Regional retailer Nakumatt Holdings has announced the scheduled late opening of all its branches across East Africa this Sunday to allow the firm observe the Westgate Shopping Mall Terror attack first anniversary memorial activities.

One year after the tragic terror attack, Nakumatt which hitherto operated its flagship store at the Westgate Mall will this Sunday conduct interdenominational religious prayers across its network.
Speaking when he confirmed the memorial plans ahead of the events, Nakumatt Holdings Managing Director Atul Shah disclosed that the supermarket chain will remain closed early morning for the prayers scheduled to commence at 9am on Sunday.

The prayers will be led by respective Nakumatt branch chaplains and catechists and will be open to members of the public. All branches are expected to reopen from 10am after the memorial prayers.
Still on Sunday, the firm will also disrupt its normal operations at 12noon to observe a minute of silence in memory of the departed souls and victims of the terror attack. The observance of the branch wide minute of silence in Kenya will be followed by the recital of the National Anthem which is also a powerful prayer to God.
“The events on that fateful Saturday midmorning are still very painful and the entire Nakumatt fraternity shall be taking time off on Sunday to say our memorial prayers to seek God’s comfort, global peace, love and harmony,” Shah explained.

In Nairobi, Shah, will also lead Nakumatt staffers to light a memorial candle outside the Westgate Shopping mall at 12noon on Sunday.

One year ago, Nakumatt Holdings suffered the loss of three of its dedicated staff members the late Veronicah Wairimu, Kennedy Mogaka and John Musango Mutinda who were fatally shot at the mall. The retailer, also lost its flagship Nakumatt Westgate branch to a mysterious fire just days after the terror attack.

Since then, Nakumatt which had a branch complement of 40 branches has managed to set off on a recovery path and recently opened its 50th branch in Arusha, Tanzania.
Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar
Siku moja baada ya mtoto Happiness Robert kupotea tena katika mazingira ya kutatanisha huko nyumbani kwao Mkuranga, Jeshi la polisi kanda maalum limefanikiwa kumpata mtoto huyo katika bandari ya Dar es Salaam sehemu ya kupandia meli za kwenda Zanzibar.

Jeshi hilo lilimpata mtoto huyo majira ya saa moja na nusu usiku ambapo askari hao wakiwa doria kwenye eneo hilo.

Akithibitisha kuokotwa kwa motto huyo kamanda wa polisi Mkoa wa Ilala Mary Nzuki amesema kwamba kwa mujibu wa askari waliomuokota walipomuhoji mtoto huyo alisema anataka kurudi tena Zanzibar.

Akizungumza mama wa Mtoto huyo amesema kwamba baba wa motto huyo wameachana tangu miaka sita iliyopita na walikuwa katika mgogoro hadi kufikishana katika vyombo vya dola na baada ya hapo ndipo hali hii inayo mkuta mtoto wake kuanza kumtokea.

Aidha Mama huyo amesema kwamba motto huyo amekuwa wa maajabu sana kwake kwani kuna wakati anatembea kama nyoka.

Naye motto huyo amesema kwamba kuna mtu alikuja kumchukua usiku na kumpeleka hapo bandarini na kasha kumtelekeza hapo.

Hata hivyo motto huyo amesema kwamba anahitaji msaada wa kuendelea kusoma.
Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog, Dar

Chama cha waandishi habari wanawake (TAMWA) kimezindua ripoti ya pili ya unyanyasaji wa kijinsia ambapo Takwimu zimeonyesha kuwa matukio ya unyanyasi kwa mwaka huu yamepungua kwa kiasi kikubwa.

Takimu hizo zimeonyesha uelewa wa wanachi katika suala zima la unyanyasaji wa kijinsia umeongezeka na wamekuwa mstari wa mbele katika utoaji wa Taarifa kwa vyombo vya sheria.

Akizindua ripoti hiyo mwenyekiti wa Tamwa Rose Reuben amesema kwamba Utafiti huu ulifanyika katika wilaya kumi na ulilenga masuala yote ya ukatili wa kijinsia.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Tamwa Gladness Munuo amesema kwamba kulingana na Takwimu zilizotolewa katika suala la ubakaji katika wilaya ya Unguja Magharibi Zanzibar umepungua ukitofautisha na miaka mingine ambapo katika wilaya ya Ilala Dar es Salaam kwa mwaka huu takwimu zimeongezeka ulinganisha na mwaka 2013.

