Safari ya mwisho ya mpendwa wetu George Njabili.
 Marehemu George Godwin Njabili enzi za uhai wake.
 Mjane wa marehemu (wa tatu), akiwa na watoto na ndugu na jamaa wakati wa ibada hiyo.
 Geneza lenye mwili wake likiingizwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kwa ajili ya ibada hiyo.
 Wachungaji wa Kanisa hilo wakiongoza ibada hiyo.
 Ndugu jamaa na marafiki wa marehemu wakiwa kwenye 
ibada hiyo.
 Hakika ni huzuni kubwa kwa kuondokea na mpendwa wetu George.
 Ni huzuni kwa ujumla.
 Mjane wa George Njabili (katikati), pamoja na watoto wao.
 Ni ibada iliyowagusa wengi waliomfahamu George Njabili.
Wanakwaya wakiimba kwenye ibada hiyo. 
 Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kwenye ibada hiyo.
Ni nyuso za huzuni ndani ya ibada hiyo.
Ndugu na jamaa wakitoa heshima za mwisho.

Mjane wa George akisali na watoto wake mbele ya jeneza la mume wake wakati wakiaga mwili wake.
* (HII NI KUFUATIA VIDEO YA HOUSE GIRL AKIMTESA MTOTO MDOGO INAYOTEMBEA KWENYE MITANDAO)

Inabidi pia wazazi kufahamu kuwa wafanyakazi tunaowaajiri wanatoka katika backgrounds tofauti tofauti sana, na kwa jinsi wengine walivyokuzwa, kunyanyasika au kuonewa au kunyimwa haki labda hadi ndoto zao kukatishwa wakajikuta wanakuwa wafanyakazi wandani tofauti na walivyotamani, ndivyo mianya ya hasira, visasi na machungu hupanuka na kuishia kwa watoto wetu wapenzi tuliowaacha wakae nao nyumbani. 

Huku ukidhani kuwa mwanao yuko salama kumbe yuko kwenye mikono ya muhanga wa maisha ambaye anaishi chini ya dari yako ili tu ale na alale na apate hela kidogo lakini moyoni mwake yamkini mazingira yameshamuandaa kuwa jitu na sio mtu. 

Ni vema tukafahamu historia za wadada na wakaka tunaowaajiri na tukaishi nao chini ya dari moja, unaweza kumuliza katika kupiga story za kawaida tu, jifunze kuwafanya wawe marafiki ili waweze kuelezea matukio yaliyowahi kuwasibu maishani mwao. 

Usimuangalie tu kama mfanyakazi kwasababu unamlipa bali muangalie kama mtu anayekaa na watoto wako, tena anayekaa muda mrefu kuliko wewe. Watu hawa wananafasi kubwa sana ya kuwaathiri watoto wetu katika maisha mazima, tena athari hizi zinaweza kuendelea hadi utu uzima wao. 

Achana na kupigwa au kuteswa kwa watoto wetu, hivyo angalau unaweza kuviona kwa macho, vipo vitu tele tena very sensitive ambavyo huwezi kuviona wala kuvisikia lakini vina athari kubwa sana kwa watoto wetu kutoka kwa wafanyakazi hawa.

 Zaidi ya yote tumruhusu Mungu kuwa mlinzi mkuu kwa watoto wetu kwasababu wenyewe hatuwezi hii kazi.Tuwe macho wapendwa - Dr. Chris Mauki
 Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Angellah Kairuki 
Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Angellah Kairuki (kushoto), akimkabidhi cheti Muhitimu aliyefanya vizuri Shahada ya Kwanza ya Jinsia na Maendeleo, Nyamambara Simon katika Mahafali ya Tisa ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yaliyofanyika Dar es Salaam leo. W apili kulia ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo, Samwel Lunyelele na Mkuu wa Chuo, Profesa Shadrack Mwakalila.
 Vyeti vikiendelea kutolewa.
 Wimbo wa Taifa ukiimbwa- Kutoka kulia ni Kaimu Naibu Mkuu wa Chuo, Samwel Lunyelele na Mkuu wa Chuo, Profesa Shadrack Mwakalila, Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuki, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Maryam Abdallah Yusuph na Mjumbe wa Bodi Dk.Terezya Huvisa (MB).
 Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema (wa pili kushoto), naye alikuwepo na waalikwa wengine.
 Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Ndugu jamaa na marafiki wa wahitimu hao wakiwa kwenye sherehe hizo.
 Mwanahabari, Msuya Selemani (katikati), akiwa na wanafunzi wenzake baada ya kuhitimu Shahada ya Kwanza ya Siasa na Uendeshaji wa Maendeleo ya Jamii. 
 Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Mwanahabari, Msuya Selemani akiwa katika mahafali hayo.
 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo, Maryam Abdallah Yusuph, akizungumza katika mahafali hayo.
 Ndugu wa wahitimu hao wakifuatilia matukio mbalimbali katika mahafali hayo.
 Wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Mjumbe wa Bodi ya Chuo, Dk.Terezya Huvisa MB (kushoto), akitoa shukurani kabla ya kuhitimisha mahafali hayo.
 Wahitimu hawa wakitafakari jambo.
 Wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Blasi band ya Jeshi la Polisi ikitoa burudani.
 Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuku akiwaaga wageni waalikwa baada  ya kumalizika kwa mahafali hayo. Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Shadrack Mwakalila.
Naibu Waziri wa Sheria na Katiba, Angellah Kairuku akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu na viongozi wa chuo hicho.

Na Mwandishi Wetu.

SERIKALI imeendelea kufanya jitihada za dhati  kwa ajili ya kukabiliana na kushuka kwa ufaulu katika vyuo mbalimbali nchini.

Hayo yalibainishwa na Naibu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Angela Kairuki wakati akihutubia katika mahafali ya tisa ya katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam leo kwa niaba ya Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenister Mhagama ambaye alipaswa kuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.

Alisema juhudi hizo za Serikali ni pamoja na Mpango wa Elimu ya Shule za Misingi, Mpango wa Elimu ya Sekondari, Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Ufundi wa miaka Mitano 2013-2014 na 2017-2018 na Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN)

"Jitihada hizi zinaonesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kutafutia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu nchini.

Kairuki alisema juhudi za Serikali zimeanza kuzaa matunda na kujionesha kwa kupanda kwa kiwango cha ufaulu katika shule za Sekondari nchini.

Aliongeza kuwa bajeti finyu ya chuo hicho ni changamoto ambayo ipo katika vyuo mbalimbali vinavyo milikiwa na serikali nchini na kuwa lengo la Serikali ya awamu ya nne ni kuimarisha vyuo vya elimu ya juu ili viweze kutoa elimu iliyobora.

Mkuu wa chuo hicho, Profesa Shadrak Mwakalila alisema changamoto kubwa ya chuo hicho ni pamoja na tatizo la uhaba wa hosteli katika chuo hicho cha Kivukoni na Tawi la chuo hicho Zanzibar hivyo kuwafanya wanafunzi kuishi uraiani.

Alisema katika Kampasi ya Kivukoni, chuo kinahosteli tatu zenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzio 480.

"Katika mwaka wa masomo wa 2013/2014 wanafunzi walioishi kwenye hosteli za chuo nio wanaume 214 na wanawake 266" alisema Mwakalila.

Aliongeza kuwa katika mwaka wa masomo wa 2013/2014 jumla ya wanafunzi 998 sawa na asilimia 67.57 ya wanafunzi 1478 waliishi nje ya chuo na kuwa idadi zaidi ya wanafunzi wanaoishi nje ya chuo inategemewa kuongeza mwaka hadi mwaka.

Katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 689 walitunikiwa cheti, Stashahada ya Kawaida na Shahada ya Kwanza ambapo wanawake ni 400 sawa na asilimia 58.1 na wanaume ni 289 sawa na asilimia 41.9.

Mwaka huu kuna upungufu wa wahitimu 231 sawa na asilimia 25.03 ukilinganisha na mwaka jana ambapo walikuwa 919.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Mkutano wa pili wa Kimataifa kuhusu Lishe na Virutubisho (ICN2) uliofanyika katika ukumbi wa Makao Makuu ya Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Rome, Italia juzi Novemba 19, 2014.
 Papa Francis, akihutubia wakati wa mkutano huo....
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakati wa mkutano huo wa ICN2 (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, James Nsekela na Msaidizi wa Rais katika Masuala ya Lishe Dkt. Wilbald Lorri.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe kutoka Tanzania wakati wa mkutano huo wa ICN2 (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, James Nsekela na Balozi Wilfred Ngirwa (kulia).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango Maalum wa Chakula Duniani (WFP) Ethria Cousin (kulia) na Balozi Wilfred Ngirwa wakati wa mkutano huo wa ICN2, uliofanyika juzi Novemba 19, 2014, Jijini Rome Italy. 
 Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi walioshiriki katika Mkutano huo wa ICN2. Kulia ni Mfalme Letsie III wa Lesotho. 
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa FAO Jose Graziano da Silva, wakati alipomtembea ofisini kwake na kufanya naye mazungmzo, juzi Novemba 19, 2014. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid. 
---
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal Novemba 19, 2014 ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Kimataifa kuhusu Lishe na Virutubisho uliofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) jijini Rome Italia. 

