Simanzi zimetanda jiji la Arusha baada ya watu zaidi ya 15 kufa katika ajali iliyotokea eneo la Tengeru. 

Akiongea na Kajunason Blog mmoja ya mashahidi aliyefika eneo la tukio na hospitali ya Mount Meru amesema ajali ilitokea majira ya saa kumi jioni huko maeneo ya Sadec-Darajani -Tengeru iliyohusisha gari la abiria aina ya Hiace linalobeba watu toka Usa-River kwenda Arusha mjini na Lori la mafuta.

Aliongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hiace (gari la abiria) iliyokuwa ikijaribu kupita magari mengine ndiyo akakutana uso kwa uso na lori hilo. Habari kamili zitawajia punde.
Watu wakiwa wamefika eneo la tukio kutambua miili ya ndugu zao.
President Kikwete has sent a congratulatory message to Her Excellency Dilma Rousseff on the occasion of her re-election as President of the Federative Republic of Brazil

H.E. Dilma Rousseff, President of Brazil

H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to Her Excellency Dilma Rousseff on the occasion of her re-election as President of the Federative Republic of Brazil.

The message reads as follows.

“Her Excellency Dilma Rousseff
  The President of the Federative Republic of Brazil,
  Brasilia,
  BRAZIL.

I have received with great pleasure the news of your re-election to the highest office of your country. On behalf of the Government and people of the United Republic of Tanzania and indeed on my own behalf, I wish to convey my sincere and warmest congratulations to You and through you to the Government and the people of the Federative Republic of Brazil for your election to the Presidency of Brazil.

Your re-election is a sign of the trust and confidence that the people of Brazil have in your leadership qualities. As you continue discharging the noble duties bestowed upon you, I would like to assure Your Excellency of my continued co-operation in further strengthening the bilateral relations that so happily exist between our two countries.

Please accept, Your Excellency, my personal regards and best wishes for your continued good health and success”.

ISSUED BY: THE MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, DAR ES SALAAM

29TH OCTOBER, 2014
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. 

Baada ya makada mbalimbali wa CCM kutangaza nia ya kugombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa anasema bado hajaona mtu mwenye sifa ya kupewa nafasi hiyo kubwa nchini miongoni mwa waliojitokeza.

Hadi sasa ni makada wa CCM pekee waliotangaza nia hiyo ya kumrithi Rais Jakaya Kikwete, wakati vyama vya upinzani vimeingia makubaliano ya kumteua mgombea mmoja kupambana na chama hicho tawala.

Pamoja na wanasiasa wazito wa CCM kutangaza nia ya kugombea urais na baadhi kuanza harakati kabla ya kutangaza, Mchungaji Msigwa anasema wote waliojitokeza hawana dira ya kuipeleka nchi sehemu fulani kutoka hapa ilipo na hivyo hawastahili kupewa nafasi hiyo.

Akizungumza katika mahojiano mwishoni mwa wiki iliyopita kuhusu mambo mbalimbali ya kisiasa na kijamii, Msigwa alisema kujitangaza kwao siyo tatizo, lakini haoni kama kuna mtu mwenye sifa za urais. “Ukimuuliza kila mmoja kwa waliojitangaza kwamba ana vision (dira) gani kwa ajili ya nchi katika miaka mitano ijayo, wengi watatoa ahadi badala ya kueleza ataifikisha nchi wapi katika muda huo,” alisema mchungaji huyo bila ya kutaja majina ya waliojitokeza.

“Wengi kati ya hawa wanaojitangaza wanataka power (madaraka) ya kulinda status quo (nafasi zao), lakini nakuhakikishia hawana ‘vision’. Wanatumia hela zao kununua madaraka.”

Alisema hata siku moja mti wa mwembe haujawahi kumwita mtu akatungue maembe, bali msimu ukifika watu hufuata mti na kutungua maembe, akimaanisha wanaojitangaza sasa hawajafuatwa na mtu wajitangaze. “Tunahitaji mtu mwenye dira nzuri na si watu ambao watatupa ahadi ambazo hazitekelezeki,” aliongeza mchungaji huyo wa Iringa Vineyard Church na ambaye pia ni mratibu wa taifa wa kanisa hilo.

Pia, Mchungaji Msigwa alisema ni wapinzani pekee ambao wana mtu ambaye ana dira na ambaye wakati ukifika atajitokeza kutangaza kuwania kuingia Ikulu.

“Katika Ukawa viongozi wetu wakiafikiana na tukapata mtu mwenye maono ambaye ana anakubalika pia anaweza kupambana na mambo, tutafanikiwa,” alisema.