Aidha Munuo amesema kwamba kuna changamoto kubwa katika wilaya ya Newala kwenye vituo vya afya kwa kuwa watoto wadogo njia za uzazi wa mpango ambapo bado itakuwa na kichocheo kikubwa cha watoto hao kupata virus vya ukimwi.

Rapoti hii ni ya pili ambapo Takwimu zinaonyesha kuna mabadiliko makubwa ya mafanikio katika Takwimu.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Wazalendo wa Vyuo vya Elimu ya Juu Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Omary (katikati), akizungumza na waandishi wa habari wakati akisoma tamko hilo. Kulia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Theodora Malata na Mwanachuo Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Rehema Akukweti.
Wawakilishi wa wanafunzi wa vyuo vikuu 12 vya Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Mwanachuo wa UDSM, Gulatone Masiga akijibu maswali ya waandishi wa habari. Kushoto ni Mwanachuo Mwita Nyarukururu na Mwenyekiti wa umoja huo, Mussa Omary.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Theodora Malata, akichangia jambo wakati wa kujibu maswali ya wanahabari.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwanachuo Mussa Mashamba kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii, akisisitiza jambo wakati akijibu maswali ya wanahabari. Kulia Massoro Kivuga na William Haule.

Na Dotto Mwaibale.

UMOJA wa Vijana Wazalendo wa Vyuo Vikuu 12 vya Mkoa wa Dar es Salaam, wamemshukia Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kwa kutaka kuitisha maandamano ya kupinga Bunge Maalum la Katiba.

”Sisi umoja wa vijana wa vyuo vikuu tunapinga vikali kauli hiyo na kulaani vikali ya kuhamasisha uasi kwa njia ya maandamano,”alisema.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa vijana hao Mussa Omary alisema kauli aliyotoa mwenyekiti huyo inahamasisha kuleta mgogoro nchini.

”Tumesononeshwa na kauli hiyo ya kibabe ya kiongozi huyu ya kuhamasisha vurugu ambazo tumezishuhudia zikisambaratisha umoja wa nchi nyingi na kuwa chanzo cha vita,”alisema.

”Tulimsikia akiahidi maandamano bila kikomo kwa kibali cha polisi au hata bila kibali cha polisi mbele ya wajumbe ambao wengine sio watanzania,”

Omari alisema uzito wa jambo hilo unaonesha wazi kuwa Mwenyekiti huyo hasatahili hata kidogo kuweza kupewa uongozi wa nchi hii.

Aliongeza kuwa mwenykiti huyo na viongozi wenzakae wanatumia maandamano na damu za watanzania kutafuta fedha kwa wafadhili wao ambao hawaitakii nchi hii mema.

”Wakiandaa maandamano haya huwa wanapiga picha na kuwatumia wafadhili wao na kupata fedha na kujenga majumba na kununua magari makubwa na huku watanzania wakiendela kuathirika,”alisema.

Alisema thamani ya mtanzania mmoja ni kubwa kuliko hiyo katiba mpya wanayodai ni vizuri watanzania kuacha kuwaunga mkono na kufanywa kama mbuzi wa kafara.

Aliongeza kuwa ni vyema vyombo vya dola visiweze kuvumilia kauli hiyo iliyotolewa hivyo kuendelea,kulinda kutunza na kuweza kuiendeleza amani ya nchi.

”Ni vizuri watanzania wakakaa na kufikiria kauli hii ya mwenykiti huyu na kujiuliza kuwa je ni kweli anaweza kuwa kiongozi wa nchi hii,”alisema.

Naye,mmoja wa wanafunzi hao Theodera Nalaya alisema ni vizuri tukaliachia bunge maaluma likafanya kazi yake ya kutafuta katiba mpya.

”Sisi kama vijana wa vyuo vikuu msimamo wetu ni kuwa tuliachie bunge la katiba likafanya kazi yake na muda ukifika wa kutoa maoni yetu ukifika tutatoa maoni yetu na si kuvamia,”alisema.
Karibuni wateja wote MARANATHA GRAPHICS SOLUTIONS hawa ni mabingwa wa kudizaini na uchapishaji aina mbali mbali kulingana na mahitaji yako. Unaweza kuwasiliana nao 0715 040 310, Wanapatikana Mivinjeni-Kurasini jijini Dar es Salaam.
Kutana na Mkurugeni wa Maranatha Graphics Solutions, Imani Ntila... Mtaalamu wa mambo yote.