Mkutano huu umefanyika ikiwa ni miaka 22 baada ya mkutano wa kwanza maarufu kwa jina la ICN1 kufanyika katika jiji la Rome na kuazimia kuwa, upo umuhimu wa kuhakikisha binadamu wanapata Lishe bora yenye virutubisho ili kusadia kujenga afya ya binadamu duniani. Mkutano huu wa pili pia umeandaliwa kwa pamoja na Shirika la Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Mkutano huo ulifunguliwa na Balozi wa Kudumu wa Italia katika Umoja wa Mataifa Gianni Ghisi aliyesoma hotuba kwa niaba ya Rais wa Italia Giorgio Napolitano ambapo alifafanua kuwa Rome inawakaribisha wawakilishi wan chi mbalimbali na kwamba inatamani kuona mkutano huu unatoka na majibu ya tatizo la lishe duni kwa watu wa mataifa mbalimbali. 

Katika siku ya ufunguzi pia hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon iliwasilishwa pamoja na uzoefu wa masuala ya Lishe kutoka Italia ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Italia Paolo Gentiloni aliwasilisha hotuba yake huku akiwakaribisha washiriki wa mkutano huu wa ICN2 katika jiji la Rome na kufafanua kuhusu matarajio ya Italia katika mkutano wa sasa ukilinganisha na ule uliofanyika miaka 22 iliyopita.

Akiwasilisha taarifa ya Tanzania, Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wadau wa Maendeleo ambao wamekuwa wakichangia katika sekta za Afya na Kilimo na akafafanua kuwa Tanzania imepiga hatua tangu ICN1 na sasa inahitaji kuona mkutano huu unatoka na maamuzi yanayotekelezeka ili kuwasaidia wananchi wa mataifa mbalimbali hasa watoto na akina mama wajawazito kuwa na uhakika wa lishe bora yenye virutubisho.

Mheshimiwa Makamu wa Rais alifafanua kuwa Tanzania imepiga hatua katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto ambavyo vingi vilitokana na lishe duni na kwamba serikali ya Tanzania inaendelea kulipatia msukumo suala la lishe na virutubisho kwa wananchi wenye uhitaji ili kujenga taifa lenye afya na lenye watu wenye uwezo wa kusaidia nguvu zao katika kuleta maendeleo.

Akizungumza siku ya pili ya Mkutano huo Baba Mtakatifu Fransis alisema haki ya chakula bora si tu kuwa imetolewa na Mwenyezi Mungu kwa binadamu bali pia ni haki inayoashiria utu na ambayo haipaswi kutolewa kama zawadi kwa wanadamu. 

Papa Fransis aliendelea kusema kuwa, katika dunia ya sasa masuala ya chakula, lishe na mazingira yametokea kuwaunganisha binadamu wa mataifa yote sasa kuliko ilivyokuwa huko nyuma na akazitaka serikali za dunia kuhakikisha zinapunguza utupaji wa vyakula sambamba na kuongeza mikakati ya kuhakikisha kila mwanadamu anapata lishe bora.

ICN2 inatazama pia kuhakikisha kuwa nchi zinakuwa na mikakati ya kupunguza utapiamlo na kwamba chakula kinachopatikana kiwe kile kilichoboreshwa ama kuongezewa virutubisho ili kusaidia jamii zinazokabiliwa na matatizo kama utapiamlo kuepukana nayo na hivyo kuwa na kizazi chenye afya bora na chenye uwezo wa kutumika katika uzalishaji ama katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Dkt. Margareth Chan, Mkurugenzi wa WHO aliueleza mkutano huo kuwa suala la lishe ni mhimili katika kufanya jamii inayoweza kukabiliana na magonjwa huku pia Mkurugenzi wa FAO Jose Graziano da Silva akifafanua kuwa, shirika lake linautumia mkutano huu unaoshirikisha nchi 172 kutoa mwongozo kwa dunia kuhusu jambo hili muhimu katika maisha na hasa sasa ambapo tunaelekea kukamilika kwa Malengo ya Milenia na kuanza malengo mapya.

Katika mkutano huo, licha ya Mheshimiwa Makamu wa Rais, Tanzania pia iliwakilishwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid pamoja na Waziri wa Mifugo Dkt. Titus Kamani sambamba na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim. 

Sambamba na kuhudhuria mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais alipata fursa ya kukutana na Jumuiya ya Watanzania wanaishi Italia na kufanya nao mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa sambamba na kukutana na Mkurugenzi wa FAO ambaye alionesha furaha yake kuhusu hatua mbalimbali ambazo Tanzania imepitia na kuahidi ushirikiano zaidi katika masuala ya Kilimo. 

Mheshimiwa Makamu wa Rais na ujumbe wake umeondoka kurejea nyumbani Tanzania tayari kuendelea na shughuli nyingine za Kitaifa leo Ijumaa Novemba 21, 2014.