001: Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimsikiliza kwa makini Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa (kulia) muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya utiaji saini mikataba ya usambazaji huduma za mawasiliano ya simu za mkononi maeneo ya vijijini kati ya makampuni ya simu na Mfuko wa Wamasiliano kwa Wote - (UCSAF) jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasilano wa Airtel Beatrice Singano.
 Mkuu wa Idara ya Sheria wa Vodacom Ngayama Matongo akimuongoza Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Georgia Mutagahywa (aliyeketi) kutia saini mkataba wa makabaliano ya usambazaji huduma za mawasiliano vijijini kupitia ruzuku ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam. Wa pili kulia aliyesimama ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa akishuhudia. Vodacom kupitia mfuko huo itafikisha huduma kwenye kata 37 za pembezoni mwa miji na yenywe ikiahidi kufikisha huduma kwenye kata 36 za pembezoni kwa gharama zake ili kuwawezesha watanzania wasihia vijijini kuunganishwa kwenye mtandao wa huduma za simu za mkononi.
Kutoka kulia Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Georgia Mutagahywa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Kamugisha Kazaura na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Peter Ulanga wakitia saini makubaliano yanayayawezesha makampuni ya simu kupokea ruzuku kwa ajili ya kufikisha huduma kwenye maeneo yaliyo pemebezoni na miji kadiri walivyoomba. Vodacom imeahidi kufikisha huduma hiyo kwenye kata 73 kati ya hizo 37 kupitia ruzuku YA UCSAF.
 Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Georgia Mutagahywa kulia akibadilishana nyaraka za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Kamugisha Kazaura zinazohusiha upokeaji wa ruzuku kwa ajili ya kufikisha huduma za mawasiliano vijijini inayotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).Wa kwanza kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Peter Ulanga akisainia makubaliano hayo. Vodacom imeahidi kufikisha huduma kwenye kata 73 zilizopo vijijini kati ya hizo 37 kupitia ruzuku hiyo. Wa pili kulia waliosimama ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa.
Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania wa kwanza kulia na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Kamugisha Kazaura (katikati) wakipitia kwa umakini mikataba kati ya makampuni yao na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inazoziwezesha kampuni hizo kupokea ruzuku kusaidia usamabzaji wa huduma za mawasiliano ya simu vijijini. Wa kwanza kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Peter Ulanga akitia saini makubaliano hayo. Vodacom imeahidi kufikisha huduma hiyo kwenye kata 73za vijijini kati ya hizo 37 kupitia ruzuku ya UCSAF.
Majibu ya Meya wa Manispaa ya Ilala, Mh. Jerry Silaa kuhusiana na sakata la kumtukana Mh. Lowassa. 

Kwa mujibu wa ukurasa wa Facebook wa Mh. Silaa alisema amepokea kwa Masikitiko makubwa taarifa zinazosambazwa mitandaoni ikidaiwa ni mawasiliano baina yangu na Ridhiwani Kikwete, Mjumbe wa NEC na Mbunge Mteule wa Jimbo la Chalinze, Pwani.

Ingawa si tabia yangu kukanusha mambo yaliyotengenezwa kwa sababu anazojua muandaaji lakini kwa idadi ya simu nilizopokea kwa faida ya wengi ni bora niseme yafuatayo;-

1.Kwa wanaofahamu matumizi ya Whatsapp, Screenshot hii ilipaswa kutoka kwenye simu yangu, kwa maana nyingine ni mimi mwenyewe ndiye chanzo cha jambo hili.

2. Wanaonifahamu Whatsapp sio moja ya njia yangu ya mawasiliano, situmii simu aina ya Samsung ambayo ndiyo inayoonekana ilikuwa inatumika katika mawasiliano hayo na pia siifahamu na wala sijawahi kuwa na namba ya Airtel ya Ridhiwani.

3. Ukiiangalia Lugha na aina ya uchaguzi wa maneno uliotumika si aina yangu ya uandishi na maneno hata ambayo huwa nayatumia katika mazungumzo ya kawaida, mtu yoyote anayejua siasa atatambua mazungumzo hayo hayana mantiki yanaongelea mambo mengi na watu wengi kwa wakati mmoja.

4.Mnamo Aprili 5, nilikuwa kwenye (Hall of Fame) Chuo Kikuu, Mzumbe na si Chalinze nilikokuwa tarehe 2,3 na 7. Muda wa ujumbe unatofautiana sana 5am, 6:30am na 2:32pm. Ujumbe uliopigwa picha (Screenshots) zinaonyesha kwamba majadiliano hayo yalifanyika Aprili 5 ambayo mimi nilikuwa tayari Chuo Kikuu, Mzumbe. Mimi niliondoka Dar kwenda Chalinze rasmi siku ya Aprili 2 nikitokea katika shughuli za ugawaji wa madawati katika shule ya Sekondari Pugu jijini Dar es Salaam ambapo nilikuwepo huko tangu asubuhi bila kupitia sehemu yoyote na niliongozana na MNEC, Anthony Mavunde kwa kupitia njia ya Kisarawe ili kukwepa foleni. Na Aprili 7 nilienda tena Chalinze, Pwani kusherehekea ushindi.

5. Jambo hili ni rahisi sana kulitengeneza kwa simu mbili na kusave majina unayotaka na unawezo hata wa kutoa ya upande wa pili inayoonyesha jina langu. Matumizi haya ya teknolojia ni vyema yatumike katika mambo ya msingi badala ya kujaribu kuleta fitna zisizo na maana na kujaribu kuwapa watu tabia ambazo hawajawahi kuwa nazo.

6. Ushauri wangu ni kwa kila mmoja wetu hasa wanasiasa kuwa makini na kuepuka kufitinishwa kwa fitina nafuu kama hii. Kwa jambo lilozungumzwa kwanza wakati bado na pili wanasiasa wa ngazi yangu na Ridhwan si wakulijadili jambo kubwa namna hiyo kwa hoja dhaifu hivyo na tena kwenye whatsapp.

JERRY SILAA.
----
Inadaiwa huu ndiyo ujumbe mfupi uliopatikana wakiwa wanawasiliana Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwan Kikwete na Mh. Jerry Slaa.
SAKATA LENYEWE NDILO HILI AMBALO MH. JERRY SLAA KAJIBU;
Ofisa utumishi Mkuu Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bwana Godfrey Mugomi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa hoteli ya kisasa STAR CITY HOTEL iliyopo Afrikasana, Sinza wanaoshudia ni Mkurugezi mkuu na mmiliki wa hoteli hiyo, Bwana Obadia Mtewele na Mkewe Joyce Msigwa. Hoteli hiyo ya kisasa ina uwezo wa kupokea wageni kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi.
 Muhudumu aliyefuzu katika kazi za Hoteli akiandaa vyombo kwa ajili ya wageni.

Karibu katika mazungumzo na Dr Patrick Nhigula kuhusu mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba na mwenendo mzima wa nchi ya Tanzania.

Huu ni mfululizo wa mazungumzo na watu mbalimbali kuhusu suala hili muhimu kwa mustakabali wa nchi ya Tanzania. Karibu

Kwa maoni, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe kwanzaproduction at gmail dot com
Mrembo Wema Isaac Sepetu 'Beautiful Onyinye' akiwa na tuzo yake baada ya kuibuka Ijumaa Sexiest Girl 2013/14 ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Wema akiwashukuru mashabiki wake waliompigia kura na hatimaye kuibuka mshindi.
...Akiwapa tano mashabiki waliofurika Dar Live katika Sikukuu ya Pasaka.
Wema, Wema, Wema... mashabiki wakimshangilia 'Beautiful Onyinye' baada ya kutangazwa mshindi.
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa lililokuwa likiendesha shindano la Ijumaa Sexiest Girl, Amran Kaima (kulia) akipozi na mshindi Wema Sepetu. Kushoto ni shabiki wa Wema.
Mashabiki wakiwa wamepagawa na shangwe za Dar Live.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho akiongea machache kabla ya zoezi la utoaji tuzo.
Msanii kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili akimtaja mshindi.
Nikki wa Pili akimkabidhi tuzo ya Ijumaa Sexiest Girl, mrembo Wema Sepetu.
Wema akipozi na tuzo yake.
Wema akicheza wimbo wa Number One ulioimbwa na mpenzi wake Diamond Platnumz baada ya kutwaa tuzo.
Washereheshaji katika usiku wa Pasaka, Pamela Daffa na Benjamin Mwanambuu wakifanya yao stejini.
Said Fella (wa pili kushoto) akiwa na crew ya Madj ndani ya Dar Live.Dogo Aslay akiwapagawisha mashabiki wa burudani waliofurika ndani ya Dar Live.
...Aslay akijiachia na shabiki wake aliyepanda stejini kumpa sapoti.
Chegge Chigunda 'Mtoto wa Mama Said' akizikonga nyoyo za wana Dar Live.
TMK Wanaume Family wakizidi kulishambulia jukwaa la Dar Live la kupanda na kushuka.
Wana Hip hop wa Kundi la Weusi, Joh Makini (kulia) na G-Nako wakiwapa raha mashabiki.
Mashabiki wakifuatilia shoo ya Weusi.
Joh Makini kazini.
G-Nako akiwadatisha wapenzi wa Hip hop.
Kaimu Mhifadhi wa Mbuga ya Ngorongoro, Bw. Amio Amio ambaye aliyemwakilisha mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mbio za Tigo Ngorongoro zilizofanyika jana Aprili 19, 2014 kuanzia Mbuga ya Ngorongoro na kuishia mjini Karatu akiongea machache wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi zawadi zao. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Kanda wa Kampuni ya simu ya mkononi ya TIGO, Brian Kalokola.
Kaimu Mhifadhi wa Mbuga ya Ngorongoro, Bw. Amio Amio (kushoto) na Mkurugenzi wa Kanda wa Kampuni ya simu ya mkononi ya TIGO, Brian Kalokola (kulia) wakimkabidhi zawadi ya shilingi Mil. 1 mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 22 (Half Marathon) kwa upande wa wanaume, Alphonce Felix mara baada ya kunyakua taji hilo kwa kuvunja rekodi kwa kukimbia muda wa 1:03:59. Mbio hizo za Tigo Ngorongoro zilifanyika jana Aprili 19, 2014 kwa kuanzia geti kuu la Mbuga ya Ngorongoro na kuishia mjini Karatu. Tigo ndiyo walikuwa ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo,
 Mkurugenzi wa Kanda wa Kampuni ya simu ya mkononi ya TIGO, Brian Kalokola (kulia) akimkabidhi zawadi ya shilingi Mil. 1 mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanawake, Jackline Sakilu mara baada ya kunyakua taji hilo kwa kuvunja rekodi kwa kukimbia muda wa 1:14:29.
Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Riadha Tanzania, akitoa zawadi kwa Fabian Joseph aliyeshika nafasi ya nne,
Mwakilishi wa kampuni ya Utalii ya ZARA ambao ndiyo waandaaji wa mashindano hayo akitoa zawadi kwa mshindi wa saba kwa upande wa wanawake.
Washindi wa Mbio za Tigo Ngorongoro upande wa wanawake wakiwa wamejipanga kusubiri zawadi zawadi zao… kutoka kulia mshindi wa kwanza Jackline Sakilu, Nathalina Elisante, Marry Naali, Failuna Abdi na Flora Yuda.
Wanariadha wa Mbio za Tigo Ngorongoro Kilometa 21 (Half Marathon) wakianza mbio katika geti kuu la Mbuga ya Ngorongoro na kuishia mjini Karatu.
Mchuano wa wanariadha ukiendelea kwa kasi.
Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kila mmoja akitaka kuchomoza ili aweze kushinda.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanaume, Alphonce Felix akiwachomoka wenzake.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanaume, Alphonce Felix akimaliza kwa furaha.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanawake, Jackline Sakilu akimaliza mbio.
Umati wa Wakazi wa Mji wa Karatu wakifuatilia michuano hiyo.
Hapa ndipo kulipoanzia kwa mbio za makampuni... ambapo makampuni yalikimbia kilometa 5.
Mshindi wa kwanza wa mbio za makampuni akifurahia mara baada ya kumaliza.
Mkururenzi Mtendaji wa Kampuni ya Frontline Porter Novelli, Irene Kiwia hakuwa nyuma kushiriki mbio hizo.
Washiriki wa Mbio za Tigo Ngorongoro Kilometa 5 za Makapuni wakimenyana vikali.
Timu ya Kampuni ya Frontline Porter Novelli ya jijini Dar es Salaam wakiwa katika sura ya furaha mara baada ya kumaliza kukimbia Kilometa 5 katika Mbio za Tigo Ngorongoro.