 Mfanyakazi wa Maranatha Graphics Solutions akibandika stiker.

Wanaprint pia vikombe.

Kama utahitaji mabango ya nakshi nakshi waone Maranatha Graphics Solution. 


Mkurugeni wa Maranatha Graphics Solutions, Imani Ntila akiwa kazini.
 
 Mara baada ya kazi akishoo love.

Sikuzote mteja ni mfalme hufuatwa alipo na kuchukiliwa vipimo stahiki.


Wanaprint tisheti kwa mitindo tofauti unayopenda wewe mteja.
Nembo za biashara.

Mabango ya matangazo kwenye magari.
Kuchapisha mikoba. Kazi zote zimefanywa na MARANATHA GRAPHICS SOLUTIONS.
Mkurugenzi Mkazi wa Amref Health Africa Tanzania, Dr. Festus Ilako (Kulia) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Naibu Mkurugenzi Dr. Rita Noronha.
Msanii maarufu wa kizazi kipya Banan Zorro ametangazwa pia kuwa balozi wa Kampeni hii ya Stand Up for African Mothers inayoendeshwa na Amref kusomesha wakunga ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
Msanii Maarufu wa Kizazi Kipya Mwasiti( Kulia) ametangazwa kama Balozi wa kampeni ya Stand Up For African Mothers, akiongea na waandishi wa habari.

Na Mwandishi Wetu.

Nchini Tanzania, wanawake 7,900 hupoteza maisha kila mwaka wakati wa kujifungua. Zaidi ya asilimia 80 ya vifo hivi vingeweza kuepukika endapo wahudumu wa afya wenye utaalamu wangetoa huduma kwa wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua. Kwa kuamini kuwa hakuna mwanamke anayepaswa kufa wakati wa kujifungua, Shirika la Amref Health Africa Tanzania kwa kushirikiana na Bank za Barclays na Bank M leo wametangaza nia ya kuongeza nguvu na juhudi za kutunisha mfuko wa kusaidia mafunzo ya wakunga kupitia kampeni yake ya Stand up for African Mothers.

Kampeni hiyo ya kimataifa inalenga katika kuongeza uelewa juu ya mchango unaotolewa na wakunga wenye ujuzi katika kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wachanga. Kampeni hii pia inalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wakunga 15,000 katika nchi 13 za Afrika, kati yao wakunga 3800 wanatarajiwa kupata mafunzo nchini Tanzania ifikapo mwaka 2015/2016. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Changia mafunzo ya wakunga , okoa maisha ya mama na mtoto” kwa kuunga mkono nia hii njema unasaidia kuwapatia mafunzo wahudumu wa afya walio mstari wa mbele kuokoa maisha ya mama na mtoto nchini Tanzania
Nchini Tanzania kampeni hii ilizinduliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete tarehe 15 Mei mwaka 2012. Mke wa Raisi amekuwa balozi wa kampeni hii akiongoza juhudi za kuwaokoa kina mama wa kiafrika. Tunayo furaha pia ya kuwatangaza wanamuziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Banana Zoro na Mwasiti Almasi ambao wamejitoa katika kushiriki na Amref Health Africa kuelimisha jamii juu ya afya ya mama na mtoto kupitia kampeni hii ya Stand up for African Mothers.

Mpaka sasa, fedha zilichongishwa kupitia kampeni hii zimewezesha kusomesha wakunga 80 kwa kiwango cha cheti; wakunga 10 wanatarajiwa kuhitimu mwezi wa 11 mwaka huu na 70 wanaingia mwaka wa pili wa mafunzo yao. Jumla ya wanafunzi 176 wanaongeza ujuzi kwa kupata mafunzo ya ukunga kwa njia ya masafa, ili kuongeza elimu kutoka kiwango cha cheti hadi diploma. Mafunzo hayo yanaendeshwa kati ka vituo kumi vilivyo katika mikoa ya Mbeya, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro, Mwanza, Mara, Zanzibar and Mtwara. Na kiasi cha fedha kilichopatikana mwaka 2013 kinatarajia kusaidia wanafunzi 60 watakaoanza masomo yao mwezi wa 10 mwaka huu.

