (katikati) pamoja na Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Tanzania,SACP Simon Siro kwenye uzinduzi wa kadi mpya ya B PESA kutoka benki ya I&M
 Kikundi cha kuigiza kutoka THT kikitoa burudani kwenye uzinduzi wa kadi mpya ya B PESA 
Burudani ikiendelea 
ALIYEKUWA mnenguaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi nchini Aisha Mohammed Mbegu maarufu kama Aisha Madinda amefariki dunia leo nyumbani kwao Kigamboni Jijini Dar es Salaam. 

Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta Luizer Mbutu amethibitisha kuwa Aisha amefariki dunia na alifia nyumbani kwao sababu ambazo bado hazijafahamika.

Akizungumza kwa masikitiko Mbutu alisema kwamba mwili wa merehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

“Hapa nilipo natetemeka kwa msiba huu sababu marehemu alikuwa mzima na leo ndiyo ilikuwa aanze mazoezi na bendi ya Twanga Pepeta kwa ajili ya maandalizi ya onyesho la maadhimisho ya miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta” alisema Luizer.

Aliongeza kwa kusema: "Hapa natetemeka siamini lakini mwili nimeuona ni kweli Aisha amefariki na amefikishwa hapa hospitalini akiwa tayari amefariki.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka pia amethibitisha habari hizo na hivi sasa yuko njiani kurejea Dar es salaam kwa ndege akitokea Kigoma ambako alikwenda kwa shughuli za uchaguzi wa serikali za mitaa.

Msiba uko Kigamboni maeneo ya Mikadi Beach.
KOCHA wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo amewaaga rasmi leo asubuhi wachezaji wa timu hiyo kwenye mazoezi uwanja wa Sekondari ya Loyola huku akitarajia kuvuna zaidi ya Milioni 20 ndani ya klabu hiyo ikiwa ni mshahara wake wa dola 1200 na yupo kwenye harakati za kudai fidia ya kuvunjiwa mkataba na kuletwa mrithi wake kabla uongozi wa klabu hiyo haujamaliza nae.

Hata hivyo, tayari Maximo ameaga wachezaji wake kwenye mazoezi ya asubuhi leo ambapo mazoezi hayo yaligeuka shubiri baada ya Maximo  kuwakusanya wachezaji wake na kuwambia kuwa kuanzia leo  sio kocha wa timu hiyo tena na kuwatakia maisha mema ndani ya klabu hiyo ya Jangwani.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wachezaji wa klabu hiyo ambao pia hawajaridhishwa na uamuzi wa uongozi wa klabu hiyo kumuacha mshambuliaji Hamis Kiiza na kumsajili Amis Tambwe.

Mmoja wa wachezaji hao alisema  "Ni kweli kocha ametuaga asubuhi daa! ndio hivyo tumesikitika lakini hatuna jinsi."

Naye mchezaji mwingine ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema "Inaumiza sana jana (juzi) tumefanya nae mazoezi vizuri kabisa tena amechangamka kama kawaida kumbe nyuma kuna mambo yanaendelea, leo asubuhi tumeenda mazoezi kama kawaida tukijua tunafanya mazoezi matokeo yake anasema acheni kila kitu kaeni hapo nataka kuzungumza na nyinyi.

"Uwezi kuamini kidogo machozi yanitoke pale aliposema kuanzia leo yeye sio kocha wetu tena, dah inaumiza sana, mtu ambaye mmemzoea mnafanya nae kazi kuondoka, ndo hivyo wakubwa wemeshaamua bwana wenye timu yao.

Wakati huyo akisema hayo, mchezaji nguli wa timu hiyo yeye alisema "Hakuna mchezaji kwa kweli aliyependezwa na kitendo cha uongozi, yani kwenye mazoezi asubuhi ilikuwa kama msiba, 'mood' ya kufanya mazoezi iilisha kabisa, yani hakuna aliyekuwa na hamu ya kuendelea na mazoezi.

"Tumefanya kidogo mazoezi tukaondoka, ukiangalia ni sawa tumefungwa cha muhimu ilikuwa ni kukaa chini na kuzungumza na kuangalia cha kufanya, kama kuna mapungufu basi yafanyiwe kazi, mimi sijaona haja ya kumfukuza kocha hasa kipindi kama hichi."

Meneja wa timu hiyo Hafidhi Saleh alikiri Maximo kuaga wachezaji kabla ya mazoezi ya timu hiyo kuanza akiwapa moyo wajitume kwa kuwa ni wachezaji wazuri na timu ni nzuri na kuwataka kuongeza bidii ili wafike mbali.

"Kwa kweli inasikitisha hakuna mchezaji wala mtu aliyefurahia, kama yupo labda kimoyomoyo ila dah imetuumiza, ni mazoea cha muhimu tugange yajayo hayo mengine tuwaachie viongozi."alisema Saleh

Saleh alisema kuwa tayari kocha Hans van Der Pluijm ambaye amefikia kwenye hoteli ya Tansoma jana alikuwa kwenye mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo ili aichukue nafasi ya mbrazil Marcio Maximo ambaye amekumbwa na kipunga cha kutimuliwa baada ya kunyukwa mabao 2-0 katika mechi ya mtani Jembe, akiwa ni kocha wa pili kutimuliwa Yanga baada ya matokeo ya mtani jembe mwaka jana alitimuliwa Ernie Brandts baada ya kunyukwa mabao 3-1 na nafasi yake kuchukuliwa na Pluijim ambaye nae hakukaa sana akaikacha timu hiyo baada ya kupata kibara nchini Saudi Arabia.

Wakati huo huo, uongozi wa Yanga umegwaya mchezaji Andry Countinouh kuvunja mkataba wake baada ya kuwa wangelazimika kuvunja kibubu cha Sh185 milioni ili kumlipa fidia ya mshahara wake ambao ni dola 2800 kwa mwezi.

Katika hatua nyingine, pamoja na Yanga kumfungashia virago Emerson De Oliveira Neves Roque imemuombea kibali cha usajili wa kimataifa (ITC) kutoka Bonsucesso Brasil kwenda Yanga.

Mkurugenzi wa mashindano ya TFF, Boniface Wambura alisema kuwa TFF haina taarifa za Yanga kumuacha mbrazili huyo.
Mfalme wa Muziki wa Taarab nchini, Mzee Yusuf (wa pili kushoto) akielezea kwa wanahabari (hawapo pichani) alivyojipanga kuanguasha shoo ya nguvu katika Tamasha la Wafalme Sikukuu ya Xmas Dar Live. 
Meneja wa Mashauzi Classic, Ismail Rashid 'Suma Ragar' akiongea na wanahabari (hawapo pichani) jinsi walivyojipanga kutoa burudani katika msimu wa Xmas Dar Live wakati wa mkutano na wanahabari hao uliofanyika leo kwenye Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza-Afrikasana jijini Dar . Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo, Benjamin Mwanambuu, Mkurugenzi Bendi ya Extra Bongo, Ali Choki (wa pili kushoto), Mzee Yusuf (wa pili kulia) na Damian Raphael 'MC Dalada Kikombe' kutoka Kundi la Masai Worriors (wa kw nza kulia).
Damian Raphael 'MC Dalada Kikombe' kutoka Kundi la Masai Worriors (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu makamuzi watakayoyafanya Dar Live katika msimu huu wa sikukuu.

KAMPUNI ya Dar Live kwa mara nyingine imetoa ratiba kamili ya burudani katika msimu huu wa kufungia mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015.

Usiku wa Wafalme

Kwa mara nyingine shoo bab’kubwa ambayo ni habari ya mjini kwa sasa ijulikanayo kama Usiku wa Wafalme itagongwa ndani ya ukumbi huo pekee kwa burudani, Desemba 25 ‘Sikukuu ya Krismasi’ ambapo mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ atagonga nyimbo zake zote kali siku hiyo.


Diamond ambaye ni mshindi wa tuzo tatu kutoka Channel O zijulikanazo kama Channel O Africa Music Video Awards (CHOAMVA), siku hiyo atatinga na tuzo zake zote hizo ikiwa ni kuwapa shukrani mashabiki wake wote kwa sapoti waliyoitoa huku akipiga nao picha kwenye ‘red carpet’ na kuongea nao mawili-matatu.

Mashabiki pia watapata nafasi ya kumshuhudia Diamond kwa mara ya kwanza akipiga nyimbo zaidi ya 20 jukwaani pasipo kusimama huku akiwatambulisha madensa wapya sambamba na kupiga pia na nyimbo zake zote ambazo zilishawahi kuachiwa na hazijawahi kuisha mpaka mwisho.

Kwa upande wa muziki wa Pwani, usiku huo utafunikwa pia na Mfalme Mzee Yusuf ambaye siku hiyo ataungana na kundi lake la Jahazi Modern Taarab katika kuwaonjesha mashabiki ngoma zao zote zilizopo katika albamu yao mpya ya Chozi la Mama huku wakifunga mwaka na ngoma ambayo ni habari nyingine kwa sasa ya Mahaba Niue.

Mashabiki watakaofika usiku huo pia watapata bahati ya kushuhudia mshindi wa shindano la kumtafuta mwanaume mwenye mvuto kutoka Gazeti la Ijumaa lijulikanalo kama Ijumaa Sexiest Bachelor ambapo mpaka sasa wamebaki washiriki watatu, Yusuph Mlela, Diamond Platnumz pamoja na Ali Kiba.

Mapema kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na burudani kwa watoto ambapo watoto wote watakaofika watapata bahati ya kucheza michezo kibao kama vile kubembea, kuteleza, kuogelea na mingine mingi huku kundi la sarakasi la Masai Worriors likiwapagawisha kwa kutoa michezo kibao ya sarakasi , mazingaombwe sambamba na kumwaga zawadi kwa kila mtoto.
Mkurugenzi wa Huduma za Kutuma na Kupokea Fedha wa Tigo Andrew Hodgson (wa pili kulia) akipongezana na Mkurugenzi wa Huduma za Kutuma na Kupokea Fedha wa ZANTEL Hashim Mukudi mara baada ya kutangaza ushirikiano kati ya huduma zao za TigoPesa na EzyPesa mapema leo Zanzibar. Kutoka kushoto ni Meneja wa Biashara wa ZANTEL Zanzibar Mohamed Mussa, Meneja Miradi wa ZANTEL Shinuna Kassim na Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga (kulia).
Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mjini Zanzibar mapema leo kuhusu ushirikiano kati ya TigoPesa na EzyPesa ambapo sasa wateja kutoka mitandao hiyo miwili wataweza kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao hiyo moja kwa moja kutoka kwa wakala wa mtandao wao bila kuwa na ulazima tena wa mteja kutafuta wakala wa mtandao wa mtu aliyemtumia pesa.
Mkurugenzi wa Huduma za Kutuma na Kupokea Fedha wa Tigo Andrew Hodgson akitoa maelezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo Zanzibar ya namna ya kutumiana fedha kati ya mteja wa TigoPesa na EzyPesa ambapo hakuna gharama za ziada anayoingia mteja anapotuma pesa kwa mtandao mwingine isipokuwa gharama zinakuwa sawa na zile zile anapotuma kwenye mtandao wake wa TigoPesa ama EzyPesa. Kulia ni Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga.
Mkurugenzi wa Huduma za Kutuma na Kupokea Fedha wa ZANTEL Hashim Mukudi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano maalum ulioandaliwa kwa ajili ya kutangaza ushirikiano kati ya EzyPesa na TigoPesa mapema leo Zanzibar. Anayemfutia ni Meneja wa Biashara wa ZANTEL Zanzibar Mohamed Mussa, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kutuma na Kupokea Fedha wa Tigo Andrew Hodgson na Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga.
---
Kampuni za simu za mkononi za Tigo na ZANTEL zamezindua rasmi huduma za kutumiana pesa miongoni mwa wateja wake Tanzania. Mbali na huduma hiyo ya kutumiana pesa miongoni mwa wateja wa mitandao hiyo, wateja wa EzyPesa na TigoPesa sasa wataweza kutuma na kupokea pesa kwa marafiki na ndugu walio katika mitandao hiyo popote pale nchini.

Kutekelezwa kwa mpango huo kunazifanya Tigo na ZANTEL kuwa viongozi wa huduma kama hiyo Duniani. Haya ni matokeo ya makubaliano yaliyotangazwa mwanzoni mwa mwaka huu na EzyPesa, TigoPesa na Airtel Money.

Jinsi Huduma hiyo inavyofanya kazi: 
Wateja wa Zantel:
Wateja wa Tigo:
1.      Piga *150*02#
1.      Piga *150*01#
2.      Chagua: Chaguo la 1 (Tuma Pesa)
2.      Chagua: Chaguo la 1 (Tuma Pesa)
3.      Chagua: Chaguo la 2 (Tuma TigoPesa)
3.      Chagua: Chaguo la 5 (Tuma EzyPesa)
3.1.   Ingiza Namba ya TigoPesa
3.1.   Ingiza Namba ya TigoPesa
3.2.   Ingiza Kiwango
3.2.   Ingiza Kiwango
3.3.   Ingiza Neno la Siri
3.3.   Ingiza Neno la Siri
3.4.   Subiri Uthibitisho wa Ujumbe Mfupi wa Maneno
3.4.   Subiri Uthibitisho wa Ujumbe Mfupi wa Maneno
 Hakuna gharama za ziada mteja anapotuma pesa kwa mtandao mwingine isipokuwa gharama zinakuwa sawa na zile anapotuma kwenye mtandao wake. Wateja wanaopokea pesa kutoka mtandao mwingine wanaweza kutoa pesa kwa wakala wa mtandao wao na hapatakuwa tena na ulazima wa mteja kutafuta wakala wa mtandao wa mtu aliyemtumia pesa.

Akizungumza kutoka Zanzibar, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Andrew Hodgson alisema: “Tunafuraha kupanua wigo kwa wateja wetu kwa ubia na Zantel. Hatua hii ni muhimu hasa kwa Zanzibar ambapo fursa ya kukua kwa huduma za fedha kwa mitandao ya simu bado ni kubwa.”

Anasema kama ilivyo kwa huduma nyingine za simu kama milio ya sauti na ujumbe mfupi wa maneno, kuna fursa kubwa ya kuimarisha huduma kwa wateja kwa kushirikiana badala ya kushindana baina ya wadau katika sekta ya mawasiliano kwa kupanua huduma za kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao Tanzania.

Anafafanua zaidi kuwa kwa kufanya kazi na wadau wengine, kunawawezesha kupanua wigo wa wateja na hivyo kwa pamoja kutoa huduma ambazo ni bora zaidi, salama, na za haraka kwa wateja wa pande zote.

“Ubia ambao tumeingia leo sio tu utaleta karibu kampuni zetu, bali muhimu zaidi ni ukaribu wa wateja wetu kwa kuwapatia huduma za fedha za kielektroniki bora zaidi ambazo hawakuweza kuzipata hapo awali,” alisema Hodgson.

Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel, Mohamed Mussa, anasema Zantel inaendelea kutimiza ahadi ya kuwarahisishia huduma za fedha wateja wake kwa kufanya kazi pamoja na Tigopesa.

“Kwa kufanya hivi tunapanua wigo kwa wateja wetu, huduma hii inawawezesha zaidi wateja kutuma na kupokea fedha kwa urahisi zaidi,” anasema.

Anafafanua zaidi kuwa kwa huduma hii itasaidia kuimarisha huduma za fedha kati ya visiwa vya Zanzibar na Tanzania Bara.

“Zantel iko katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa ushiriki wa wananchi wa Zanzibar katika sekta muhimu ya fedha unaimarika na kukua. Tumehakikisha kuwa mtandao wa mawakala wetu na watoa huduma wengine wako tayari kuwahudumia wateja wetu,” anasema Bw. Mussa.
Wasamalia wema wakiwa katika eneo la tukio
Namna gari la abiria lilivyo haribiwa na gari kubwa la mizigo aina ya scania
Lori kubwa aina ya Scania limesababisha ajali baada ya kukatiza barabara
ghafla na kuigonga daladala aina ya DCM yenye maba za usajiri T797 BED
lenye kufanya safari zake kati ya G/LAMBOTO to UBUNGO.Ajali hii imetokea  leo maeneo ya Tabata Matumbi jijini Dar es salaam

Damu ambazo ni kwa wale abiria walio jeruhiwa katika ajali hiyo.
 Gari hili likiwa limepasuka vioo vyote na kuumia kwa face ya mbele.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka Nje Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel (Wa pili kutoka kulia) akiwaonyesha ramani ya maonyesho ya Kimataifa ya Elimu kwa wadau wa Elimu waliojitokeza kushiriki maonyesho yanayoanza Leo Desemba 17-21, 2014 katika viwanja Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka Nje Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel akielezea maonyesho ya Kimataifa ya Elimu yanayoanza kesho Desemba 17-21, 2014 katika viwanja Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka Nje Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel akiwakaribisha wagei katika ofisi za GEL.
 Washiriki wa maonyesho ya Kimataifa ya Elimu waombwa kuendelea kujitokeza ili waweze kujitangaza kutokana na maonyesho hayo yanayotarajia kuanza leo Desemba 17-21

Akizungumza wakati wa kuwagawia mabanda, Mkurugenzi Wa GEL alisema bado wanazo nafasi ni vyema washiriki wakajitokeza kwa wingi.
---
Hivi wewe ni mwanafunzi? Je wajua :

·Umuhimu na faida ya mchepuo au kozi unayosoma sasa?

·Fursa ya kozi mbalimbali unazoweka kusoma baada ya kuhitimu elimu yako ya sasa?

· Fani zitokanazo na elimu unayosoma au kulenga kwa sasa baada ya kuhitimu.

·Fursa mbalimbali zilizopo katika soko la elimu kwa sasa?

Yote hayo pamoja na mengine mengi…  zikiwemo taarifa za kozi mbali mbali kama Udaktari, Biashara, Nishati na Madini hususani Gesi, urubani na zingine nyingi zitapatikana kupitia maonyesho ya elimu ya kimataifa yanayofanyika viwanja vya Mwl. J. K Nyerere SabaSaba Dar  s Salaam.

Fahamu pia watakuwepo wauzaji na wasambazi wa vifaa mbali mbali vya elimu kama madaftari, vitabu, uniforms, laptops na kampuni za huduma ya uchapishaji n.k

Wasubiri nini? Usikose kufika katika onesho la kipekee linaloonza, leo Jumatano tarehe Desemba 17 mpaka Jumapili Desemba 2, 2014 kuanzia saa 3 asbh – 11 jioni.

Usidanganyike urafiki wa kweli zama hizi ni wa elimu tu, hivyo basi usikose kumpatia rafiki yako juu ya onyesho hili.


Pia kwa taarifa zaidi, tembelea tovuti yet www.tiee.co.tz au piga simu namba 0656 200200