Akizungumzia makubaliano ya vyama vya upinzani kusimamisha mgombea atakayeungwa mkono na wote katika ngazi zote kuanzia Serikali za Mitaa alisema, “Kuna tofauti kati ya mwanasiasa na kiongozi. Mwanasiasa ni mtu anayependa kufanya mambo mazuri, lakini kiongozi ni mtu anayefanya mambo sahihi,” aliongeza:

“Mtu anayefanya jambo sahihi mara nyingi anafanya kwa kuwa jambo hilo linakuwa linaumiza, lakini mtu anayefanya mambo mazuri siku zote anafurahia.

“Siasa za siku hizi zimebadilika, hivyo mtu anayezifanya lazima ajue kwamba kuwa mwanasiasa na kuwa kiongozi ni vitu viwili tofauti.”

Hivyo alisema ni muhimu kwa wananchi kuwachunguza hao wanaojitangaza kuwania urais na kuzijua tabia zao kuanzia sasa. “Ukichagua mwizi, lazima atakwenda kuiba kwa sababu ndiyo tabia yake, hivyo ni lazima tuwachunguze, tuwajue ili tusije kuchagua watu wenye hulka ya wizi,” alisisitiza na kuongeza: “Tuwachunguze hawa watu na tusikurupuke.”
no image

A dog has taken on the role of foster parent to two young children in a small village in Kenya. The motherly dog named Oscar keeps a watchful eye on the young children and escorts them to and from school every day.

Seven-year-old Mbogo and six-year-old Wanjiku were abandoned by their alcoholic mother after she could not care for them. They are now in the care of their grandmother. But with five other children to look after, their grandmother cannot watch over them all the time.

Oscar began looking after the children around 6 years ago, taking on the role of their protector. She is well liked by many residents in the Kirigu Village in the Dagoretti area of Nairobi, and her motherly duties have made her a bit of a legend.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Tano la Kimataifa la kujadili matumizi ya Nishati itokanayo na joto ardhi katika Nchi za Afrika zinazopitiwa na bonde la ufa. Kongamano hilo limeanza leo Oktoba 29, 2014 katika Ukumbi wa AICC Jijini Arusha.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt Bilal, kufungua kongamano hilo. 
Baadhi ya Wabunge wa Kamati ya waliohudhuria kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal, wakati akihutubia. 
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika waliohudhuria Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo baada ya ufunguzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya washiriki wakati akiondoka eneo hilo baada ya kufungua kongamano hilo. Picha na OMR
Na Mwandishi Wetu

Baada ya siku ya Jumanne kuamkia Jumatano kuzagaa kwa uvumi kuhusu kufariki kwa rais wa Zambia Michael Sata, hatimaye hii leo Serikali ya nchi hiyo imethibitisha kifo chake.

Satta aliyekuwa na umri wa miaka 77 alisafiri kuelekea jijini Londo Uingereza juma moja lililopita kwaajii ya kupata matibabu zaidi lakini hii leo katibu wa baraza la mawaziri, Roland Msiska amethibitisha kifo chake.

Akitoa tangazo hilo mapema leo alfajiri, Roland amewaambia wananchi wa Zambia kwa masikitiko makubwa angependa kutangaza kifo cha rais wao aliyekuwa akipatiwa matibabu nchini Uingereza.

Tangazo hili linathibitisha madai ya vyama vya upinzani na watu wa karibu wa rais Sata ambao mara kadhaa walidai kuwa kiongozi huyo anaugua na ameshindwa kutekeleza majukumu yake kama rais lakini mara zote Serikali imekuwa ikikanusha hadi juma moja lililopita ilipothibitisha kuugua kwa rais Satta.

Wakati alipokuwa akiondoka kuelekea jijini London kwa matibabu, rais Sata alimteua waziri wa ulinzi na sheria Edgar Lungu kukaimu madaraka ya rais kwa kipindi ambacho hatokuwepo.

Makamu wa rais Guy Scott ambaye mara kadhaa amekuwa akishiriki shughuli mbalimbali za Serikali kama kiongozi wa nchi, yeye ana uraia wa Uskochi hali ambayo inamfanya ashindwe kuwa rais kamili wa taifa la Zambia kwakuwa wazazi wake hawakuzaliwa nchini Zambia.

Satta ambaye alibatizwa jina la "King Cobra" na wafuasi wake wakati alipochaguliwa mwaka 2011, alionekana kama mbadala wa siasa za Zambia na mtu ambaye alikuwa wavitendo licha ya kukosolewa kwa sehemu kubwa na upinzania.

Hivi karibuni rais Satta alianza operesheni dhidi ya wapinzani wake na waandishi wa habari wlaiokuwa wakikosoa Serikali yake jambo ambalo lilianza kumchora kama mmoja wa viongozi wababe kusini mwa bara la Afrika.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Rajabu (aliesimama) akizungumza wakati wa kuwakaribisha Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii,waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.Katika ziara hiyo ya Wabunge chini ya Mwenyekiti wao,Mh. Said Mtanda (katikati) walivutiwa sana na maendeoe ya miradi hiyo na hivyo kulipongeza Shirika la NSSF kwa kazi nzuri wanayoendelea kufanya. Picha zote na Cathbert Kajuna na Othman Michuzi.
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka (aliesimama) akifafanya jambo mbele ya Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam
Mbunge jimbo la Lindi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Salum Barhan akifatilia kwa makini taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni iliyokuwa ikitolewa na Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo (hayupo pichani)
Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo akielekeza jambo wakati akitoa taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni mbele ya Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii waliofanya ziara ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Manyovu Mkoani Kigoma,Mh. Albert Obama akiuliza swali kwa Meneja Miradi wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mhandisi John Msemo kuhusiana na mradi huo wa Daraja la Kigamboni.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii wakisikiliza kwa makini taarifa ya Mradi wa Daraja la Kigamboni.
Meneja wa Mradi wa ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Mhandisi Karim Mattaka (katikati) akiwaeleza Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii namna wanavyopanga nondo ili kuweka uhimara wa daraja la Kigamboni ambalo linatarajiwa kumalizika mapema mwakani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda (wa tatu kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (wa nne kushoto) wakati wajumbe wa kamati hiyo wakitembelea Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii wakiangalia namna maji yanavyotolewa chini kwa ajili ya kuweka nguzo za Daraja la Kigamboni.
Waheshimiwa wakijadiliana wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (wa pili kulia mbele) akimuongoza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda alieambatana na ujumbe wake wakati wakitembelea miradi mitatu inayofadhiliwa na NSSF ambayo ni Mradi wa Daraja la Kigamboni,Mradi wa nyumba wa Mtoni Kijichi na Mradi ujenzi wa kijiji cha kisasa kiitwayo 'Dege Eco Village',iliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Maendeleo ya Mradi wa Daraja la Kigamboni.
 Ubao wa Maelezo ya Mradi wa Kijiji
Baadhi ya Nyumba za Mradi wa Kijichi.
Mh. Obama akiangalia Mandhali tulivu ya Kijichi.
Wadau wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ziara hiyo.
Majengo yanayoendelea kujengwa katika eneo la Mradi wa Kijichi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau akielekeza jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii. 
Mh. Maua Daftari
Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu.
Baadhi la Majengo ya Mradi wa Kisasa wa Dege eco Village yakiendele kujengwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,Mh. Said Mtanda akizungumza na wanahabari walioambatana nao kwenye ziara hiyo.
Picha ya pamoja ya Wabunge Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii pamoja na Viongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) mara baada ya kumalizika kwa ziara.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza (wa pili kushoto), Mbunge wa Ilala na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Mussa Azzan Zungu (kulia), Mbunge wa Tumbe Mhe Rashid Ally Abdallah (kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini China Luteni Jenerali (Mst.) Abdulrahman Shimbo muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam jijini Hanoi leo Oktoba 28, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na wenyeji wake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi tayari kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam leo Oktoba 28, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na wenyeji wake katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi tayari kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam leo Oktoba 28, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhandisi Christopher Chiza na Balozi wa Tanzania nchini China Luteni Jenerali (Mst.) Abdulrahman Shimbo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Noi Bai jijini Hanoi tayari kuanza safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku sita nchini China na Vietnam jijini Hanoi leo Oktoba 28, 2014

PICHA NA IKULU
Shirikisho la kandanda Ulimwenguni ( FIFA ) hii leo limetangaza jumla ya majina 23 wa wachezaji wa soka watakaowania tuzo ya Mchezaji bora wa FIFA " Ballon d'Or " kwa mwaka 2014. 

Hata hivyo kabla ya mwezi wa 12, majina hayo yatachujwa na kubakizwa majina ya wachezaji 3 ambao ndio wataingia katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo hiyo. 

Mshindi atakabidhiwa tuzo hiyo January 12' 2015 mjini Zurich, Uswis.Majina hayo ya wachezaji na nchi wanazotoka ni kama ifuatavyo:-

Gareth Bale (Wales), Karim Benzema ( Ufaransa ), Diego Costa ( Hispania ), Thibaut Courtois ( Ubelgiji ), Cristiano Ronaldo ( Ureno ), Angel Di Maria (Argentina ), Mario Goetze ( Ujerumani )

Wengine ni Eden Hazard ( Ubelgiji ), Zlatan Ibrahimovic (Sweden), Andres Iniesta ( Hispania ), Toni Kroos ( Ujerumani ), Philipp Lahm ( Ujerumani ), Javier Mascherano (Argentina ), Lionel Messi (Argentina ).

Pia wamo Thomas Mueller ( Ujerumani ), Manuel Neuer ( Ujerumani ), Neymar ( Brazil ), Paul Pogba ( Ufaransa ), Sergio Ramos ( Hisapnia ), Arjen Robben ( Uholanzi ), James Rodriguez (Colombia), Bastian Schweinsteiger ( Ujerumani ), na Yaya Toure (Ivory Coast).