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo Mkurugenzi wa Amref Tanzania Dr. Festus Ilako alisema “Tunatoa mchango wetu katika kulisaidia Taifa kufikia malengo yake ya millennia (MDGs) yanayohusiana na afya kwa kuboresha huduma za afya na kuchangia katika kuboresha hali ya sasa ya afya ya uzazi. Mafunzo ya ukunga yatawaongezea ujuzi wakunga walioko na kufundisha wakunga zaidi ambao baada ya kuhitimu watatoa huduma za afya ya uzazi katika zahanati hivyo kuchangia katika kupunguza vifo vya kina mama vinavyoweza kuzuilika. Tunatoa rai kwenu kuunga mkono na kubadilisha maisha ya kina mama”

Tunawashukuru wadhamini wote walio pamoja nasi katika kufanikisha juhudi hizi. Bank M na Barclays bank wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia mafunzo ya wakunga kuanzia mwaka 2013 mpaka sasa. Pia tunatambua mchango mkubwa uliotolewa na Benki ya Authetic Media Group, BG, Coca Cola Excel Management, FBME, KPMG, NBC, MICHUZI Blog, Mohan’s LTD, Jaffsher foundation LTD, Jamii forums, KCB bank, UCHUMI Supermarket, IPP Media, Push Mobile, , PWC, Pyramid Pharma, Southern Sun Hotel, Songa's, SERENA Hotels, Serengeti Breweries, Stanbic Bank and TCRA.

Ombi letu kwa mashirika, makampuni ya uma na yale ya binafsi, pamoja na watu binafsi ni kuunga mkono jitihada hizi kwa kudhamini mafunzo ya wakunga (mafunzo ya mkunga mmoja yanagharimu dola 3000). Unaweza kuchangia kwa njia mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kupitia

• Account ya benki National Bank of Commerce (NBC), Corporate Branch, Akaunti Namba 0111030004548
• Mpesa Namba 0762 22 33 48
• Tigo pesa Namba 0716 032 441
• Airtel money Namba 0685 506306.
The idea behind the party is to popularize trance music in Tanzania and Africa at large. Trance music is popular in the west and is an attraction of the whites. Plans are underway to have several Tanzania Bongo Artists to do REMIXES to their Hit songs. This will give them international appeal.

The most anticipated Fresh Masala: Trance Urban Party organized last weekend at the High Spirit Lounge was such a great success. It started off with the local Djs doing their thing while building up the tempo.

When the International DVJ Delph took to the Decks, it was NOT business as usual, since everybody in the house wanted to see what the “UPS”. It was NOT easy for this Vj since it was his first time in Tanzania and did NOT know the music preference for these beautiful people of BONGO ( Dar es salaam Party Animals).
 It took Vj Delph nearly fourty five minutes or so to synchronize with the party people. He touched their hearts through KWAITO ( South African Music Hits). The Bongo party animals are great lovers of Kwaito. Here now the party started to Rock. After Kwaito VJ Delph gave another HOT direction the Naija. ( Naija is Nigerian music hits). Here again the direction was rocking. After which it was now full power mix and match with Trance, House, Electro Hits and all round urban Hits.

With super presentation on the LIVE video screens it was party that has NEVER been seen in the History of partying in Dar es salaam and Tanzania. The audience went wild. The fusion of Trance urban hits and Bongo music was such an attraction that the party people loved.

The party that was sponsored by Jim Beam American Whisky, RedBull energy drink and Pepsi was the party that Dar es salaam has been missing. The standards of organization by Starlight Moon, a marketing and promotions agency was quite styling and fulfilling.

The party people and especially the HOT gals could be heard yelling with happiness. With the party house down and upstairs, it was a beehive of partying activities. Several Bongo celebrities were in the house including, Mwana FA, Vannessa Mdee,Dj Peter Moe, Shadee of Clouds Dj. They all had good time
 The next party is set for 10th October 2014 at the same venue, High Spirit Lounge. This coming party is expected to be hotter and pulsating since the DVJ Delph and the Dar Party people now have a GRAND chemistry. The chemical equation is very necessary for any entertainer, Dj included to perform successfully at any given party.

Meanwhile Vj Delph is a Seasoned all round Dj. He has performed in several International Dj arenas, including Germany, UK, Austria, California USA, Nairobi and Mombasa Kenya.

Currently Vj Delph has permanent contract on Saturdays in Mombasa Kenya, where he performs at an upscale facility, the Yuls beach Club. His audience is upscale personality with an understanding for urban international music blending locals, tourists, Asians, Arabs and pure affluent personality.
The Fresh Masala Team is studying the Dar es salaam emerging market for the Trance Partying and there are strong possibilities that the party would soon be every Friday Nite, after the 10th October 2014 party.

The Starlight Moon Marketing agency under the Fresh Masala Brand, has introduced in the Market a new BRANDS activation during the party “ The big screen live activation and hyping”. Also the promotions are done differently from the usual style. Here the Fresh Masala Team produces missed tape DVDs which are given free to target market to play at home. Several TVCs have been inserted therein.

Dar es salaam party people get ready for the second TRANCE URBAN PARTY on second Friday of October the 10th 2014 at the High Spirit Lounge, @ the IT plaza Ohio Street.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Dkt. Ambwene Mwakyusa (wa kwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika leo ofsini kwao kuhusu tuzo mbalimbali za mashindano ya insha zinazotaraji wa kutolewa kesho katika mkutano wa 22 wa Bodi hiyo (katikati) ni msajili wa Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Bw. Jehad Jehad, (wa kwanza kushoto) ni mtendaji wa bodi hiyo.
Msajili wa bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Jehad Jehada kifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam. (kulia) ni mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi, Dkt. Ambwene Mwakyusa.

Na Mwandishi Wetu.

Wanafunzi nchini wamehimizwa kushiriki katika mashindano mbalimbali yanayoandaliwa na Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi chini ya Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB) ili kuwajengea uwezo wa udadisi utakaowawezesha kupenda masomo ya Sayansi na kuongeza idadi ya wataalam hao nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Msajili wa bodi hiyo Bw. Jehad Jehad, amesema bodi yao imeimarisha mashindano ya insha kwa wanafunzi wa kidato cha pili ili kuwajengea uwezo na kuondokana na dhana ya ugumu wa masomo ya Sayansi uliopo kwa watu wengi.

“Kwa kuzingatia wanafunzi ni wadau muhimu wanaohitaji kuelewa fani hizi ili hatimae waamue kusoma taaluma hizi, Bodi imeandaa mashindano ya insha kwa wanafunzi wa kidato cha pili, alisema Msajili.

Pia Msajili wa Bodi hiyo alibainisha kuwa endapo wanafunzi wa kidato cha pili watakapofahamu taaluma hizi wataweza kushawishika kusoma masomo ya Sayansi wafikapo kidato cha tatu na hatimae kuamua kusomea taaluma hiyo.

Aidha, Bw. Jehad alifafanua kuwa mwaka jana Bodi ilipokea jumla ya insha 954 kutoka mikoa 13 na kuchambuliwa na jopo la wataalam kwa kutumia vigezo mbalimbali vikiwemo uelewa wa somo linalolengwa, matumizi ya lugha na mantiki katika mtiririko wa mawazo.

Bw. Jehad aliongeza kuwa mashindano ya insha ya mwaka jana yalibeba mada inayozungumzia ‘utaratibu utakaotumika katika mchakato wa kupata majengo mawili ya madarasa na maabara bora kushinda yaliyopo sasa katika shule ikiwa ni pamoja na wataalam wanaotakiwa’.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Ambwene Mwakyusa, amesema kuwa tuzo mbalimbali zinatarajiwa kutolewa kwa washindi hao ikiwemo ya washindi kumi wa kitaifa, Mshindi mmoja kwa kila mkoa ulioshiriki, shule iliyopata mshindi wa kwanza kitaifa pamoja na shule iliyotoa washiriki wengi.

Pia Dkt. Mwakyusa amefafanua kuwa tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa kesho katika mkutano wa elimu endelevu wa 22 wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi utakaofanyika katika ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania (BOT).

Jumla ya wanafunzi 109 wamepata tuzo hadi kufikia mwaka 2012 ambapo 66 kati yao ni wasichana tangu tuzo hii kuanzishwa mwaka 2008.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban ki  Moon akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) siku ya jumanne ambapo alitumia fursa hiyo kuainisha masuala mbalimbali yatakayopewa kipaumbele wakati wa  Mkutano wa 69 wa  Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa  unaoanza wiki ijayo  hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  jijini New York, Marekani.  Mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola ni  moja ya  suala litakalopewa kipaumbele cha pekee wakati wa mkutano huo utakaohudhuriwa na  wa viongozi  zaidi ya 140 wakuu wa nchi na serikali,   viongozi wa  asasi za kiraia, na wakuu wa mashirika mbalimbaliya Kimataifa.
---
Na Mwandishi Maalum, New  New York

 Viongozi  Wakuu wa Nchi na Serikali  zaidi ya 140 kutoka mataifa mbalimbali duniani  wamethibitisha  kuhudhuria na kushiriki  majadiliano ya  jumla wakati wa Mkutano  wa  69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoanza wiki ijayo.

Akizungumza na  waandishi wa habari hapo siku ya  Jumanne, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki Moon, amesema,  viongozi hao pamoja na  kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia hivi sasa,  watautumia mkutano huu kujadiliana kwa kina kuhusu  mchango na ushiriki wa jumuiya ya kimataifa katika kuukabili  mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete  ni
miongoni wa viongozi hao 140 na anaongoza 
ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu.

 Akizungumzia zaidi kuhusu mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola na athari zake kwa uhai wa mwanadamu na kwa maendeleo ya  kiuchumi na kijamii,   Ban ki Moon amewaeleza  waandishi hao, kuwa Jumuiya ya kimataifa haiwezi kuendelea kuufumbia macho na kwamba kadiri inavyochelewa kuutafutia ufumbuzi ndivyo hatari yake inavyozidi kuongezeka.

“Tutatoa kipaumbele cha peke kuhusu ugonjwa wa Ebola ambao umeleta athari kubwa kwa baadhi ya nchi za Afrika ya Magharibi na maeneo mengine. Siku mbili zijazo (Alhamisi) Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana kwa dharura kuzungumzia mlipuko wa Ebola.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Margaret Chan na Mimi tutazungumza katika mkutano huo” akasema Ban Ki Moon.

Akaongeza kwa kusema wiki ijayo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa litakuwa na mkutano wa kilele kuhusu mahitaji ya watu na nchi zilizokabiliwa na ugonjwa wa Ebola. Pamoja na  kujadili na kutafuta mkakati wa pamoja wa kukabiliana na Ebola,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  anasema viongonzi hao wakuu wa nchi na serikali pia wanatarajiwa  kujadili na kubadilishana  mawazo kuhusu changamoto za mabadiliko ya tabia nchi katika  mkutano utakaofanyika septemba 23.

Mhe. Rais Jakaya  Kikwete ni kati ya  Viongozi walioalikwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  kuhudhuria na kuzungumza katika mkutano huu
muhimu kuhusu  suala zima la mabadiliko ya tabia nchi na  athari zake.

Akielezea zaidi kuhusu mkutano huo wa mabadiliko ya tabianchi, Ban Ki Moon anasema mkutano huo utakuwa na malengo mawili, kwanza ni ukusanya utashi wa kisiasa  ili kufikia makubaliano ya pamoja hapo mwakani katika mkutano utakaofanyika huko Paris , Ufaransa. Na pili kuchukua hatua madhubuti za kupunguza uzalishaji wa gesi chafu.

Akiainisha zaidi  kuhusu ajenda mbalimbali zitakazojadiliwa wakati wa Mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa,  Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, amesema,   majadiliano ya Baraza Kuu (General Debate) yatakayoanza septemba 24   yatatumika  kukusanya nguvu za pamoja za  kuushinda umaskini, na kupitisha ajenda za malengo mapya ya maendeleo endelevu .Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya  Mrisho Kikwete atalihutubia Baraza Kuu Septemba 25.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati) akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy nchini, Philippe Corsaletti (kulia) baada ya kupokea hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 40 msaada uliotolewa kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo, jijini Arusha. Kushoto
ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ukumbi mdogo wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea hundi ya Sh. Milioni 40 kwa ajili ya maandalizi ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy nchini, Philippe Corsaletti (kulia). Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inatarajiwa kufanyika wiki ijayo, jijini Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ukumbi mdogo wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima (katikati) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea hundi ya Sh. Milioni 40 kwa ajili ya maandalizi ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy nchini, Philippe Corsaletti (kulia). Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inatarajiwa kufanyika wiki ijayo, jijini Arusha. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ukumbi mdogo wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI