Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe Zitto Kabwe akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini,Mhe. Ismail Aden Rage wakati akiwasili bungeni kuwasilisha Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti ya ESCROW.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati akiendesha Bunge hilo leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto Kabwe akienda kusoma Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Mhe Zitto Kabwe akisoma Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (GAG) kuhusu akauti ya ESCROW Bungeni Mjini Dodoma leo.
Waheshimiwa Wabunge wakimsikiliza Mhe. Zitto Kabwe (hayupo pichani) wakati akisoma ripoti ya CAG.
Baadhi ya wahudumu wa Bunge wakigawa Ripoti ya GAG kuhusu akauti ya ESCROW kwa Wabunge
Waheshimiwa Wabunge wakipitia ripoti ya GAG kwa makini wakati ikisomwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Mhe Zitto Kabwe.
Baadhi ya waandishi wanaoripoti habari za Bunge wakifuatilia mjadala kwa makini.
Naibu katibu wa Bunge, John Joel akijadiliana jambo na Mhe. Spika Anna Makinda.
Wabunge wakiwa wamesimama kuashiria kuunga mkono taarifa iliyosomwa Bungeni leo na Mhe. Zitto Kabwe.
Mhe Said Arfi akimpongeza Mhe.Zitto Kabwe ,mara Baada ya kumaliza kusoma ripoti ya GAG.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,Mhe DEO Filikunjombe akiwasilisha maazimio ya kamati yake.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuahirisha Bunge mpaka kesho ambapo Serikali inatarajiwa kutoa majibu.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mhe. Stephen Masele akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Bunge kuahirishwa. Picha zote na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii kanda ya kati.

Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akiteta na wanafunzi waliofika kuangalia jinsi mafunzo ya Ujasiriamali yakiendeshwa na Taasisi ya mrembo huyo (BAF) na Taasisi ya Junior Achievements Tanzania. Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akiwa katika pozi na wanafunzi waliofika kuangalia jinsi mafunzo ya Ujasiriamali yakiendeshwa na Taasisi ya mrwembo huyo (BAF) na Taasisi ya Junior Achievements Tanzania. Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred akiwa katika picha ya pamoja na walemavu wa ngozi mara baada ya kumaliza mafunzo ya usajisiriamali kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini.

Na Mwandishi wetu

Taasisi ya Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Foundation (BAF) imeendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana 50 wenye ulemavu wa ngozi.
Brigitte aliendesha mafunzo hayo kwa kushirikiana na taasisi ya Junior Achievement Tanzania yalifungwa jana kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa na kupambwa na maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali mbalimbali ambao ni zao la mradi huo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Brigitte alisema kuwa mafunzo hayo yamelenga mambo mbalimbali katika maisha ya kila siku ikiwa pamoja na kuwawezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha ya kila siku.

Alisema kuwa BAF kupitia Taasisi ya Junior Achievement Tanzania kwa pamoja wameweza kutoa elimu ya kujitambua na stadi za biashara ili walemavu wa ngozi waweze kuthubutu, kuanzisha na kuendeleza biashara na shughuli nyingine za kiuchumi zitakazo wapa ajira, kipato na kuinua ustawi wa maisha yao na familia zao.

Alisema kuwa mpango huu umekuwa wa kipekee kwa kundi hili kwa kuweza kuwajengea mtazamo chanya wakuthubutu, kujiamini na kuweza kufanya mambo makubwa katika maisha.

“Mpango huu umeanza hapa Dar es Salaam, ila Brigitte Alfred Foundation ina azma ya kuuendeleza nje ya Dar es Salaam na kufikia walengwa waliopo mikoa tofauti nchini kwa sababu umeleta manufaa na mabadiliko makubwa sana kwa hawa vijana wenye ulemavu wa ngozi katika muda mdogo na umeonyesha kwamba walemavu wakiwezewshwa,” alisema Brigitte.

Mrembo huyo alitoa shukrani kwa Juniour Achievement Tanzania na wadhamini wakuu, kampuni ya Azam kwa kutoa mafunzo hayo ambayo anaamini wahitimu watayatumia kwa faida zaidi.

“Nawaomba wadau wengine waniunge mkono katika mpango huu kwani awamu inayofuata ambayo ni kutekeleza mipango yao ya biashara katika ujasiriamali ili kuendeleza vijana wetu wa Tanzania hususa walemavu ili weweze kujikimu na kuboresha maisha yao kwa ujumla,” alisema.

 Mkurugenzi wa Fedha wa TDL, Bwana Michael Brown (KUSHOTO) akipokea Ngao ya ushindi kwa TDL baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kama Mlipa Kodi Bora katika kundi la Viwanda, na Naibu Waziri wa viwanda na Biashara Bw Kigoma malima ndie anaemkabidhi tuzo hiyo.  KONYAGI ilinyakuwa tuzo mbili za ulipaji kodi bora. Maofisa mbalimbali wa makampuni mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa tuzo za ulipaji kodi bora nchini. Joseph Chibehe meneja mauzo wa kampuni ya KONYAGI kushoto akibadilishana mawazo na Ofisa wa TBL ambao nao walinyakuwa tuzo. Waziri Kiongozi mstaafu Vuai Nahodha akimkabidhi Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya TDL watengenezaji wa KONYAGI bw. Michael Brown Tuzo ya Mshindi wa Jumla ya Mlipa Kodi Bora katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention centre Wengine katika Picha ni Joseph Chibehe meneja mauzo na Edward Mashingia meneja wa Fedha. Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya TDL watengenezaji wa KONYAGI bw. Michael Brown akiwa na tuzo aliyoipokea. Baadhi ya washiliki walionyakua tuzo za ulipaji kodo bora wakitoka ukumbini na tuzo zao.
 Emerson Oliveira (katikati) na Couthno, wakipokelewa uwanja wa ndege leo mchana.
Mchezaji mpya wa Yanga,Emerson Oliveira Neves Roque (kushoto) akiwasalimia mashabiki wa timu iyo,baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na mchezaji mwenzake Andrey Coutinho.
Maximo akiwasili na mchezaji huyo.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

KIUNGO mkabaji Mbrazil mwenye sifa saba za kiuchezaji, Emerson Oliveira Neves Roque, amewasili jijini Dar es Salaam, leo mchana tayari kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Yanga SC.

Baada ya kuwasili uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akiongozana na Kocha Marcio Maximo na kiungo mshambuliaji Andrey Coutinho, mchezaji huyo alisema; “Ninafurahi kuwafika Tanzania, na niko tayari kupambana, hivyo nimekuja kupambana''.

Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars alisema kuwa Yanga ni timu kubwa yenye wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa, hivyo Emerson anatakiwa kupambana. 

''Emerson anakuja kuchukua nafasi ya mshambuliaji Genilson Santana Santos ‘Jaja’ aliyejiondoa Yanga kwa matatizo ya kifamilia''. alisema Maximo.
Emerson mwenye umri wa miaka 24 mzaliwa wa Rio de Janeiro, anakuja Yanga SC akitokea klabu ya Bonsucesso ya jijini humo, ambayo imewahi kucheza Ligi ya Serie B mara mbili, ingawa kwa sasa inacheza ligi ya jimbo la Rio de jeneiro.

Mchezaji huyo anatarajiwa kuanza majaribio kesho asubuhi katika mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Royola.
Jaja alijiunga na Yanga SC msimu huu, lakini hakuwahi kuwavutia wapenzi wa klabu hiyo, ingawa atakumbukwa kwa mabao yake mawili aliyofunga wakati Yanga SC ikiifunga Azam FC 3-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii Septemba 14, mwaka huu.

Kwa ujumla, katika mechi 11 Jaja aliifungia mabao sita Yanga SC, moja katika mechi saba za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na matatu katika michezo ya kirafiki mbali na hayo mawili yaliyopeleka Ngao ya Jamii Jangwani.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mtaa (Tamisemi), Jumanne Sagini, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo. Kushoto ni  Mkurugenzi Msaidizi Idara za Serikali za Mitaa, ambaye pia ni Mratibu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa, Denis Bandisa.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mtaa (Tamisemi), Jumanne Sagini (katikati), akizungumza na maandishi wa habari katika mkutano huo. 
 Mkurugenzi Msaidizi Idara za Serikali za Mitaa, ambaye pia ni Mratibu wa Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa, Denis Bandisa, akiwaonesha wanahabari daftari la kura wakati akitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa.
 Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo kuchukua taarifa hiyo.
Na Mwandishi Wetu.

WAKATI wananchi wakijishauri kujiandikisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (Tamisemi ) imekiri kuzorota kwa zoezi hilo,na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.

Akizungumza na waandishi wahabari Dar es salaam leo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Jumanne Sagini alisema kuzorota huko kumetokana na serikali kuchelewa kutoa elimu kwa wananchi na hivyo kusababisha kukosa muelekeo.

Alifafanua kuwa kwa kawaida uchaguzi huo hufanyika mwezi oktoba na hivyo waziri mkuu anatakiwa kutoa taarifa hiyo siku 30 kabla lakini kutokana na kuwepo kwa bunge lakatiba hali hiyo ilibadilika na hivyo kuiilazimu serikali kusogeza mbele mchakato huo.

"Nikweli hali hiyo ipo kama mnavyosema wandishi,lakini nyie ndio mnatakiwa kutusaidia kuzidi kutoa elimu,tumekuwa tukifanya vipindi katika vyombo mbalimbali vya habari lakini bado elimu inahitajika zaidi"alisema.

"Na wiki ya kwanza jambo hili lilionekana kuzorota kwa sababu ilikuwa ni wiki ya wagombea kuchukua fomu,wananchi wakajua ni siku ya kujiandikisha,lakini mchakato unakwenda vizuri kwasiku hizi mbili"aliongeza.

Sagini alipoulizwa na wandishi kuhusu mkanganyiko wa vituo vya kupigia kura alisema vituo vyoye vilivyopo katika mazingira ya huduma za Afya zinatakiwa kuondolewa na kupelekwa kwenye shule za msingi ilikuepusha usumbufu kwa kwa wagonjwa.

kauli hiyo ilitokana na kuwepo kwa kituo cha Zahanati ya Tandale kugeuzwa kuwa kituo cha uandikishaji kwa wapiga kura hali inayopeleka wagonjwa kulalamika kuwa wanapata usumbufu,hivyo kuwataka wahusika kuhamisha kituo hicho.

Akizungumzia bajeti ya uchaguzi huo, Mratibu wa uchaguzi Taifa, Denis Bandisa alisema serikali imetenga bilioni 20 kwa ajili ya uchaguzi huo ambapo,kati ya hizo bilioni nane kwa ajili ya malipo ya makarani,bilioni sita vifaa vya kujiandikishia,na bilioni sita kwa ajili ya matumizi mengine.

Hata hivyo Denis hakutaka kubainisha kuwa matumizi mengine ni yapi katika fedha hizo,na kusema kila karani atakuwa atalipwa sh. 10,000 kwa siku kutokana bajeti ya serikali kuwa ndogo.

"Kipindi cha mwanzo tlikuwa hatulipi kabisa,kwasababu sio kazi ngumu,ila kwasasa tukaona sio vema kwa sababu wanatumia nauri zao,tukaamua kutenga kiasi hicho cha fedha ila badae tutaangalia utaratibu wa kuwaongezea katika uchaguzi mkuu"alisema Denis.

Hata hivyo alitaja idadi ya kata zinazo husika na uchaguzi kuwa ni 3,802,mitaa 3741,Vijiji 12,443 na vitongoji 64,616.

Hata hivyo gazeti hili lilipa baadhi ya vituo na kushuhudia makarani wakisema kuwa kwasiku huandikisha wananchi 30.
 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Kwesigabo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu Siku ya Takwimu Afrika itakayo adhimishwa Dar es Salaam kesho. Kulia ni Mtakwimu Mkuu, Adella Ndesengia. 
 " Nilazima picha hii niipate hata iweje' kama anaongea Ofisa Habari wa Idara NBS, Veronika Kazimoto wakati akichukua taarifa hiyo kwa njia ya picha- kweli mama yupo kazini -chezea kazi wewe.
 wanahabari wakichukua tukio hilo.
 Mkrugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Iphrahim Kwesigabo (kushoto), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.

Na Mwandishi Wetu.

OFISI ya Taifa yaTakwimu imeitaka jamii  kutoa ushirikiano wakati wa ukusanyaji wa taarifa za matumizi,kwamba husaidia kuandaa sera na kupanga mipango ya maendeleo nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam  na Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo wakati akitoa taarifa ya maadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yatakayofanyika kesho.

"Maadhimisho ya siku ya siku ya takwimu Afrika hufanyika kila ifikapo Novemba 18 kila mwaka, kwa Tanzania tumechelewa kwa sababu ya utekelezwaji wa majukumu mengine ya kiserikali, hivyo maadhimisho hayo yanafanyika leo," alisema Kwesigabo.

Kwesigabo alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa tasinia ya takwimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa  kuwa ni Waziri wa Fedha kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Yosuf Mzee na kwamba wadau wengine watakaoshiriki ni  wizara, Idara na Taasisi za Serikali, wadau wa maendeleo,vyuo vya elimu ya juu,wadau wengine wa takwimu nchini.OFISI ya Taifa yaTakwimu imeitaka jamii  kutoa ushirikiano wakati wa ukusanyaji wa taarifa za matumizi,kwamba husaidia kuandaa sera na kupanga mipango ya maendeleo nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam  na Mkurugezi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii,Ephaim Kwesigabo wakati akitoa tarifa ya maathimisho ya siku ya takwimu Afrika.

"Maadhimisho ya siku ya siku ya takwimu Afrika hufanyika kila ifikapo novemba 18 kila mwaka,kwa Tanzania tumechelewa kwa sababu ya utekelezwaji wa majukumu mwengine ya kiserikali,hivyo maadhimisho hayo yanafanyika leo,"alisema.

Kwesigambo alisema lengo la maadhimisho hayo ni kuongeza ufahamu kuhusu nafasi na mchango wa tasinia ya takwimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.

Mgeni rasmi anaetarajiwa katika maadhimisho hayo ni waziri wa fedha kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Yosuf Mzee na kwamba wadau wengine watakaoshiriki ni  wizara,Idara na Taasisi za Serikali,wadau wa maendeleo,vyuo vya elimu ya juu,wadau wengine wa takwimu nchini.
 Ndugu pamoja na jamaa wa marehemu Sebastian Mgimba aliyefariki dunia nchini Malaysia wakibeba jeneza lenye mwili wa Marehemu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam eneo la Mizigo ukitokea nchini Malaysia.
Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Sebastian Mgimba aliyefariki nchini Malaysia likiingizwa katika gari maalumu la kubebea jeneza katika uwanja wa Ndege wa Dar Es Salaam katika eneo la kutolea na kusafirishia mizigo mara baada ya mwili huo kuwasilini Nchini Leo ukitokea Nchini Malaysia.
Mchungaji akiendelea na ibada fupi iliyofanyika katika eneo la Kutolea mizigo katika uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam mara baada ya Mwili wa Marehemu Sebastian Mgimba kuwasili nchini leo. Picha zote na Josephat Lukaza.

Msiba wa Marehemu Sebastian Mgimba upo Sinza Kumekucha ambapo baada ya mwili kupokelewa leo uwanja wa ndege wa Dar es Salaam umepelekwa Kwake Sinza na Hatimaye Kesho Kutakuwa na Misa ya kumuombea marehemu na hatimaye Mwili wa Marehemu kupumzishwa Katika Nyumba yake ya Milele Katika Makaburi ya Kinondoni Jijini Dar Es Salaam. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi Amina

Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.
2
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiponda mawe wakati aliposhiriki katika ujenzi wa Bwawa la maji linalojengwa katika kijiji cha Sengenya Mangaka wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara akiwa katika ziara yake ya kikazi akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali pamoja na wananchi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuhimiza uhai wa chama cha Mapinduzi CCM, Katika ziara hiyo leo Kinana amefanya kazi mbalimbali pamoja na kufanya mikutano kadhaa akiwa ameongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. 3
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na mafundi kupanga mawe katika ukingo wa bwawa hilo linalojengwa katika kijiji cha Sengenya Mangaka wilayani Nanyumbu. 4
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo wakati alipokuwa akikagua kituo cha afya cha Mangaka wilayani Nanyumbu ambapo ameelezwa kwamba kituo hicho kimeomba kupandishwa hadhi na kuwa hospitali ya wilaya ambapo kimekidhi vigezo vyote lakini wamesubiri kwa miaka mitatu bila mafanikio. 5
Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo akizungumza na waandishi wa habari adha wanayoipata wagonjwa kutokana na kutopandishwa hadhi na kuwa hospitali ya wilaya pamoja na kukidhi vigezo vyote vya kuwa hospitali ya wilaya. 6
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo katika chumba cha upasuaji kutoka kwa Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo.7
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Mangaka Dr.Ahmed Mtambo mara baada ya kutembelea kituo hicho katikati ni Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Mhe. Festo S. Kiswaga.11
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani, Mh. Festus Kiswaga Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu na Halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Mtwara wakipita kwenye daraja. 13
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata picha ya kumbukumbu na wanahabari walioko katika msafara wake. 15
Shehena ya mbao ziliokamatwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita zikiwa zimehifadhiwa katika ofisi za Mamlaka ya mapato TRA Mtambaswala katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji. 16
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na waandishi wa habari kuelezea uzembe na ukiritimba wa baadhi ya watumishi wa serikali kutokana na suala hilo kuchukua muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi. 17
Halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Mtwara akizungumza na wananchi katika kijiji cha Nanyumbu 18
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akizungumza na wananchi katika kijiji cha Nanyumbu
9
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi , Mh. Festus Kiswaga Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu na Halima Dendegu Mkuu wa mkoa wa Mtwara wakipita kwenye daraja la Umoja.19
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo